MPIGA PICHA SEHEMU YA NANE
Tatizo lililokuwa limebaki na kunisumbua kichwa lilikuwa ni moja tu. Kila siku wazazi walikuwa wakinitaka nioe. Ili nipate msaidizi. Na pia walikuwa wakidai wanataka wanione mwanao nikifunga ndoa na zaidi pia wawaone wajukuu zao ambao nitawazaa baada yakuwa nimeoa.Maneno yale ya wazazi yalinifanya nimuwaze sana Harriet. Kimbilio langu niliona ni harriet. Ukizingatia tiali nilikuwa nisha zama katika penzi la msichana wa kihehe, Harriet. Harriet ni msichana mzuri kwa mwonekano. Rangi ya chungwa. Umbo zuri, hakika kajariwa kila idara. Moyoni na akilini mwangu niliamini kuwa nimepata mke wa kuishi nae. Nilifanya mipango kisha nikaenda kumtambulisha kwetu.
Baada ya kumtambulisha Harriet kwa wazazi wangu. Wazazi wangu hawakuafiki na hawakupenda mimi nimuoe Harriet. Mama ndiye haswa hakuwa akimpenda wala kumuitaji Harriet.
"Mwanangu Lucas huyo sio mwanamke... hakufai baba tafuta mke mwingine huyu hakufai atakutesa bure mwanangu." Aliongea mama pindi tulipokuwa wawili mimi na yeye. Japo hakutaka kuniambia hasa nini chanzo na tatizo la yeye kutotaka mimi nisimuoe Harriet. Harriet alikuwa msichana aliekuwa ya sana akili yangu kutokana na uzuri wake. Harriet alikuwa na uzuri wa aina yake. Hakuna mwanaume ambaye angekataa kumuoa Harriet. Kwa uzuri aliokuwa nao. Harriet alikuwa anavutia kweli kweli.
Siku zote nilifanya siri sikutaka kumwambia Harriet kuwa mama yangu hajapendezwa na mimi kumuoa Harriet.
"Mama naomba umpokee tu mimi nishampenda."
"Sijui kwa nini lakini mwanangu Lucas umekuwa king'ang'anizi kiasi hiki. Au tiali mwenzetu ushalishwa limbwata nini?" Mama alizungumza
"Limbwata wapi mama.....! Nimetokea tu kumpenda."
"Mmmmmh..... umemchunguza lakini maana hujui amekulia familia gani?"
"Mama Harriet ni mwanamke mzuri sana si sura tu hata tabia. Ni miaka miwili nimekuwa nae kwenye mahusiano. Namjua nje ndani." Nilimwambia mama huku nikimkazia macho.
"Mwanangu Lucas najua hujui vitu vingi kuhusu wanawake. Nakuomba mwanangu kuwa makini. Pamoja na hayo yote kaa ukijua kuwa sio kama mimi mama yako labda simpendi mpenzi wako. Hapana. Lakini nawasi wasi nae sana, moyo wangu haujalizika kabsa. Kuna kitu..... kunakitu mwanangu kuwa makini." Aliongea mama huku akionesha wasiwasi.
***************
*****
Baada ya miezi mitatu Harriet alikuwa mmoja wa wanafamilia katika familia yetu. Harriet alikuwa mke wangu japo hatukuwa tumefunga ndoa. Mama hakuwa akionesha chuki yeyote kwa mke wangu. Miezi ilizidi kwenda Harriet akiwa mwenye tabia njema, kitu ambacho kilifanya mpaka mama anze kumpenda. Miezi hii tukiwa tunaishi na Harriet familia nzima ilikuwa inampenda. Harriet alikuwa mshauri mzuri, mwanamke mwenye upendo, kujali na kuwathamini wengine.
Miezi miwili badae tuliamua kuhamia katika nyumba ambayo nilikuwa nimenunua kwa pesa zangu. Tulianza maisha mapya mimi na Harriet. Harriet akuwa akifanya kazi tena alikuwa mama wa nyumbani. Rafiki zangu, ndugu na jamaa mbali mbali walimtambua Harriet kuwa ndie mke wangu.
"Harriet your so beautiful najivunia kuwa na mke kama wewe." Nilimwambia Harriet huku nikiwa nimemkumbatia asubuhi ile kabla sijaenda kazini.
"Nakupenda pia mme wangu. Nashukuru Mungu kunikutanisha na wewe........" Alinijibu Harriet huku akiwa anaendelea kunifungia vizuri tai shingoni.
"Bebie nikwambie kitu?" Aliongea Harriet
"Nakusikiliza mke wangu niambie....."
"Lini na mimi nitarudi kazini..?, au wewe unapenda mkeo niendelee kuwa tegemezi tu. Mimi sifurahi bwana kuwa golikipa." Aliongea Harriet.
"Mmmmh...! usijali mpenzi kazini utarudi nataka nifanye mpango nikufungulie kabsa duka lako." Baada ya kumwambia vile Harriet alitabasamu kisha akanibusu mdomoni.
"Nitafurahi sana mpenzi wangu."
"Usijali mama....... afu nimekumbuka kweli Ulisema wewe mshabiki wa mpira wa miguu sio?"
"Ndio mi nashabikia Man u na Yanga."
"Unaanza vipi kushabikia Man united na wewe. Bora Yanga hapo umetaja timu ya maana na sio hao mashetani wekundu siwapendi kama nini?"
"Huwapendi eeee..... utatupenda tu mwaka huu.!!!"
"Aaaa.... wapi kwanza ushaniuzi. Nilikuwa nataka nikwambie kitu nimeailisha." Nilimwambia Harriet huku nikianza kuondoka.
"Lucas....." aliniita Harriet nilisimama na kugeuka kumwangalia.
"Umesahau kamera." aliongea Harriet huku akiniletea.
"Asante wangu.... jiandae jioni nakuja kukupitia twende mpirani leo Yanga anacheza na Toto Africa." Nilimwambia mke wangu kisha nikafungua mlango a kutoka kuelekea kazini.
***************
**
Saa tisa alasiri tulikuwa kwenye lango la uwanja wa Ccm Kirumba tukiingia uwanjani.
"Hii Lucas...." sauti ilinisemesha na kunifanya nigeuze shingo kumwangalia ni nani alikuwa akinisemesha.
"Oooooo....... !. Zacharia......... ni wewe rafiki yangu." Niliongea baada ya kumtambua aliekuwa akinisemesha.
"Ni mimi kaka.. za siku?"
"Njema sana Mungu anasaidia, umepotea sana rafiki yangu."
MPIGA PICHA SEHEMU YA TISA
"Maisha kaka si unajua kutafuta ugali. Huwezi kutulia tu nyumbani ugali ukaja.""Ni kweli kabsa." Niliongea huku tukikaa katika moja ya jukwaa mle uwanjani.
"Na huyu vipi kaka ndio shemeji nini?"
"Yeah huyu ndio shemeji yako anaitwa Harriet." Nilimtambulisha Harriet kwa Zacharia kisha nikahamia kumtambulisha Zakaria kwa Harriet
"Babie huyu ni rafiki yangu toka tukiwa watoto wadogo, tumecheza pamoja tumesoma pamoja... anaitwa Zacharia." Utambulisho huu uliwafanya Harriet na Zacharia washikane mkono.
"Nafurahi kukutana na wewe shemeji." Aliongea Zacharia
"Asante shemeji karibu nyumbani." Aliongea Harriet.
"Nitakaribia" alijibu Zacharia.
Tuliendelea kuangalia mpira mpaka dakika tisini zikaisha. Tuliagana na Zacharia kisha mimi na mke wangu Harriet tukaenda nyumbani.
Maisha yalizidi kwenda huku penzi letu likizidi kupamba moto. Hatukupanga kupata mtoto tulisubili tujipange vizuri tufunge ndoa ndio tuanze harakati za kutafuta mtoto.
Baada ya miezi miwili hatimae nilimfungulia Harriet biashara. Alikuwa akiuza duka la nguo kama alivyokuwa akifanya mwanzo. Upendo ulizidi kukolea mara dufu.
***************
**
Kuna misemo mingi ya kiswahili ambayo inamana kubwa sana katika jamii. Mkomboe mwanamke ukomboe dunia. Msemo huu uligeuka na kuwa mchungu kwangu. Ndio ulipoelekea maisha yangu kuyumba na kuingia katika mkasa mkubwa, mkasa wakuishi maisha ya kujificha kama digidigi kwenye nyika lililotawaliwa na simba wakari.
Mwanzoni nilijua kuwa kumwezesha Harriet kwa kumwanzishia biashara, itachangia maendelea katika familia. Sikujua kama nilikuwa naharibu uhusiano wetu.
Maisha yalizidi kwenda. Nilifurahi sana kuona mke wangu mpenzi Harriet akiwa anafanya biashara yake kwa uhuru. Sikuwa namuingilia katika biashara yake, pasipo yeye kunishirikisha na kunipmba msaada.
Harriet alikuwa mwanamke anayejituma katika kufanya biashara.
Jioni baada ya mihangaiko yangu nilirudi nyumbani. Nilipofika nilimkuta Harriet kashafika mapema. Nilifungua mlango na kuingia ndani. Harriet baada ya kuniona alinyanyuka toka kwenye sofa ambalo alikuwa ameketi na kuja kunipokea. Alifika na kunikumbatia huku akinipa pole za mihangaiko.
"Lucas mpenzi mzigo umeisha fanya mpango umtume yule jamaa yako anaetuleteaga mzigo atuletee mwingine." Aliongea Harriet
"Umeisha na kuisha.....!" Niliongea huku nikionesha kushangazwa na taarifa zile. Maana mzigo ulikuwa haujamaliza hata wiki mbili.
"Ndio... zimebaki chache sana naimani nazo kufikia kesho zitakuwa zimeisha."
"Aaaaa.... oooo usijali mpenzi ngoja nifanye mawasiliano naye usiku huu ikiwezekana kesho autume." Nilimwambia Harriet ambae alikuwa amelishika koti langu mkononi. Nilimuacha Harriet pale mlangoni akichukua viatu vyangu kisha mimi nilielekea chumbani.
Nilifika chumbani na kukaa kitandani kisha nilichukua simu yangu na kutafuta namba ya jamaa yangu ambaye huwa ananiletea mzigo.
Baada ya simu kupokelewa maongezi yalifata. Na kisha tukafikia makubaliano kuwa mzigo ungetumwa kesho kutwa. Kisha nikakata simu.
***************
**
Siku tatu zilipita bila mzigo kutumwa. Huku jamaa yangu ambae huwa ananiletea mzigo akizidi kunipa promise kuwa mzigo upo njiani. Hatimae wiki ilikatika bila mzigo kufika. Kipindi chote hichi Harriet alikuwa haendi tena kazini maana hakuwa na kitu cha kuuza dukani kwake.
"Huyu jamaa naona kashindwa kazi.... kashindwa kazi kabasa. Sasa chakufanya sijui utaweza. Lakini nakuamini jembe langu utaweza tu......"
"Nini hicho unataka kusema hubby." Aliongea Harriet huku akinikatisha kumalizia kuongea.
"Vipi kama mzigo ukiufata mwenyewe maana huyu jamaa haeleweki kabsa."
"Mmmmm... nitaweza kweli? Changamoto za jiji lile mimi nitaziweza?"
"Usijali utaweza tu.... mimi nina connection nyingi sana. Kuna jamaa yangu mwingine anaitwa Zacharia yupo kule hivyo hamna shida."
"Zacharia.... Zacharia yupi huyo?"
"Zacharia ambae tulikuwa tunaangalia nae mechi hapa juzi kati. Mechi ya Yanga na toto."
"Yule ambae uliniambia mmesoma nae shule moja?"
"Yeah exactly.... huyo huyo. Yuko kule anafanya kazi hii hii kama yako tena yeye yuko more advanced huwa anafata nguo nje ya nchi kisha anawaletea wale wauza maduka wa Kariakoo." Nilimwambia Harriet.
"Sasa kwanini usingemwambia hata huyo Zacharia akatuletea mzigo. " Aliongea Harriet
"Mmmm... kwa Zacharia kumwagiza ni kazi ngumu sana maana huwa anadai yuko bize sana. Hata kipindi kile alikuwa amekuja huku ilitokea tu kama bahati. Alikuwa amekuja kwenye msiba wa baba yake." Nilimwambia Harriet.
"Chamsingi kinachotakiwa wewe inabidi uende tu mpenzi. Ukachague na mzigo ambao utaenda kasi. Najua unajua nini hasa kwa wakati huu wateja wako wanapenda na wanahitaji." Nilimwambia Harriet.
Siku nzima Harriet alikuwa akifanya maandalizi ya safari. Alikuwa mtu mwenye hofu sana lakini mimi nilikuwa nikimtia moyo. Nilienda kukata tiketi kisha nikamletea.
Asubuhi na mapema nilimsindikiza Harriet katika stend ya mabasi ya nyegezi. Nilimshuhudia akipanda bus. Nilikaa pale stend mpaka bus lilipo ondoka ndipo nami nikaondoka kurejea nyumbani. Nilifika nyumbani na kujianda kisha nikaelekea kazini kwangu.
Harriet alikuwa akinijuza kila mkoa aliokuwa akifika. Mda ote tulikuwa tukichati na Harriet. Mpaka majira ya saa nne usiku alipofika Dar es salaam na kupokelewa na Zacharia.
******ITAENDELEA