MOYO ULIOJAA MAUMIVU
SEHEMU YA 42
Huyo aliitwa Iyanya Kobero, msichana wa Kizulu aliyekuwa na urembo wa kila namna. Alikuwa mwembamba, kiuno chake kilikuwa chembamba zaidi lakini kwa nyuma alifungashia.
Alikuwa mzuri, alijua kupendeza na kila alipokuwa akipiga picha, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuyaonyesha makalio yake kwanza huku lengo lake likiwa ni kuwadatisha wanaume wengi.
Iyanya alikuwa mfanyabishara mkubwa mitandaoni. Alifungua akaunti yake Instagram kwa ajili ya kujiuza. Aliweke picha nyingi zilizokuwa na mitego ya kila namna, mwanaume ambaye alimtaka, alimfuata sehemu ya meseji, waliwasiliana na kumpa namba ya simu.
Hiyo ndiyo ilikuwa biashara yake, alikuwa malaya, si wa kwenda klabu au barabarani, aliingiza pesa kupitia akaunti yake ya Insragram tu. Alikuwa mwanamke hatari, aliyezitetemesha ndoa za watu wengi, kulikuwa na wanawake waliolia sana kuibiwa wanaume zao, ilikuwa ni vigumu kuiona picha ya Iyanya kwenye akaunti yake halafu usibonyeze sehemu ya ‘like’
Shepu yake, jinsi kali lake lilivyokuwa ndiyo ilikuwa silaha yake kubwa, ya kuwateka wanaume wengi kiasi kwamba alikuwa na uhakika wa kulala na wanaume wanne tofauti ndani ya wiki moja kwa malipo makubwa tu.
Hiyo haikuwa kwa Iyanya tu, kulikuwa na wasichana wengi katika vyuo mbalimbali nchini Afrika Kusini ambao kazi yao ilikuwa ni kujiuza tu kwenye mitandao ya kijamii.
Ni kama mambo yalionekana kunoga kwani kila msichana ambaye aliamini kwamba alikuwa na makalio makubwa, kitu cha kwanza kilikuwa ni kuingia kwenye mitandao ya kijamii, kupiga picha za kihasara na kuziweka huko, na kwa kufanya hivyo, walitengeneza pesa nyingi mno, na miongoni mwa watu hao alikuwa huyo Iyanya.
|
|
|
Je, nini kitaendelea?