MOYO ULIOJAA MAUMIVU
SEHEMU YA 43
Wakati Theo akijiandaa kwenda kufanya video nchini Afrika Kusini, kampuni ambayo ilikuwa ikitarajiwa kufanya video hiyo ikaanza kuandaa warembo kwa ajili ya kutumika. Miongoni mwa warembo hao alikuwepo Iyanya ambaye alitumia video nyingi kuwatega wanaume na kuwalia pesa zao.
Alipoambiwa kwamba video ambayo walitakiwa kushuti ilikuwa ni ya Theo, alichanganyikiwa mno, alimpenda mwanaume huyo kupita kiasi, kwake, masupastaa hawakuwa wakipindua, alipenda kuwa nao na kufanya uchafu wowote ule huku akilipwa kiasi kikubwa cha pesa.
Alihitaji kujiweka katika mazingira mazuri, ya kumtega mwanaume huyo ambaye aliamini piga ua ilikuwa ni lazima achanganyikiwe kwa jinsi atakavyokuwa. Siku ambayo waliambiwa waende location, akaenda huku akiwa na muonekano wa kuvutia kupita kawaida.
Wanaume ambao walikuwa mahali hapo wakaanza kumwangalia kwa macho ya uchu, japokuwa hapo kulikuwa na wanawake wengi lakini huyu Iyanya alionekana kuwa moto wa kuotea mbali, alikuwa ni mzuri zaidi ya wanawake wote waliokuwa hapo.
Mitego yake ilikuwa ni kwa Theo tu. Alimpenda mwanaume huyo, alitamani kulala naye kitanda kimoja. Alihitaji pesa zake pia, aliamini kwamba endapo angekuwa na mwanaume huyo ingekuwa rahisi sana kupata pesa kutoka kwake, hivyo alitaka kujaribu bahati yake.
Baada ya kukaa hapo kwa dakika kama thelathini ndipo Theo akaingia huku akiwa na wapambe wake.
Baada ya kukaa hapo kwa dakika kama thelathini ndipo Theo akaingia huku akiwa na wapambe wake.
Iyanya alipomuona tu, moyo wake ukapiga paaa, hakuamini kumuona mwanaume huyo mahali hapo, siku hiyo alipomwangalia, alionekana kuwa mzuri kupita kawaida.
Theo hakutakiwa kuongea na mtu yeyote, hasa wanawake hao ambao walipelekwa mahali pale kwa ajili ya kushuti kisha kuondoka zake.
Theo hakutakiwa kuongea na mtu yeyote, hasa wanawake hao ambao walipelekwa mahali pale kwa ajili ya kushuti kisha kuondoka zake.
Kwa Iyanya hilo likaonekana kuwa gumu, hakuwa tayari kufika sehemu ya tukio, amwangalie Theo na kuona mwanaume huyo akiondoka pasipo kuongea naye lolote lile.
“Ni lazima nitaongea naye! Siwezi kubaki kama sanamu,” alijisemea huku muda mwingi wa kushuti macho yake yalikuwa kwa mwanaume huyo tu.