SAFARI YA KUZIMU EPISODE YA KWANZA
MTUNZI. OPPAHNO.0678635182
Mussa mwanangu nimekwambia mara ngapi urithi mikoba yangu ya uchawi. hapana mama sitoweza kuwa mchawi kamwe,kitu hicho ndo umeniitia toka dar mpk huku sumbawanga ngoj nirudi zangu dar ila siwez kuwa mchawi kamwe mama. unajifanya umekua mbwa ww sasa subir nntakufundisha adabu. aliongengea mama huku sura yake akiwa ameikunja lakn sikujali
nilikusanya kilicho changu na kuanza safar ya kurud dar baada ya kuona mama ana mambo ya ajabu sana. nilianza safar ya kuelekea stend lakn nikiwa njian kila mtu niliepishana nae alionyesha hali ya kunisikitikia na wengne mpaka wanalia nijiuliza lakn skupata jibu.
nilipofika stend nilimpigia simu mke wangu na kumwambia kuwa narud. alihoji mbon umeenda jana alaf unarud leo si ulisema unakaa mwezi nikamwambia tu mambo yameingiliana na bosi ananitaka kazini alisema sawa mme wangu nakusubir.
nilipomaliza kuongea na mke wangu nilimuona kuna bibi kizee aliesimama upande wangu wakushoto alikuwa akilia machozi huku akiniangalia lakn sikutilia maanani sana nilijua tu analia na shida zake looooh kumbe ningejua??????
nilipanda gari na safari ilianza kutoka sumbawanga kuja dar nikiwa na abiria wenzangu kutokana skukata tiketi ilibidi nitoe hongo kwa utingo na utingo alikubali na nilifanikiwa kupata siti ambayo nilikuwa nimekaa na mama fulani aliekuwa na kitoto kichanga yule mtoto baada ya kuniona mm alianza kulia kilio cha nguvu mpaka mama mtu akaduwaa kwan mwanae hakuwa analia kabla baada ya kuniona mm ndo kilio kikaanza
lakn akambembeleza na akalala
baada ya mwendo kama wa nusu saa hv nilijikuta nikipitiwa na usingizi na nilianza kuota ndoto mbaya niliota mama akiwa na wachawi wenzake huku mama akiongea MUSSA MUSSA!!!!!! NGOJA NIKUFUNDISHE MWANAHARAMU WEWE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
SAFARI YA KUZIMU SEHEMU YA PILI
tulipoishia namba moja. nikiwa kwenye gari niliota ndoto mbaya sana niliota mama yupo na wachawi wenzake na akinimbia MUSSA MUSSA NGOJA NIKUFUNDISHE MWANAHARAMU WW!!!!
sasa endelea
Nilishtuka baada ya kelele za watu zikipiga kwa nguvu kwani kila mtu alikuwa analia wakati ule nilinyanyuka na kumfata mmoja kati ya abiria wenzangu na kumuuliza kwan kuna nini lakini cha ajabu sjui alikuwa anafanya kusudi lakin hakuweza kunijibisha nilijaribu kumshika lakn hakuonyesha hali yeyote ya kushikwa na mtu
punde si punde watu walijaa eneo lile lakin cha ajabu kila niliemshika nimuulize kuna nn alikuwa hanisikii wala hanioni nilisogea mbele nikakuta watu wakililia viungo vyao hapo ndo nilipogundua kuwa tumepata ajar nikajiuliza mbona mimi ni mzima lakin kila nnaemuongelesha hana habar na mimi???
nilisogea mbele kidogo laaaaaaa haulaaaaa mungu wangu!!!!!!! nilishangaa baada ya kuona mwili wangu ukiwa umelala chini duuuuh ina maana nimekufaaa?????? aaaaaaaah nililia kwa uchungu lakini hakuna alieskia. nilienda mpaka pale ulipo mwili wangu niliugusa lakini niliona kama nimegusa kitu mithili ya gogo maana ulikuwa ni mgumu bas nilibaki nikiwa nalia bila ya mafanikio
punde si punde niliona kundi kubwa la wachawi likiongozwa na mama yangu lilifika sehemu ile na kuanza kuchukuwa miili ya watu waliokufa! asikwambie mtu kwa macho ya kawaida huwez ona nini kinaendelea maana ake watu wanaona ni miili lakin huwa yanaachwa magogo tuuh! mara wakaja wakanikamata na mimi na ckujua nini kinaendelea lakin nilishtuka nipo nyumbani kwa mama nikiwa kwenye chumba kimoja wapo cha nyumbani niligeuza macho nijue nini kinaendelea niliwakuta watu wengi wakiwa kwenye hali ya uzezeta yaani misukule
nikajiuliza mama ameniweka msukulee mimii. MAMA MAMA MAMA!!!!!!!!!!!!!!!
SAFARI YA KUZIMU EPISODE YA TATU
Tunaanza tulipoishia sehemu ya pili
NILILIA KWA UCHUNGU MAMA MAMA MAMAAA!!!!!!!!!!!!!
Tuendeleeni
nililia kilio kisicho na kifani ila watu wa mule ndani hawakuonyesha hali yeyote ile ya kusikitika wala kufurahishwa kutokana walikuwa mazezeta kabisa na walikuwa wakitokwa na udenda mda wote.nikiwa kwenye hali ile mara mlango ulifunguliwa alikuwa ni mama aliefungua mlango na alikuja na ndoo ya unga.
wale misukule baada ya kuona ule unga walianza kucheza huku wakionyesha kama ishara ya kushangilia nilijiuliza lakn sikupata jibu ndipo mama akaiweka ile ndoo chini nilishtukia nipo chini baada ya kupigwa kikumbo kizito loooh kumbe jamaa ulikuwa ndo msosi wao??? nilishindwa kula unga tena mkavu kabisa lakin jamaa waliona kama wali dakika tatu tu misukule ilimaliza ule unga wote uliokuwa kwenye ndoo nikajiuliza maisha yangu yote yatakuwa kwenye hali hii?? stokubali nitapambana mpaka nitoke kwenye hii dunia mbovu
nilishushwa na sauti kali ya mama ikisema wewe s umejifanya mshenz eeeh ngoja tukufundishe na leo mke wako christina anakuja ili kesho tukakuzike na tukimaliza tu hivyo maisha yako yote yatakuwa kama hawa wenzako mpaka siku tutakutoa kafara. mama kwani nini nimekukosea kumbuka nina watoto wawili na mke wangu christina wote wananitegemea mimi mama ukifanya hivyo unafkiri wataishije wanangu pamoja na mama yao kama nntakuwa hivi niliongea huku nikilia machozi lakini mama hakujali hilo alifunga mlango na kuondoka na zake
nilikaa kwa mda mrefu kidogo ndipo mlango ulifunguliwa tena alikuja mama na kunishika mkono na kunitoa nje looooooh nilikutana ana kwa ana na mke wangu christina pamoja na watoto wangu niliita CHRISTINAAAA!!!!!
nilimuona akigeuka nyuma.....
SAFARI YA KUZIMU EPISODE YA NNE
tulipoishia episode ya tatu
nilimuona mke wangu christina akiwa na watoto wangu niliita kwa sauti CHRISTINAAAAAA!!!! aligeuka nyuma na
sasa tuendelee
aligeuka nyuma christina lakin cha kushangaza hakushtuka kama kaona mtu japo nilikuwa karibu nae. mama alimuuliza vip mkwe mbona naona kama umeshtuka na kugeuka nyuma alijibu niliskia sauti kama ya mtu ikiniita kwa nguvu. lakin mama alimtoa hofu na kumwambia aaah unaweza ukawa labda hauko vizur kutokana na matatizo yaliyokusibu kwa hiyo ukiwaza sana utajikuta ndo kama hivyo yanavytokea
Loooooooh!!! angejuaa
Ratiba ya mazishi ilipangwa na kuwa kesho yake ndipo nntaenda kuzikwa nilikuwa nalia kutokana niliskia kila kitu kilichoongelewa. lakin mama mbona tunaenda kuzika mapema hivyo s tungesubir kidogo aliuliza mke wangu mama alijibu hapa hakuna cha kusubir kesho tutaenda kuzika aliongea kama anafokea. sawa mama nimekubali aliongea mke wangu akionyesha kukubl
usiku ulipofika mama alitoka ki uchawi pamoja na misukule wote kwenda katika mikutano yao. jamani kesho tunaenda kuzika na tukimaliza kuzika huyu atakuwa msukule wetu na atakuwa wa kwanza kutolewa sadaka kwa mkuu wetu ambae tutamualika katika sherehe hii ya kafara aliongea mama huku akiwa mkavu hacheki. mmoja wa wachawi alihoji lakini mkuu tunasiku nyingi sana hatujala nyama ila siku hiyo ya kafara itakuwa vizuri sanaa. weweeeeeeh wachawi walishangilia na ngoma kuanza kupigwa walicheza uchi kabisa.
Asubuhi ilifika na maandalizi ya msiba yalianza muda huo mama alijifanya akilia kwa unafki mke na watoto wangu walilia sana. nilisimama mlangoni nikiona kila kitu kinachoendelea
kuna mzee mmoja aliniona sijui alianza kumtukana mama. wewe mama mpumbavu kabisa unamuweka mwanao msukule shenzi kabisa unafikiri watu hatuoni au kama kuna mtu anataka aone dawa hii apa njoo nikupakae muone mtoto yule alinyoosha kidole palepale nilipo!
je nini kitafuata usikose