MPIGA PICHA SEHEMU YA KWANZA.
Mara ya kwanza kukutana nae alinivutia sana. Siwezi kumsahau maana nilitokea kumpenda. Ni mzuri anavutia. Anasifa ya kuwa mke, na kwa mwonekano wa nje amekamilika kila idala.
Mweupe mwenye asili ya kiarabu. Nywere ndefu za shombe shombe. Pua ndefu, mrefu na si mfupi kwa kimo. Saizi ya kati na si mnene wala mwembamba kwa umbo. Kifuani alikuwa kajaa na kufanya avutie maana viembe dodo viliishika vizuri t-shet yake ya rangi nyeupe aliyokuwa amevaa. Katikati alikuwa katenganishwa vizuri na kufanya muunganiko wa umbo namba nane. Hakika alikuwa na umbo namba nane. Nyonga iliyokuwa imetanuka kwa ustadi mkubwa ilikuwa imehifaziwa ndani ya suruali nyeusi ya njinsi fulani hivi laini. Alipendeza mara dufu baada ya kutabasamu. Nilipatwa na kigugumizi kumsemesha, lakini aliponifikia alinisalimu. Sauti yake ilivutia na kufurahisha ngoma za masikio yangu. Kigugumizi kilinipata kujibu salamu yake. Japo kwa shida niliitikia salamu yake. Nilisimama pembeni nimwache apite ili nimwone kwa nyuma. Waaaaooo alikuwa kabeba mzigo wa maana. Kila alipopiga hatua nyuma kulitingishika. Haswaa..... alikuwa anapendeza kumtazama. Hakika Muumba hakukosea kuumba alimuumba haswa. Acha nimwite african beauty japo sio yule wa diamond.
Hivyo ndivyo alivyo kuwa kwa nje.
*********************************************
Usiku ulifika nilifunga ofisi yangu na kuanza safari ya kurejea nyumbani. Kutoka mahari nilipokuwa nafanyia kazi mpaka kufika nyumbani kwetu ilikuwa ni mwendo wa kama nusu saa hivi. Kwa umri wangu wa miaka 23 nilikuwa bado naishi nyumbani kwa wazazi wangu. Sikuwa nimeanza kujitegemea, na si kwamba sikuwa naweza kujitegemea. Hapana ni wazazi tu ndio walitaka niwe nyumbani mpaka mda umri ule....
Familia yetu ilikuwa ni familia ya kidini tena yenye imani haswa. Katika familia yetu tulizaliwa watoto watatu. Wa kiume wawili na wakike mmoja. Mimi kama first born. Nilipewa heshima sana nyumbani nilikuwa na uhuru wa kusikilizwa. Wa pili alikuwa mdogo wangu wakike Alice. Wa mwisho alikuwa Misago. Alice alikuwa akisoma kidato cha tano katika shule ya sekondari Ifunda girls. Huku Misago ambaye alitumia jina la babu mzaa mama alikuwa akisoma darasa la tano katika shule ya msingi ya private nje na mkoa wa Mwanza.
Baada ya kumaliza chuo kikuu na kukaa mtaani kwa mda mrefu bila kuajiriwa. Nilielekeza lawama zangu kwa wazazi hasa baba mzee Damian. Baba yangu mzee Damian ni mwalimu wa shule ya sekondari Mwenge, kwa sasa amebakiza miaka miwili astafu kazi. Mama yangu Caroline yeye ni nesi katika hospital ya wilaya Nyamagana. Baba alipenda sana mimi nisomee ualimu, japo kwa upande wangu mimi nilikuwa napenda sana kusomea mambo ya uandishi wa habari na utangazaji. Nilibadili mawazo yangu na ndoto zangu za kuja kuwa mwandishi mkubwa ama mtangazaji wa television mkubwa. Nilijikuta nikiangukia kusomea maswala ya ualimu tena ualimu wa masomo ya historia na geografia.
Mwaka mmoja baada ya kumaliza elimu yangu ya chuo kikuu kupitia kozi ya ualimu. Sikuweza kupata ajira. Mwaka na sehemu ulipita nikiwa mtaani bila ajira yeyote. Baada ya mda kupita na kuona mambo ya kusubili kuajiriwa sio sawa. Niliamua kuwekeza na kufungua ofisi yangu ambayo ilikuwa inajihusisha na k upigaji wa picha na kusafisha. Mwanzo ulikuwa mgumu lakini sikukata tamaa. Nilikuwa nikipiga picha kwenye sherehe za kipaimara, sendoff, ndoa kichenpart, graduation na pia kwenye happy birthday na pia kwenye shuguri zingine nyingi.
Taratibu nilianza kujulikana na kuwa maarufu. Na jina langu kukua. Nilikuwa nafanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo yangu. Pesa nilikuwa napata za kutosha kuweza kuishi mwenyewe lakini nguvu ya wazazi ilinifanya nifate watakavyo wao.
Hatimae, miezi ilikatika nikawa si mtu yule wa kukaa mtaani na kulalamikia serikali kuhusu ajira. Sikuwa nasubili tena ajira kutoka serikalini, bali nilikuwa nimetoa ajira kwa vijana wanne ambao niliwafundisha kazi. Vijana walikuwa wakijituma haswa.
*********************************************
********
Baada ya kufunga ofisi niliwakabizi vijana wangu wa kazi ujila wao wa siku, kisha mimi nikaanza safari ya kuelekea nyumbani. Sikiwa na appointment na mtu yeyote hivyo sikuwa na sehemu yeyote ya kupita, moja kwa moja nilielekea nyumbani. Nilipofika nyumbani kitu cha kwanza nilielekea bafuni kuoga. Baada ya kuoga nilibadili nguo na kwenda kuungana na familia kwa ajiri ya chakula cha usiku.
"Lukas naona mambo sio mabaya mwanangu." Aliongea baba baada ya kumaliza kula chakula.
"Hapana baba kawaida tu kwani vipi?" Nilimjibu baba.
"Sikusikii tena ukilalamika kuhusu serikali kutoa ajira........ maana kipindi cha nyuma nilikuwa nakusikia kila mara ukitupia lawama serikali." Baba aliendelea kuonge.
"Akili ilikuwa bado haijakoma tu baba lakini sasa sina tatizo kabsa." Niliongea.
"Ndio kusema kwamba hata zikitoka ajira huwezi kwenda mwanangu." Aliongea mama aliekuwa amekaa pembeni kwa baba.
"Yani mama kwa kipato nachokipata kwa sasa hata sina shida tena ya hizo ajira. Akiri yangu saizi inawaza mambo makubwa ambayo nauhakika kama nikisubili kuajiriwa sitaweza kuyatimiza." Niliongea kwa kujiamini.
Baada ya maongezi tulitawanyika kila mmoja na kwenda kulala.
Asubuhi ya siku iliyofata niliamka mapema kama kawaida yangu. Nilijianda kisha nikaelekea mezani kupata kifungua kinywa. Ilikuwa kawaida kwetu kila siku ifikapo saa moja lazima chai iwepo mezani. Nilikunywa chai na siresi tatu za mkate kisha nikatoka na kuanza safari ya kuelekea ofisini kwangu. Nilipofika ofisini niliwakuta vijana tiali washa fika. Kama kawaida niligawaia majukumu ya kazi kila mmoja nilimpa kadi ya mwaliko wa kwenda kupiga picha kutoka katika sherehe nilizokuwa nimepata kadi.
Siku ilienda poa sana jioni vijana walirudi na picha. Siku zote kitu ukikifanyia ubunifu lazima kitapendwa na wengi. Ndivyo ilivyo kuwa hata kwenye kazi yangu. Baada ya vijana wangu wa kazi kuwasirisha kazi nilizichukua na kuziweka kwenye laptop yangu na kuanza kuziwekea mandhari nzuri ili kuzipendezesha zaidi. Kwa kutumia faili la adobe photo shop nilikuwa nikizitengeneza picha na kuzifanya ziwe na mwonekano angavu.
"Tino hii picha vipi mpaka hapa unaionaje si iko poa sana." Nilimuliza kijana wangu mmoja wa kazi ambae alikuwa akinifatilia kipindi nikiwa naifanyia editing ile picha.
"Hapa boss mbona mwake picha imetoka unaweza sema location ilikuwa UK vile." Aliongea Tino.
MPIGA PICHA SEHEMU YA PILI
"Hivi wewe Tino utakuja ubadilike lini lakini...... kila siku nakwambia sitaki uniite hilo jina sijui boss...." niliongea huku nikimkazia jicho Tino.
"Sorry bo..... sorry kaka si unajua tena nisha zoea. Ata ivyo lakini wewe si ndio boss wetu." Alizidi kuongea Tino.
"Tuachane na hayo maana wewe mtu sio muelewa kabsa..... turudi kwenye mada. Hii picha ya pili hii sijui mpigaji alikuwa kalewa maana haijatoka vizuri ulipiga umekurupuka nini?" Niliongea huku nikimwonesha Tino picha ambayo ilikuwa haioneshi vizuri sura za watu.
"Hiyo sikupiga mimi boss... alipiga Majaliwa....." alizidi kuongea Tino.
"Khaaa...! usha anza uongo wako dogo.... hii sherehe nilikutuma ukapige wewe inakuwaje tena unaniambia alipiga Majariwa. Majariwa anakujaje kati yeye alikuwa ameenda kupiga kwenye sherehe ya ubatizo." Niliongea huki nikizima laptop
"Nisamehe kaka daa....! Nilijichanganya tu si unajua tena." Aliomba msamaha.
"Sawa ila siku nyingine uwe makini sana Tino. Kazi za watu hizi si unajua ushindani mwingi tukicheza itakula kwetu." Niliongea kisha nikamwambia Tino awaite wenzake niwapatie ujira wao wa siku. Baada ya mda Tino alikuja na wenzake kisha nikawapatia posho zao wakaondoka.
Nikiwa najianda kufunga ili niondoke alikuja Leticia. Leticia alikuwa alikuwa ameijia picha yake. Leticia ni msichana mwenye mwonekano mzuri lakini alikuwa akiutumia mwonekano wake vizivyo sitahiri. Alikuwa anapenda sana kupiga picha huku akiacha sehemu kubwa ya mwili wake wazi. Kifupi alikuwa hasamini mwili wake. Japo yeye alikuwa anadai kuwa alikuwa akitumia kupata pesa. Pia alikuwa akidai picha izo zimempa umaarufu mkubwa mpaka kufikia kushirikishwa kuwa video vixin kwenye moja ya nyimbo za mastaa wakubwa wa mziki wa kizazi kipya hapa nchini.
"Nimechelewa eeee.......?" Alifika na kuniuliza swali
"Umechelewa ndio si unaona niko nafunga hapa.... yani ungekawia kidogo ulikuwa hunikuti?" Nilimjibu Leticia
"Basi nitakuwa na bahati maana leo mara ya pila nakukuta ukiwa unataka kufunga.... ok tuachane na hayo vipi ule mzigo usha maliza kifanyia kazi maana ninamda nimeadimika sana Insta(gram). Mpaka followers wangu wanauliza kulikoni, nimepotea." Aliongea Leticia
"Yeah nisha maliza kitambo sana nilikiwa nakusubili wewe tu uje uchukue." Nilimwambia Leticia ambae alikuwa akiniangalia pindi nilipokuwa nikiongea.
Nilimalizia kufunga mlango kisha nikafungua begi langu na kutoa laptop na kuiwasha.
"Vipi flash unayo?" Nilimuliza Leticia
"Ndio ninayo hii hapa." Aliongea Leticia huku akinikabizi ile flash. Nilichukua na kuichomeka katika laptop yangu na kisha nilimhamishia Leticia zile picha zake.
Baada ya kumaliza kumhamishia picha Leticia alinipa ujira wangu kisha akaondoka. Uzuri wa Leticia huwa hanaga shida kwenye kumlipa mtu. Ni mmoja wa wateja ambao ni wazuri kufanya nao kazi.
*********************************************
****
Siku zilizidi kwenda na majukumu yakazidi kuongezeka. Nilibidi kutafuta mtu mwingine wa kunisaidia katika maswala ya editing. Nilibahatika kumpata msichana mmoja ambaye alikuwa anaitwa Sarafina. Katika hiki kitengo sikuwa nimekosea hakika nilikuwa sahihi tena sana Sarafina alikuwa anajua zaidi yangu. Katika mashwara ya editing software sikuwa na chakuongea alikuwa fundi haswa.
Maisha yalizidi kusonga. Nyumbani wazazi walitaka nioe. Kila siku neno lilikuwa moja tu kosa wanitie machoni mwao. Hasa hasa mama ndio alikuwa msitari wa mbele kunitaka nitafute mchumba nioe.
"Mama mda bado.... mda ukifika mbona hata hamta niuliza nitamleta.... afu pia mambo mazuri hayahitaji haraka. Sitaki nikosee kuchagua." Nijibu ambalo nilikuwa nikiwajibu wazazi wangu kila waniulizapo swala la kuoa.
*********************************************
******
Siku moja nilimaliza kufanya kazi mapena. Tulikuwa tunapiga story na Tino alikuja msichana mmoja mwenye asili ya kiarabu ambae kwa mda mchache toka nimuone alitokea kuziteka akili zangu. Alikuwa mzuri sana anavutia kumtazama. Kwa sekunde kazaa akili zangu na ubongo wangu ulisimama.
"Habari zenu?" Alitusalimia yule binti
"Nzu...uuu.....riii.....tuuu..... za kwako." Nilijikuta napatwa na kigugumizi kujibu salamu yake.
"Nahitaji kupiga picha." Aliongea kwa sauti nyembamba nzuri ambayo huweza kusababisha usingizi kwa mtu aliye na ugonjwa wa kukoswa usingizi.
"Vipi kuhusu location unapigia hapa au kuna sehemu ambako unataka tukakupigie?" Nilimuliza yule dada.
"Mmmmm......i think hata hapa panafaa maana nahitaji picha mbili tu kubwa..... kuhusu location haina tatizo." Aliongea yule dada.
"Ok sawa haina tatizo." Nniliongea kisha nikachukua kamera mwenyewe.
"Sorry sister itabidi upite huku." Nilimwambia yule dada huku nikimwelekeza kwa kidole sehemu ya kupita. Yule mrembo alipita kisha akaingia kwenye chumba ambacho tulikuwa tukitumia kupigia picha, kwa watu waliokuwa wakitaka picha za haraka.
Kwa mda niliokuwa nao katika fani ya upigaji picha na uzoefu niliokuwa nao. Nilikuwa najua mapozi/mikao ambayo mtu akikaa lazima apendeze zaidi.
"Ok napigaa..... moja......mbili.......tatu....
..KACHAAAAA." mlio wa kamera ulisikika. Nilimpiga picha huku akiwa amekaa kwenye kiti cha duara cha plastiki.
"Fanya kama una tabasamu kidogo... binua mdomo.... afu mkono wa kulia fanya kushika kiuno. Afu hebu fanya kama unabinya jicho moja kama unanikonyeza. Eeee hivyo..... KACHAAAA." Nilimpiga picha nyingine.
"Nimekumbuka kweli kuna pozi moja hiliapa, kwa jinsi ulivyo naimani utatoka mbaya." Nilimwambia yule dada aliyebaki kutabasamu tu. Alifata jinsi nilivyo mwelekeza kisha nikampiga picha. Baada ya kumaliza kumpiga picha nilienda kumkabizi Sarafina zile picha azifanyie kazi. Mrembo yule alilipa pesa yote kisha ikabaki kucha kuchukua picha zake tu.
MPIGA PICHA SEHEMU YA TATU
"Utakuja saa kumi na mbili utazikuta ziko tiali." Nilimwambia yule dada.
"It's ok hamna shida." Aliongea huku akibinua midomo na kufanya azidi kupendeza mara dufu.
"Afu samahani dada kweli unaitwa nani?"
"Zulfa." Alitaja jina lake, kisha akaaga na kuondoka.
"Vipi bosi mtoto kakudatisha nini?" Alikuja Tino na kuniuliza swali.
"Hapana kawaida tu, mimi najielewa siwezi kudata kishamba kiasi hicho." Niliongea jibu ambalo hakika halikiwa na ukweli wowote. Moyoni mwangu Zulfa alikuwa amenikamata haswa.
Kwa mara ya kwanza nilihisi kupenda. Zulfa aliteka moyo wangu na akili zangu kwa pamoja. Mawwazo yangu yalibaki kumwaza yeye tu.
Hatimae saa kumi na mbilo za jioni zilifika. Zulfa alikuja tena pale ofisini akiijia picha zake. Mda huu alikuja akiwa kapendeza zaidi japo alikuwa ndani ya dela, lakini umbo lake liliweza kwendana vilivyo na nguo ile. Alifika na kutusalimia kisha akaomba mzigo wake. Nilimkabizi picha zake. Zulfa alianza kuziangali picha zile, huku akinishushia sifa kede kede kwa kazi ile ya kupendezesha picha zake. Kweli picha zilikuwa zimetoka bomba sana.
"Ok kaka mimi naenda, asante kwa kazi nzuri...." aliongea Zulfa
"Ni wajibu wangu kufanya hivyo ili mteja afurahie uduma yetu. Karibu tena mrembo Zulfa." Nilimjibu Zulfa huku nikiwa nangalia uzuri wake ule aliojariwa.
Zulfa alitabasamu kisha akaaga na kuondoka.
"Mtoto mzuri kweli huyu sijui nampataje? Anafaa kuwa mke mwone alivyo. Lakini kwa uzuri huu alionao si atanitesa sana maana wengi watakuwa wanamtaka. Nikiwa nae ataniua kwa wivu huyu mtoto." Mawazo yalizidi kutawala akili yangu kumuwaza Zulfa.
Nikiwa katika dimbwi la mawazo alikuja Tino na kunikatisha baada ya kuanza kunisemesha.
"Boss vipi unawaza nini? Nimefika mda hapa nakuangalia unavyofanya hata sikuelewi. Kuna tatizo kwani?" Aliongea Tino kisha akamalizia kwa kuniuliza swali.
"Tino mshikaji wangu we acha tu nakwambia achatu."
"Niache nini boss.... mbona sikuelewi funguka boss wangu kama kuna tatizo na kuna uwezekano wa kulitatua tutasaidiana."
"Sikia.... unajua nini Tino acha tu niseme ukweli. Kwa mara ya kwanza tu nilipomuona katokea kuuteka moyo wangu, yani hata sielewi kuna nini hapa kati. Nimetokea kumpenda Zulfa sana tena sana. Yani hata sijui nieleze vipi." Niliongea ili nikitaka msaada wa mawazo toka kwa Tino.
"Haaaa kaka bora umeongea ukweli. Afu kumpata mbona sio kazi mimi napajua mpaka kwao. Mimi ndio city boy so usiwe na shaka. Nitafanya kila kitu umpate boss wangu." Aliongea Tino maneno ambayo yalinitia moyo na kunipa tumaini jipya.
"Kuna zawadi yako Tino endapo ukifanikisha kunikutanisha nae."
"Kweli boss......?"
"Yeah....! Kweli wewe fanya mpango tu. Serious zawadi ipo sikutanii." Niliongea huku nikimpiga piga Tino mgongoni.
Mda wa kufunga ofisi ulifika tukafunga. Kisha kila mmoja akaondoka na kuelekea nyumbani. Nilifika nyumbani, moja kwa moja nilipitiliza mpaka chumbani kwangu. Nilivyofika ndani nilifungua mkoba na kutoa picha moja na kianza kuiangalia. Mda ote nilifurahi kuitazama picha ile.
"One day.... i will marry you." Niliiambia ile picha. Nilitupia ile picha kitandani kisha nikanyanyuka na kuliendea begi dogo ambalo lilikuwa mle ndani. Nililifikia na kulifungua kisha nikatoa gundi. Nilirudi kitandani na kuichukua ile picha kisha nikaenda kuibandika ukutani. Kwenye picha alionekana Zulfa akiwa kama ananikonyeza vile. Huku tabasamu lake zuri liliacha meno yake meupe nje na kufanya azidi kupendeza mar dufu. Alivutia hata kwenye picha.
"Lucas.... Lucas......" nilisikia sauti ya mama ikiniita tokea sebuleni.
"Naamu... mama.....!" Niliitika kisha nikaanza safari ya kutoka mle chumbani kwangu na kuelekea sebuleni.
"Mdogo wako Alice anakuja.... wamefunga shule toka jana. Mda mfupi uliopita nimeongea nae amesema wamefika Buhongwa. Nahisi baada ya kama dakika kumi watakuwa stendi. Fanya mpango ukampokee." Aliongea baba.
"Sawa baba hamna shida. Acha nijiandae mara moja niende." Nilitoka na kwenda bafuni kuoga. Baada ya dakika kumi nilikuwa nisha maliza kila kitu nilitoka nje ya nyumba na kuita boda boda ambayo ilinichukua na kunipeleka mpaka nyegezi. Nilifika nyegezi na kukaa mda wa dakika mbili ndipo gari alilokuwa amepanda Alice lilifika. Nilinyanyuka toka nilipokuwa nimekaa na kusogea usawa wa mlango wa basi lile. Abilia walikuwa wakishuka mmoja baada ya mwingine. Hatimae niliweza kumwona Alice nae akishuka. Nilisogea zaidi ili kumpokea Alice aliponiona alinirukia na kunikumbatia.
"Waooo... kaka, naona umekuja kunipokea."
"Ndio nimekuja kukupokea mdogo wangu nilikumiss kweli." Niliongea na kumpokea begi alilokuwa nalo. Kisha tukanza kutoka pale.
"Umekuja na nani?" Aliniuliza Alice
"Niko mwenyewe."
"Mmmmh mbona umekuja mwenyewe mimi nilijua umekuja na wifi yangu." Aliongea Alice.
"Wifi yako ama nini.....? Usijari awamu ijayo ukiwa unakuja kama hivi niymtakuja nae kukukopea ila kwa sasa bado hajapatikana."
"Kaaaaa... na wewe kaka unataka mpaka ufikishe miaka mingapi ndio uoeeee."
"Soon tu nitaoa... ila inatakiwa mipango na maandalizi ili kumpata mtu anae stahiri. Au wewe unapenda siku moja uje unione kaka yako nikiwa nateswa na mapenzi?" Nilimjibu Alice aliyeonekana kunielewa kile nilichokuwa naongea.
*********************