Notification texts go here Contact Us Buy Now!

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 12

RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA KUMI NA MBILI

MTUNZI : ALEX KILEO..

SEHEMU YA KUMI NA MBILI

_______________
ILIPOISHIA..
_______________

Gari ikafika mwisho wa safari,
watu wakaanza kutelemka, wale
wakina mama kwa ajili ya kuwa na
mtoto, ikabidi wasubiri ili watu wote
watoke na wao ndio watoke wawe wa
mwisho, sasa wakati wakina kayoza
wanawapita, Omary akamkanyaga
yule
mama mwenye mtoto kwa bahati
mbaya,

"samahani mama" Omary
akamtaka radhi yule mama huku
akimwangalia
usoni, yule mama akapata mshtuko,

"ah!, si ndo
huyu?" Yule mama alisema kwa
kupayuka..

____________
ENDELEA...
_____________

"sio mimi" Omary aliongea bila kutarajia huku akijinasua kutoka kwenye mkono wa yule mwanamke, kisha wakatoka haraka ndani
ya ile gari na kukimbilia nje.

Yule mama akachukua
gazeti kutoka kwa mwenzake, kisha
akaiangalia ile picha ya Omary iliyokuwepo katika gazeti

"mh!, haswaa
ndiye yeye" Yule mama akajisemea moyoni, kisha
akatoka kwa lengo la kuwatazama
walipoelekea wakina Omari, ila
alichelewa, akakuta peupe.
akaangaza tena, hakuona mtu,
akaishia kusonya.

Baada ya wakina
kayoza kufanikiwa kushuka kwenye
gari, wakakimbilia nyuma ya ile gari,
wakawa wanamchunguza yule mama,
paka alivyotoka ndani ya gari na kuanza kuangaza
walikuwa wanamuangalia, mpaka ule
msonyo uliotolewa na yule mama pia waliusikia, wakasubiri mpaka yule mama alipoondoka, nao
ndio wakaondoka ila kwa kujificha ficha sana nyuma ya magari mengine yaliyokuwepo pale.

"Yaani tayari habari zimeshasambazwa katika vyombo vya habari?" Omary alimuuliza mwenzake wakiwa tayari wameshatoka katika kituo cha mabasi,

"Tena wamechelewa kweli, ilitakiwa watoe taharifa jana" Kayoza alijibu huku akikagua mandhari ya mji wa Tanga,

"Ebu twende pale tukasome some magazeti" Omary aliongea huku akielekea sehemu ambapo kulikuwa na magazeti yametandazwa juu ya meza,

"Acha ujinga wewe" Kayoza aliongea huku akiwa anamzuia Omary,

"Kwanini?" Omary aliuliza huku akimshangaa Kayoza,

"Unajua kuwa sisi tunatafutwa na mbaya zaidi picha yako ndiyo imeonekana kwenye magazeti, kwa hiyo wewe huoni kwenda eneo kama lile ni rahisi sana kukamatwa?" Kayoza aliuliza baada ya maelezo marefu,

"Ila kweli, basi nenda wewe kaangalie, alafu uje unijulishe" Omary alimwambia Kayoza,

"Mimi naenda, ila sio kuangalia. Naenda kununua gazeti tutaenda kusoma mbele Safari" Kayoza aliongea huku akielekea pale walipotandaza magazeti mezani. Alifika na kununua magazeti mawili ya kisiasa na jamii na kisha akarudi mahali Omary alipo na kumpa gazeti moja, nae akabaki na moja,

"Alafu ujue umenishangaza sana" Omary alimwambia Kayoza,

"Kwanini?" Kayoza aliuliza,

"Kwanini yule Askari mweupe haujamuua?" Kayoza aliuliza huku akimaanisha Sajenti Minja,

"Mimi?" kayoza aliuliza tena,

"Ndio, ni wewe" Omary alikazia swali lake,

"Sasa mimi nitajuaje wakati unajua kabisa mimi nikiwa katika hali ile uwa sijitambui?" Kayoza nae alijibu kwa mtindo wa kuuliza,

"Hicho kitu kimenishangaza sana" Omary aliongea huku akiendelea kushangaa,

"Wewe mwenyewe uwa sikudhuru na Kwanini hushangai?" Kayoza alimuuliza Omary,

"Dah, tuachane na hayo, maana tukiulizana sana hatutapata majibu ila tutaongeza maswali" Omary aliamua kupotezea huo mjadala,

"Na mbona hawajaandika habari za Denis katika haya magazeti?" Kayoza alimuuliza Omary,

"Hata mimi sijaelewa, au labda kuna sababu waliyofanya wafiche kifo chake?" Omary aliongea ila wote walilijadili jambo hilo huku wakiwa na huzuni,

"Muda bado upo, Ngoja tusubiri habari za kesho, labda wanaweza kuja na habari zake" Kayoza aliongea na baada ya hapo ukimya ukafuata.

*******************

Sajenti Minja hakuwa na raha kabisa siku hiyo, maana ndani ya siku chache alishuhudia vifo vya ajabu sana na pia na yeye aliponea chupuchupu kufa na akaachwa na alama ya meno kwenye shingo,

"Kiongozi bora uende hospitali ukaangaliwe kama ayo meno yanaweza kukuletea madhara" Askari mmoja alimshauri Sajenti Minja,

"Nina mpango huo, ila mkuu amesema anataka kuongea na mimi muda huu, so nasubiri nimalize nae maongezi ndio niende hospitali" Sajenti Minja alimjibu yule Askari na muda huo huo kuna Askari mwingine akaja kumwambia Sajenti Minja kuwa anahitajika na mkuu.

Sajenti Minja akanyanyuka na kwenda moja kwa moja ofisini kwa mkuu wake.

"Poleni kwanza kwa matukio mabaya" Mkuu wa polisi aliongea baada ya salamu,

"Tumeshapoa" Sajenti Minja alijibu kwa unyonge,

"Nini maoni yako kuhusu hii kesi?" Mkuu wa Polisi alimuuliza Sajenti Minja,

"Naomba mnitoe kwenye hii kesi, naona kama nimeishindwa" Sajenti Minja aliongea kwa heshima mbele ya mkuu wake,

"Kwanini?" Mkuu aliuliza,

"Nafikiri hiyo ndio njia pekee ya kuweka maisha yangu salama, maana wale tunaowafuatilia sio watu wa kawaida" Sajenti Minja alimueleza mkuu wake,

"Wewe unadhani kufanya hivyo ni sahihi?" Mkuu aliuliza,

"Nadhani inaweza kuwa sahihi" Sajenti Minja alijibu,

"Sawa, nakupa muda wa kwenda kujiuliza tena kuhusu hili, alafu kesho uje tena kuzungumza kuhusu jambo hili hili" Mkuu aliongea na kumruhusu Sajenti Minja aondoke.

Sajenti Minja akatoka na akili yake yote akaielekeza hospitali kwa nia ya kwenda kuangalia kama jeraha aliloachiwa na Kayoza lina madhara gani.

********?******

Kayoza na Omary baada ya mwendo mrefu kutoka kituo cha mabasi, Wakatafuta
baiskeli za kuwafikisha kijijini, bahati
nzuri wakaipata. Walitumia muda wa
dakika ishirini kufika kijiji husika,
wakawalipa madereva ujira wao,
kisha wakaanza kutembea kwa
miguu, walitembea hadi wakafika
sehemu moja, ambayo kulikuwa na
kajumba kadogo kamejitenga kidogo
na nyumba nyingine,

"sijui ndio hapa, ebu ngoja tujaribu" Omari
aliongea bila ya uhakika,
wakiisogelea ile nyumba, kisha wakagonga mlango,

"karibu" sauti
ikajibu kutoka ndani, wakasubiri
mwenyeji hatoke, lakini hakuna
aliyetoka, wakarudia tena kugonga

"shabashi, pita ndani" ile sauti ikajibu kwa ghadhabu kidogo, Omari
akausukuma mlango kisha akaingia,
akamkuta mzee mmoja mfupi mweupe, kavaa baraghashia,

"shikamoo babu" 0mari akamsalimia
kwa furaha.

"marhaba, karibu" yule
mzee aliitikia huku sura yake
ikionesha anajaribu kuvuta
kumbukumbu fulani.

"asante" 0mari
akajibu huku akitambua alichokuwa
anakifikiria babu yake,

"Karibuni mkae" Yule mzee aliongea huku akiendelea kuvuta kumbukumbu,

"babu mimi
mjukuu wako 0mari" Omari akasema huku akitabasamu,

"omari, omari, Omary wa wapi? " Babu aliuliza akiwa bado
anafikiria huku akijaribu kuvuta
kumbukumbu.

"omari mkwiji mtoto wa mwanao wa Dodoma" Omari akamsaidia babu yake kumuelewesha.

"ooh, karibu babu, vipi
mbona umekuja bila taharifa" Babu
akauliza huku akimpa mkono Omary na Kayoza.

"ni matatizo babu,
nitakusimulia tu babu" 0mari akamwambia babu yake huku akifurahi babu yake kumtambua,

"Naona umekuja na mwenzako?" Babu akamuuliza Omary,

"ndio babu" 0mari akajibu,

"karibu kijana" Babu akamwambia Kayoza huku
akimpa mkono, ila kitu cha ajabu,
babu aliung'ang'ania mkono wa
kayoza kwa dakika mbili nzima huku akiwa amemkazia macho,

"kijana una mzigo mzito sana wa matatizo" Babu alimwambia Kayoza huku machozi yakimtoka....

******ITAENDELEA******

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.