Ulikuwa ni usiku wa baada ya Sherehe ya Ndoa yangu. Nilikuwa nimechoka.
Nilihitaji kuoga na kupumzika, maana nilicheza sana hivyo miguu ilikuwa ikiniuma kutoka na kuvaa viatu virefu.
Mume wangu alikuwa akinitania utani wa hapa na pale. Zaidi alikuwa akinihitaji kwa ajili ya tendo la Ndoa usiku ule.
Sikumlaumu, najua mwanaume yeyote asingetaka kupotezana nafasi usiku wa Ndoa yake tena ukizingatia wakati wa uchumba wetu nilikuwa nikimzuia kukutana kimwili mpaka tutakapofunga Ndoa.
Wakati akiendelea na utundu wake wa kunishawishi, tulisikia mlango ukigongwa. Nikafikiri, ni nani anaetugongea usiku ule wa saa sita? Nilishangaa.
Baada ya sekunde kadhaa tukasikia sauti ya Mama (Mama Mkwe wangu) ikiita kutokea nje ya Mlango. "Diana, Michael, fungueni mlango." Michael akainuka, akavaa nguo zake na kwenda kufungua mlango.
Mama na Mawifi zangu wawili wakaingia ndani na kukaa kwenye kochi lililokuwemo mule ndani. Kisha akaanza kuongea.
"Diana, sijui kama kuna mtu yeyote alishawahi kukwambia hiki kitu ninachotaka kukwambia."
Nikauliza ni kitu gani hicho?
Akaendelea..
"Diana, kuna laana fulani katika ukoo wa Mume wangu. Yaani Baba Mkwe wako. Watoto katika Ukoo wa huyu mume wako hufuatwa na laana fulani ya kutofanikiwa mara tu wanapooa ikiwemo uzao wao wa kwanza kufariki."
Akaendelea..
"Kutokana na nilivyoelezwa ni kwamba, moja ya mababu zake alimuua mtoto wa Mganga wa kienyeji maarufu aliyekuwepo pale kijijini kwao na huyo Mchawi akaweka laana kwamba, kwa kila mtoto atakaezaliwa, akija kuoa na kuzaa mtoto uzao wake wa kwanza utafariki na wataishi kwa umasikini"
Kisha Mama mkwe akamaliza kwa kuniambia hivi ;
"Mwanangu, sababu kubwa ya kukueleza haya nataka uelewe kwamba, Ndoa yako sio maziwa na asali lakini ni vita kubwa."
Nilishangaa mno. Kwanini sikuambiwa hayo kabla?
Hata hivyo, nikamwangalia na kumwambia haya ;
"Mama, samahani, na mimi sikukwambia haya. Nakuomba unisikilize. Hata mimi natoka katika familia ambayo huwapigania wale tunaowapenda. Baba yangu (Yesu Kristo) alikufa wakati akijaribu kuwaokoa anaowapenda.
Ukoo wangu hauna laana kwa sababu tunaishi chini ya Baraka za Mwenyezi Mungu - Yohana 1:12-13. Hivyo, yeyote atakayeoa/kuolewa katika ukoo huu automatically atakuwa amebarikiwa. Laana, visasi na taabu vitakuwa si sehemu ya maisha yake. Kwahiyo Mama wala usijali, mwanao hayupo katika sehemu ya laana hiyo."
Mama mkwe akanitazama kwa mshangao na hata wale Mawifi zangu nao ambao naambiwa kila mmoja alifiwa na mtoto wake wa kwanza wakanitazama wasiamini ninachowaambia.
Nikaendelea kuongea...
"Mama, wewe nenda kapumzike. Najua tutakua tumechoka sana. Tutaonana kesho.
Mama mkwe akainuka akaondoka akifuatana na wale mawifi zangu.
Nikamgeukia Michael aliyekuwa amekaa ameshika kichwa. Nikamvuta karibu yangu na kumueleza haya ;
"Nisikilize Michael Mume wangu. Mimi sijali Mababu zako walifanya nini, lakini kwa kuwa upo na Mimi na Unamuamini MUNGU wangu, tutafanikiwa tu, iwe katika uzao wetu, shughuli zetu na kazi za mikono yetu.
Nisikilize mume wangu, Paulo pamoja na Wahalifu kadhaa walikuwa kwenye Meli. Bahati Mbaya Meli ile ilitaka kuzama baada ya kuharibika ikiwa majini. Askari walitaka kuwaua wafungwa waliokuwemo ndani ya meli ile ili wasitoroke, lakini Mkuu wa Askari akazuia wasiuawe ili tu, kumuokoa Paulo. Kwa ajili ya kuokoa Maisha ya Paulo, Wafungwa waliokoka kifo.
Hivyo Michael Sweetheart, kwa Sababu umenioa mimi, kwa sababu tupo kwenye meli moja. Ndio, meli moja. Meli ya Ndoa, Kwa jina la MUNGU wetu Mkuu naapia hautokuja kuadhibiwa kwa makosa na laana za mababu zako.
Nilimhakikishia Michael.
Kuanzia siku ile, Hilo likawa Ombi langu kubwa kwa MUNGU wangu. Nilikuwa nikiomba kila siku kwa MUNGU amuokoe Mume wangu na laana za shetani za kipumbavu pamoja na uzao wangu ujao.
Kwa MUNGU hakuna jambo linaloshindikana, hivi sasa ninao watoto Watatu wenye afya, Nguvu na maarifa. MUNGU anazidi kuwapigania, pamoja na kupigania familia yangu pamoja na ukoo wa mume wangu!
Mungu alibadilisha kabisa muelekeo na mawazo ya mume wangu na ukoo wake kiujumla.
____________________________________
Wanawake ni Asset kubwa ya kubadilisha hali. Tupate wapi wanawake wanaojua kuomboleza? Wanawake ni baraka kwa maisha ya mwanaume!
Mwanamke bora anapokuja katika maisha ya mwanaume, milango ya mafanikio hufunguka, upendo, utulivu wa nafsi hutamalaki. Laana, visasi na maumivu hupotea.
Wanawake, Ombeni sana kwa ajili ya waume zenu. Maombi yenu yanafanya kazi, maombi yenu yatamuokoa na aibu yoyote ile !
Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA. - Mithali 18:22
God bless you .
Please share.