MAPISHI YA NOODLE'S ZA PILAU
Kosha mchele weka upande.
Mkoshekuku mtie spices mkaushe ikisha mtie maji achemkie badae towa maji weka pembeni utayatumia badae.
kwenye blander tia Tungule kitungumaji kipande nakotmiri saga uzuri usitie maji ukishasaga mimina rojo kwenye Kuku mkaushie awe mkavu na awive.
MAHITAJI YA KUPIKA NOODLE'S PILAU
- Noodles/tambi nyembamba pakti 1
- kitungu maji kidogo extra
- Majani ya mvuje ukipenda.
JINSI YA KUPIKA NOODLE'S ZA PILAU
- Kosha mchele weka upande.
- Mkoshekuku mtie spices mkaushe ikisha mtie maji achemkie badae towa maji weka pembeni utayatumia badae.
- kwenye blander tia Tungule kitungumaji kipande nakotmiri saga uzuri usitie maji ukishasaga mimina rojo kwenye Kuku mkaushie awe mkavu na awive.
- kata mbatata slesi za duara,vitungu 3 slesi. Chukuwa frying pan tia mafuta kanga mbataza zikishaiva zitowe, tia vitungu vikishakuwa brown towa, kanga noodles zikianza kuwa light brown zitowe. Vote vitandaze mbali mbali vipowe..
- weka sufuria safi tia mafuta anza kukanga kitungu maji kilichobaki tia spices tia Thomu Tangawizi kanga kama pilau tia maji ya supu yakishachemka mimina mchele wako pika ukishakauka maji mimina nusu wali kwenye Kuku ulomkausha tia vitungu nusu na noodle's nusu malizia kwa wali ulobaki
- ufunike ukaukie uzuri kabla kupakuwa fanya kishimo weka foil weka ganda lakitungu maji weka mka wa moto tia samli funikaa uzuri ufukizike lile ganda kavu la kitungu huwa kama ndio udi wako chakula kinanukia hadi raha.
JINSI YA KUPAKUWA NOODLE'S ZA PILAU
- Changanya taratibu wali kwenye sufuria hakikisha Kuku havurugiki.
- tia kwenye chombo tia mbatata zako kwa kuzipanga uzuri nyunyizia noodles zilobakia na mwisho nyunyizia vitungumaji .tayari kwa kula.