ELIMU BIASHARA
MAISHA HAYAKO SIRIAZI SANA
Kama unaweza kuuza Bagia 200 kwa siku makazini, kwa siku za kazi tu kwa sh 300 kwa bagia moja, zidisha siku za kazi 20 kwa mwezi mara idadi ya bagia ni 20x200= 4,000/=, alafu zidisha mara bei 4000@300 = 1,200,000/= kwa mwezi mmoja. Alafu zile za kuuzia majirani fanya ndiyo mtaji wako wa Biashara, hivyo monthly tayari una tofali 1200pcs (kwa bei ya 1000 kwa tofali) ndani ya mwaka mmoja una tofali za kutosha lavish house hata ya 3 bedrooms, mwaka wa pili ukiisha ukichanganya na incomes zingine unajikuta tayari umepaua na ushaanza finnishing, 👏
.
.
Wewe endelea kuzurura na vyeti vyako vya degree ukitafuta greene pasture halafu ukiwa njiani umechoooka unakutana na muuza bagia unanunua Bagia nne kutuliza njaa huku unashushia na maji ya kandoro huku ukiimba kimoyomoyo iko siku utafanikiwa wakati huna proper skills, huyo unaenunua bagia zake 10 yrs to come atakuajiri kwa kiwanda chake cha kutengeneza bagia kwa mshahara atakaopanga yeye, don't look for greener pastures zilizoandaliwa na wengine bali jiandalie mwenyewe kwa kuanza from the scratch.
Usiwaze sana kuhusu soko la bagia, tafuta shule za msingi na sekondari zilizo karibu yako, tafta vijana wawili au mmoja wakusaidie alafu nenda kauze mapumziko na muda wa kutoka shule. Usilalamike sana kuhusu hesabu, fanya katika 1.2m gharama yako ni 500,000/=, so faida ni 700,000/=, sawa na tofali 700. Unakajua kale Karestaurant kapo pembeni ya Ngome? Uliza wafanyakazi wa town wananunua vitafunwa wapi.
JIKUNG'UTE, JIPANGE, ANZA.
*UTAJIRI UNAWEZEKANA ANZA SASA*
By Agribusiness Expert
Latino McOwino