Notification texts go here Contact Us Buy Now!

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 20

RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA ISHIRINI.

MTUNZI : ALEX KILEO..

_______________
ILIPOISHIA...
_______________

Kesho yake ilipofika,
nikamwambia bibi yako kilichotokea,
ikabidi awaite wanaukoo wote ambao
walikuwa jirani na pale tunapoishi
na kuwaelezea yote niliyoambiwa na
mzimu.

wakakubaliana niondoke,
ila wewe nikuache, na kuhusu malezi
yako, atakaehusika nayo ni shangazi
yako
mkubwa, ambae alikuwa anakaa
kigoma, nikakubali kwa roho safi, kwa
makubaliano ya kila baada ya miezi
miwili ningeenda kwa shangazi yako
kukuangalia......

_____________
ENDELEA...
_____________
....uko kwa shangazi yako walikuwa
wanafuata masharti ya mzimu kama
kawaida.

kila mwisho mwezi
walikuchinjia mbuzi na kondoo,
damu walikupa ukainywa na sijawahi kusikia tena huo mzimu ukisumbua.

Sasa hayo matatizo yanayokukuta uko chuo labda ni kutokana na masharti kutotekelezwa
kwa sababu ya umbali uliopo" Mama
kayoza akawa amemaliza masimulizi
yake rasmi,

"mh, mbona ni shughuli
nzito?, sasa mama utanisaidiaje?"
kayoza alimuuliza mama yake,

"mwanangu sina msaada kwako"
mama kayoza akajibu.

"mama hamna
mganga yeyote wa jadi
unaemfahamu, ili anisaidie" kayoza
aliendelea kumtupia maswali mama
yake.

"kusema kweli upande wa
ushirikina huko mi sipaamini, ila..."
mama kayoza akawa kama anafikiria
kitu,

"Ila nini?" Kayoza akamuuliza mama yake,

"ila kuna mchungaji pale kanisani kwetu,
nitajaribu kumuomba msaada" Mama
kayoza akamalizia namna hiyo.

"hata hivyo ni sawa pia, sasa utaenda
kumwambia saa ngapi?" Kayoza kamuuliza mama yake.

"nitaenda
kumwambia jioni baada ya kula
chakula" mama Kayoza
akajibu.

"mambo si hayo bwana"
Kayoza akaongea huku akiwa na matumaini kibao ya kufanikiwa katika
zoezi hilo.

Baada ya kumaliza kula
chakula cha jioni, mama Kayoza
alijitanda vitenge vyake na kuelekea
katika makazi ya mchungaji.

Alipofika alikaribishwa na mtoto wa kike wa
mchungaji, ambaye alimpa taharifa Mama kayoza kuwa mchungaji
anaoga, ikambidi Mama Kayoza amsubiri mchungaji hadi
alipomaliza kuoga.

Mchungaji alipomaliza kuoga, akapelekewa
ujumbe kuwa kuna mgeni wake anamsubiri varandani.

Mchungaji akaenda mpaka
Varandani na kumkuta Mama Kayoza akimsubiri,

"karibu mpendwa"
Mchungaji akamkaribisha mama
Kayoza huku akimpa mkono,

"asante mchungaji" mama
kayoza akajibu.

Baada ya salamu na
kujuliana hali zao, mama kayoza
akamuelezea mchungaji mwanzo
mpaka mwisho wa matatizo aliyonayo
Kayoza.
Wakakubaliana hiyo kazi
angeifanya kesho yake
usiku.

***************

Sajenti Minja alipakiwa katika gari kwa makofi kama mharifu aliyekuwa anabishana na Askari.

Gari iliondolewa kwa mwendo wa kawaida lakini kipindi chote wakati gari ikitembea hakuna MP aliyemgusa Sajenti Minja.

Baada ya mwendo wa dakika kumi, Sajenti Minja alishatambua uelekeo wa anapopelekwa na alishaanza kupata wasiwasi mkubwa kuliko ule wa hawali.

"Jamani kwani nimefanya kipi kibaya?" Sajenti Minja aliuliza huku akiwatizama wale MP kwa zamu,

"Hauruhusiwi kuuliza wala kuongea kitu chochote" MP mmoja alijibu na Sajenti Minja akakaa kimya kwa kuwa alijua jeshini amri ndio kiongozi.

Gari iliyombeba Sajenti Minja iliingia katika geti moja kubwa ambalo lilifunguliwa na wanajeshi.
Gari ikapita ndani ya geti na ikatembea tena mwendo wa dakika tano mpaka ilipoenda kusimama mbele ya jengo moja lililokuwa limekaa peke yake.

Sajenti Minja akashuka na kuangaza lile eneo ambalo lilipambwa na wanajeshi wakiwa katika majukumu mbalimbali pale kambini.

Sajenti akaongozwa mpaka ndani ya lile jengo na kuingizwa katika ofisi moja nadhifu ambapo ndani ya hiyo ofisi walimkuta bwana mmoja mwenye umri wa miaka 40 - 45 akiwa amekaa katika kiti.

Sajenti Minja na wenzake wote wakampigia saluti kwa ukakamavu yule bwana.

"Asanteni vijana wangu, mnaweza kwenda nje na mniache na huyu bwana" Yule bwana aliongea kisha wale MP wakaelekea nje na kumuacha Sajenti Minja ndani tena akiwa amesimama,

"Polisi wamekubali uache kazi?" Yule bwana alimuuliza Sajenti Minja,

"Ndio mkuu" Sajenti Minja alijibu kikakamavu,

"Ni nani aliyetaka wewe uende ukafanye kazi polisi?" Yule bwana alimuuliza,

"Ni mimi mkuu" Sajenti Minja alijibu huku akiwa bado kasimama,

"Ulisema kwanini ulitaka kifanya kazi ya polisi?" Yule bwana alimuuliza,

"Ni kwa sababu nilitoka mafunzoni nje ya nchi, kwa hiyo niliitaji kupata sifa zaidi upande wa upelelezi wa ndani ili nipate nafasi ya kwenda kuongeza mafunzo ya nje ya nchi tena" Sajenti Minja alijibu,

"Je kazi ya upelelezi ulipewa uko polisi?" Yule bwana alimuuliza,

"Ndio nilipewa" Sajenti Minja alijibu,

"Nadhani umeikamilisha?" Yule bwana aliuliza,

"Hapana" Sajenti Minja alijbu,

"Kwanini?" Yule bwana aliuliza,

"Nimepata tatizo la afya, nikaona ni bora nipumzike" Sajenti alijibu,

"Lete cheti cha daktari kinachothibitisha wewe no mgonjwa" Yule bwana alimwambia Sajenti Minja,

"Nimekiacha nyumbani" Sajenti Minja alijibu ila alitoa jibu la uongo kwa maana hakuna cheti wala kitu chochote kinachoweza kuthibitisha yeye ni mgonjwa,

"Ni tatizo gani la kiafya ulilonalo?" Yule bwana aliuliza,

"Pumzi inanibana sana kiasi kwamba nashindwa kupumua" Sajenti Minja alijibu,

"Ooh pole, basi nenda kapumzike, tutaendelea baadae na maswali" Yule bwana aliongea,

"Sawa mkuu" Sajenti Minja alijibu na kuanza kuondoka,

"Unaenda wapi?" Yule bwana alimuuliza kwa mshangao,

"Umeniambia nikapumzike mkuu, naenda nyumbani" Sajenti Minja alijibu huku akisimama,

"Utapumzikia hapa hapa kambini ili nitapohitaji kuongea na wewe, nikuite" Yule bwana aliongea kisha akapiga simu katika namba anayoijua yeye na kumtaka yule anaongea nae aende ofisini, kisha akakata simu.

Baada ya sekunde kadhaa aliingia mwanajeshi na kusimama kikakamavu,

"Mpeleke huyu akapumzike" Yule bwana alimwambia mwanajeshi aliyeingia,

"Upande gani" Yule mwanajeshi aliyeingia akauliza,

"Kwa wenye Matatizo ya kupumua au kwa wagonjwa wa mapafu na kifua" Yule bwana alijibu na kisha akamshuhudia yule mwanajeshi akimuongoza Sajenti Minja kwenda nje ya ofisi.

Yule bwana akatoa tabasamu huku akitingisha kichwa kwa masikitiko.

************

Huyu mchungaji ambaye Kayoza atamtembelea anaitwa Batoromeo
mathayo wingo, jina maarufu
lililozoeleka na wahumini wake ni
Mchungaji Wingo, tokea ahamie pale
kanisani ana muda wa mwaka mmoja
na nusu, na watu wanaodaiwa kuwa
wachawi, wameshadondoka kwenye
eneo la makazi yake zaidi ya mara
nne, hii ilimjengea imani sana kwa wahumini wake na pia alijikuta waumini wengine kutoka makanisa mengine wakifurika katika kanisa lake kila siku ambayo alifanya maombi kwa ajili ya wagonjwa na walemavu.

Ndani ya muda mfupi Mchungaji Wingo aliweza kupata jina na heshima kubwa mkoani shinyanga.

***************

Kesho yake ilipofika, mama Kayoza na Kayoza
pamoja na Omari wakaongozana
usiku ule mpaka kwa mchungaji
Wingo, Walipofika, mchungaji na
familia yake, wakawakaribisha ndani,
na baada ya maongezi ya muda mrefu, mchungaji aliwaambia kuwa,
mama kayoza na Omari warudi
nyumbani, ila Kayoza abakie, kwa
sababu anataka akeshe nae huku wakimfanyia maombi na familia
yake, mama kayoza na Omari wakajiondokea zao, wakamuacha
kayoza kwa mchungaji...

KAMA MCHUNGAJI ANGEJUA KITAKACHOMTOKEA, ASINGEKUBALI
KUBAKIA NA KAYOZA...

******ITAENDELEA******

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.