BIRIYANI YA KUKU (KAVU)
MAHITAJI YA KUPIKA BIRIYANI YA KUKU (KAVU) |
- Mrowanishe kuku na viungo hivi kwa muda mdogo tu
- Kuku (Mkate kate Vipande) 4 LB
- Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi 2 Vijiko vya supu
- Chumvi kiasi
- Pilipili nyekundu ya unga 1 Kijiko cha supu
- Bizari ya manjano (Haldi au Tumeric) 1 Kijiko cha chai
- Bizari ya pilau ya powder (Jeera) 1 Kijiko cha chai
- Gilgilani powder (Dania) 1 Kijiko cha chai
- Ndimu 1 Kijiko cha supu
Mchele na vitu vya Masala:
- Mchele (Basmati mzuri) (rowanisha) 7 cups
- Mafuta ya kupikia kiasi
- Vitunguu Vilivyokatwa 8
- Nyanya iliyokatwa katwa 3
- Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi 1 Kijiko cha supi
- Garam Masala 1 Kijiko cha supu
- Hiliki powder ½ Kijiko cha chai
- Tomatoe paste 1 Kijiko cha supu
- Pilipili mbichi zipasue katikati 4
- Chumvi kiasi
- Mtindi 4 Vijiko vya supu
- Kotmiri iliokatwa (Chopped) ½ Kikombe
- Mafuta ya kunyunyuzia katika wali 3 Vijiko vya supu
- Zaafarani au rangi ya biriani kiasi
JINSI YA KUPIKA BIRIYANI YA KUKU (KAVU)
1· Weka kuku aliyerowanishwa na viungo vyake katika Foil tray au chombo chocote utakachomwagia wali humo humo na kupikia biriani, kisha mchome (Bake) mpaka awive na awe mkavu kiasi.
2· Wakati kuku anapikika, kaanga vitunguu katika karai au sufuria mpaka viwe brown na epua nusu yake weka kando.
3· Punguza mafuta yabakie kiasi tu, ongeza Thomu na tangawizi, na viungo vyote vya hapo juu isipokuwa Mtindi na kotmiri, endelea kukaanga hadi tomatoe zilainike.
4· Ongeza chumvi, malizia mwisho kwa kutia mtindi, kotmiri na vile vitunguu ulivyoweka kando. Masala yako tayari.
5· Mwagia masala juu ya kuku uliyekwishmpika changanya vizuri.
6· Chemsha Mchele uwive nusu, chuja na mwagia juu ya masala.
7· Nyunyiza mafuta kidogo juu ya mchele na zaafarani au rangi ya biriani.
8· Bake katika moto wa 350 – 400 kwa muda wa 15 – 20 minutes. Biriyani imekuwa tayari kuliwa.
Mtindi wa kutolea Biriyani:
- Mtindi 1 kikombe
- Pilipili mbichi 1 ndogo
- Kitunguu saumu(/galic)homu chembe
- Chumvi chembe tu.
Weka kwenye Blender na uchanganye, kisha mimina katika bakuli