RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA KUMI NA MOJA.
MTUNZI : ALEX KILEO.
_______________
ILIPOISHIA..
_______________
Wakaingia, safari ikawa
inaendelea, mwendo kama wa nusu
saa hivi, yule mzee kupitia kioo cha
juu mbele, alishuudia kitu,
kinachoendelea kwenye siti ya
nyuma, ambayo walikaa wakina
kayoza, akapata mshtuko,
akapunguza mwendo wa gari, kisha
akageuka ili kuhakikisha kama ni
kweli au kioo kinamdanganya?..
____________
ENDELEA..
____________
"mbona unalia kijana?" yule mzee alimuuliza
kayoza,
"ni maumivu tu, mzee
wangu" Kayoza akadanganya huku akijifuta machozi, ila
kilichokuwa kinamliza, ni mambo ya ajabu ambayo yanayomtokea, na kikubwa
haswa ni kumpoteza rafiki yake,
denis. Mzee akairudisha gari barabarani baada ya kuridhika na majibu ya Kayoza.
Gari ikaenda hadi morogoro
mjini, yule mzee akaipaki gari nje ya
hoteli moja maarufu pale Morogoro.
"twendeni tukale waheshimiwa" Yule mzee
aliwaambia wakina Kayoza huku
akiuchomoa ufunguo wa gari kutoka
mahali pake, wakina kayoza
wakashuka, huku kila mmoja akiwa
kabeba suruali na fulana ili wakazivae mariwatoni, kwa hali
waliyokuwa nayo, watu wengi
waliwashangaa kutokana na nguo zao kuchanika na kuchafuka kutokana na ajali waliyoipata.
Wakaingia hadi ndani, kisha Omary akaomba
kuelekezwa choo kilipo,
alipoonyeshwa, wakaenda kisha
wakabadili nguo, alafu wakarudi
kujumuika na yule mzee pale
mezani.
Baada ya kumaliza kula,
wakajipakia kwenye gari, kisha safari
ikaendelea.
"mnaenda Tanga katika
eneo gani?" Mzee yule aliwauliza wakati
gari ikianza kushika kasi.
"Chumbageni" Omary akajibu huku safari ikiendelea.
Tanga mjini waliingia saa nne usiku. Yule mzee
akawashusha, wakamshukuru sana,
kisha yule mzee akaendelea na safari
zake, hakuna aliyejua yule mzee alikuwa
anaelekea wapi?, ila walichoshukuru
ni kufika salama.
"kwa muda huu
hatuwezi kupata usafiri, itabidi tutafute guest ya kulala, kesho
tutaamka na hiyo safari yachumbageni" Omary alimwambia
Kayoza hayo maneno,
"mi nakusikiliza wewe" Kayoza ndivyo
alivyomjibu. Wakatafuta nyumba ya wageni, wakaipata.
wakaweka mizigo yao,
kisha wakaenda kutafuta chakula, waliporudi wakalala.
Waliamka saa
nne za hasubui, wakaoga, kisha
wakaenda kupata chai, alafu
wakarudi kuchukua mabegi yao,
safari ya kwenda Chumbageni
ikaanza, wakaulizia sehemu
yanapopaki magari ya Chumbageni,
wakaonyeshwa, wakatafuta gari
iliyokuwa karibu kuondoka,
wakajipakia.
**************
Sajenti Minja alifikia moja kwa moja kituo
kikuu cha polisi, akatoa ile taharifa
ya mauaji, ikatayarishwa gari,
ikambeba yeye pamoja na askari
wengine watatu, wakaondoka, huku
nyuma wakifuatiliwa kwa karibu na
gari la wahandishi wa habari,
wakaenda hadi eneo la tukio,
likapigwa picha pamoja na maiti
zote, kisha miili ya marehemu
ikawekwa ndani ya gari, safari ya
kurudishwa Dodoma mjini ikaanza,
walipofika, maiti zote zikaenda
kuifadhiwa katika monchwari ya
hospitali ya mkoa, kisha polisi
wakafanya kikao na waandishi wa
habari, kuhusu ule mlolongo wa
matukio ya kutisha, ila kwa bahati
nzuri, Sajenti Minja alikuwa na
kitambulisho cha Omari Said Mkwiji,
kwa hiyo akawapa nafasi waandishi
wa habari waipige picha, huku
Sajenti Minja akiwaambia ile picha ni
ya mmoja kati ya wale watuhumiwa
watatu wa mauaji na akaongeza
kuwa mtuhumiwa mwingine (Denis)
amekufa katika ajali iliyotokea wakati
wanakimbizana na polisi.
Kesho yake asubuhi, magazeti yote yalitoka na
habari hizo za mauaji, na pembeni
ya hizo habari kulikuwa na picha
kubwa ya Omari, akitajwa kama
mmoja wa wahusika wa mauaji ya unyonyaji damu.
*******************
Wakina kayoza walipoingia ndani ya basi, walikaa
siti ya nyuma kabisa, siti ya mbele
yao walikaa wakina mama wawili
ambao walikuwa wanazungumzia juu
ya mauaji ya kutisha yaliyotokea kati
ya Dodoma na Morogoro.
"na tena hadi picha ya muuaji imetolewa"
mama mmoja wapo. ambae alikuwa
kabeba mtoto katika miguu yake
alikuwa akimsimulia mwenzie,
"imetolewa na gazeti gani?" yule
mama mwingine wa makamo
akamuuliza yule mama mwenye
mtoto.
"magazeti yote unayoyajua
wewe wametoa hiyo habari" mama
mwenye mtoto akajibu.
"chumbageni
si hapo tu tunakaribia, nitanunua
gazeti ili na mimi nione" yule mama wa makamo
akajibu.
Kipindi chote wakati
wanaingia, hadi safari ilipoanza,
wakina Omary walikuwa
wanawasikiliza tu, ila habari
iliyowashtua ni kuchapishwa kwa
picha ya Omary kwenye magazeti.
"Bab hii ishu imeshakuwa kubwa kupita kiasi" Kayoza alimwambia mwenzake wakati wale wakina mamá wanaongea,
"Maji tumeshayavulia nguo, kuyaoga haina budi" Omary aliongea kwa sauti ndogo,
"Maisha ya kukimbia kimbia tutaishi mpaka lini sasa?" Kayoza aliuliza kwa masikitiko,
"Kila lenye mwanzo halikosi mwisho" Omary alijibu kifupi.
Walipofika karibu na
chumbageni, ile gari ikasimama kwa
dharura, kulikuwa na mushkeli katika
upande wa injini, wale wakina mama
wakanunua gazeti, wakawa wanasoma
ile habari
"mimi nikimuona, yaani
haraka nawajulisha polisi" yule
mama mwenye mtoto aliongea.
"hata mimi, mwenzangu milioni kumi
nyingi" yule mama wa makamo
akajibu baada ya kusoma habari
kuwa atayemkamata au atakayefanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa atapewa kiasi
hicho cha pesa, kipindi chote hicho wakina Kayoza walikaa tu kwenye siti za nyuma ya gari, hawakuthubutu kushuka.
Gari lilipotengemaa likaendelea na
safari. Kipindi chote Omari alikuwa
kaielekeza sura yake sanjari na
dirisha ili kukwepa sura yake isionekane na abiria wengine kwa maana alishapatwa na wasiwasi.
Gari ikafika mwisho wa safari,
watu wakaanza kutelemka, wale
wakina mama kwa ajili ya kuwa na
mtoto, ikabidi wasubiri ili watu wote watoke na wao watoke wa
mwisho, sasa wakati wakina kayoza
wanawapita, Omary akamkanyaga yule
mama mwenye mtoto kwa bahati
mbaya,
"samahani mama" Omary
akamtaka radhi yule mama huku akimwangalia
usoni, yule mama akapata mshtuko,
"ah!, si ndo
huyu?" Yule mama alisema kwa kupayuka..
*****ITAENDELEA*******