Watu wawili, wanaweza kuwa wanafanya kazi sehemu moja, biashara moja, wana elimu sawa, wana kipato sawa, lakini mmoja akapiga hatua sana kifedha huku mwingine akibaki kwenye umasikini. Na hapo wote wanategemea kipato kimoja tu, hakuna anayeanza na cha ziada na mmoja akapiga hatua sana kifedha huku mwingine akibaki kwenye umasikini.
:
Hii ndiyo hali ambayo ukienda popote utaikuta, na hii inatuonesha kwamba kinachowatofautisha watu kwenye fedha siyo kiasi cha fedha wanachoanza nacho au walichonacho, bali jinsi wanavyofikiri inapokuja kwenye swala la fedha.
:
Mtu mmoja atapata fedha kidogo na kuitumia kama mbegu ambayo inamwezesha kufanikiwa zaidi kifedha. Mwingine atapata fedha kidogo na kusema haitoshi chochote na hivyo kuitumia yote, akisubiri mpaka apate nyingi kitu ambacho kimekuwa hakitokei.
:
kila kitu unachopanga kuhusu fedha, lazima kwanza urudi kwenye msingi mkuu ambao ni fikra ulizonazo kuhusu fedha
:
Kama unafikiri unahitaji fedha nyingi ndiyo uweze kuanza chochote, kama unafikiri kiasi ulichonacho sasa hakitoshi, na kama unajiambia kwa pale ulipo sasa huwezi kuanza mpaka upate fedha nyingi unazotaka, unahitaji kubadili fikra zako kifedha, kwa sababu zitakuwa kikwazo cha mafanikio makubwa kwako.
:
Mafanikio kifedha yanaanzia kwenye fikra za kifedha ambazo mtu unakuwa nazo. Ukiwa na fikra bora, fikra za uwezekano na fikra za kuanza na ulichonacho, popote ulipo lazima utapiga hatua zaidi