```
Unashangaa Simba kufungwa 10 mechi mbili ila hushangai Simba kucheza hatua ambayo ww toka uzaliwe hujawahi kuiona timu yako ikicheza.
"Hii ni sawa na mtu asiejua kusoma wala kuandika lkn anamcheka mtu kua anamwandiko mbaya"
Unashangaa Simba kufungwa 10 mech mbili ila hushangai Simba kufunga goli 8 mechi mbili(au hukuiona hiyo).
Unashangaa Simba kufungwa 10 mechi mbili ila hushangai club Africain kufungwa 8 mechi moja. Wakti huo, Club africain inatoka ligi bora yenye kila kitu sembuse Simba inayocheza ligi yenye timu kama Yanga na Ruvu shooting.
Unashangaa Simba kufungwa 10 mechi mbili wakti Brazil( taifa bora kabisa kwa mpira) alipigwa 7 mechi moja.
Yani huna mtoto, halaf unamcheka jirani yako kua mtoto wake mbaya.
Kwa vlabu vya Africa Mashariki, kufika tu kwenye hiyo hatua ni mafanikio makubwa mno. Ndyo maana Ezra na kelele zake zote na umri wake wote hajawah kuishuhudia Yanga ikicheza hatua ya makundi CCL.
Joachim leo ana mpaka familia lkn hajawah kuiona yanga ikicheza hatua hiyo.
Lkn mtoto aliezaliwa 2000 tu tayar ameishuhudia Simba ikicheza hatua hiyo mara mbili.
Ezra umesema Fedha za manji zlikua na impact kuliko za Mo eti kisa hukufungwa 10 kama Simba.
TUWEKE KUMBUKUMBU SAWA HAPA.
1: Ni kipindi cha Manji Yanga ilipigwa 5: 0 na Simba.
2: Ni kipindi cha Manji yanga ilipoingia hatua ya makundi CCL( ww ulikua hujazaliwa) hakushnda hata mechi moja kwenye kundi lake. Alimaliza na alama moja tu.
4: Ni kipindi cha Manji hata kuingia hatua ya makundi shirikisho ilikua shida na kila ulipoingia ulimaliza wa mwisho mwenye kundi.
Hayo mafanikio ya hela ya Manji unayoyasema ni Yapi.
Linapokuja Suala la mafanikio kimataifa Simba ndo baba wa taifa hili.
Mfano.
1: Ni Simba pekee tz imewahi kucheza nusu fainali ya shirikisho africa.
Hii Ezra mpaka kizazi chetu hiki kinakufa hutaiona yanga ikifika hatua hiyo.
2: Ni Simba pekee tz ambayo imewahi kucheza robo fainal ya CCL. Ezra mpaka mwanao anazeeka hataiona Yanga ikicheza hii hatua.
3: Ni Simba pekee tz imewahi kumuondoa bingwa mtetezi wa CCL, Yanga juzi tu walishndwa hata kumfunga Gor mahia wa hapo Kenya.
4: Ni Simba pekee tz ambayo imecheza hatua ya makundi CCL mara 3.
Emu leta rekodi za Yanga kimataifa tuone.
My take:
Mashndano ya CCL hatua ya makundi na kuendlea siyo Makalio kwamba kila mtu anayo, hiyo ni hatua ambayo "only giant clubs play" ndio maana Africa mashariki yote ni timu moja tu iliyoingia hatua hiyo.
Hata hivo, timu znazotoka kwenye ligi bora ndizo hufanya vzur.
Kwa mpira wa Africa, Al ahly ndo Real madrid ya africa.
Kwao kombe la CCL ni kama ligi tu yandan, wameshabeba mara nying kuliko club nyingne yoyote africa(mara 8).
Kwa kiwango cha ligi yetu, na aina ya timu zetu( East Africa yote) mashndano haya siyo size yetu. Hivo inapotokea timu ikafika hatua ya makundi inamansha kua kwenye vilabu 16 bora Africa nzima siyo suala rahis.
Kipigo kile cha jana siyo aibu hata kidogo, bali ni uharisia wa soka letu lilivyo.
HABARI ya kwamba mpira wa Simba niwamdomoni, je, mpira wa Yanga wa mguuni umefanya nn cha maana kimataifa.
Kama yanga anaecheza mpira wa mguuni alifungwa 8 mechi mbili( tena na vibonde wa hapo Kenya, halaf shirikisho) utashangaaje Simba yenye mpira wa mdomon kufungwa 10 na Bingwa mara 8 wa CCL tena kwenye club bingwa.```