JICHO LA NGAMIA
MAHITAJI YA KUPIKA JICHO LA NGAMIA
- Unga ngano mweupe - vikombe 2 ½
- Unga wa mahindi (sembe) - kikombe 1
- Sukari laini kabisa (isage) - kikombe 1
- Baking powder - kijiko cha chai ½
- Siagi laini - gms 250
- Mayai - 2
- Vanilla - kijiko cha chai 1
- Chumvi - chembe
- Unahitaji kuwa na mashine hasa ya kupikia biskuti hizi za jicho la ngamia
JINSI YA KUPIKA JICHO LA NGAMIA
1. Changanya vizuri siagi, sukari kwa mchapo wa mkono kisha changanya mayai.
2. Tia pole pole unga na vilobakia uchanganye vizuri. Mchanganyiko usiwe laini sana yaani usiwe maji maji.
3. Washa mashine ishike moto.
4. Kisha fanya vidonge vya round vidogodogo.
5. Weka vidonge katika mashine ya Jicho la Ngamia.
6. Funika upike kiasi ya dakika 10 au chini yake.
7. Tumia kijiti kirefu cha mishkaki kutolea. Epua vibiskuti.
8. Rudia kumalizia kupika vidonge vyote.
9. Vikishapoa, jaza baina ya biskuti mbili kwa caramel au tofi ugandishe.
CARAMEL AU TOFI ZINAPATIKANA KATIKA VIUNGO VIFUATAVYO:
- *•Utengenezaji Wa Caramel Ya Sukari Na Maziwa ya Malai Whipping Cream.
- *• Utengenezaji Wa Caramel Au Tofi Kwa Maziwa Mazito.
10. Pangusa caramel iliyozidi kisha viweke kila kimoja katika kijikaratasi chake na upange katika sahani ya kupakulia.
11. Ukipenda saga aina za njugu unyunyize pembezoni.
VIDOKEZO
1. Andaa caramel mapema kabla ya vibiskuti ipate kupoa.
2. Unaweza kutumia sosi ya tayari inayouzwa katika chupa mfano ‘nutella’ badala ya kuandaa caramel.
3. Ukipenda kuzifanya za rangi mbali mbali au za chokoleti, basi gawa unga usarifu upendavyo.
4. Caramel hizo za kuandaa mwenyewe unaweza kutumilia katika mapishi mengineyo kama keki, biscuit, kaimati, sharbaat n.k
MAHITAJI YA KUPIKA CARAMEL
- Sukari ya brown (brown sugar) - 100 gms
- Siagi - 100 gms
- Cream au maziwa mazito -100 ml
JINSI YA KUPIKA CARAMEL
1. Weka siagi na sukari katika sufuria ndogo au frying pan, weka katika moto ukoroge mpaka siagi na sukari iyayuke. Isiungue.
2. Tia maziwa ya cream uendeleze katika moto itatoa povu, changanya na koroga vizuri usiache mkono.
3. Epua ikiwa tayari ihifadhi katika chupa ya glass.