Notification texts go here Contact Us Buy Now!

Simulizi - Bora ungekufa kesho Mwanangu Sehemu ya 3

Sehemu ya 2 Ilipoishia........ Penina alishawishika kuuliza nn kinamsibu Dada yake aliambiwa ni UKIMWI Wakati fulan Tedy alipo mwona penina alimlilia na kumwambia Mdogo wangu unaona mm nakufa ivyo acha umalaya"

Simulizi;Bora ungekufa kesho Mwanangu
Mtunzi;Ashrafu Mbaraka
Sehemu ya 3

Ilipoishia........

Penina alishawishika kuuliza nn kinamsibu Dada yake aliambiwa ni UKIMWI
Wakati fulan Tedy alipo mwona penina alimlilia na kumwambia
Mdogo wangu unaona mm nakufa ivyo acha umalaya"

Usiku majira ya SAA mbili Tedy alifariki dunia mikononi Mwa Penina

ENDELEA..........
Mm nikifikiri kifo cha Tedy kingekuwa ni somo zuri na pengine kingetosha kubadili maisha na fikra za Penina
Penina akupenda kufa kana Tedy aliogopa mateso yale kuliko maelzo aliona ni bora upate ajali mbaya na kufa apo apo kuliko kushuhudia mataso ya aina ile
Lakini penina baada ya wiki alionekana tena mitaani akijiuza kama mtu asiyena habari yoyoye ya msiba wa Tedy na mateso yake
Kilichosababisha arudi kilikuwa ni ugumu wa maisha kazi alizojaribu kutafta aliulizwa vyeti na hakuwa navyo,kuna mabosi waliomuomba awape rushwa ya ngono na Mara tu walipo pata wakitakacho walimwacha kama alivyo akazurura sana mwisho akaona kama ni kifo kipo tu si la kufanya zaidi ya mateso akarudi kwenye umalaya akiwa na lengo la kusakanya mtaji ili afanyebiashara hatimaye aache kazi hiyo

**********..........................**********

Khalfan alimlea Faraja mtoto wa Penina bila kugundua ukweli tena Kwa mapenzi ya kipekee na ukizingatia Kwa miaka mingi amekuwa akitamani kuitwa baba alimpenda sana Faraja na kumdekeza sana alikuwa tayari kufanya uadui na mtu yeyote atayejaribu kumvuruga Faraja
Faraja alipougua Khalfan akulala alikesha usiku kucha akimwangalia Faraja kiasi kwamba alishibdwa hata kuzifanya kazi vizuri
Akihangaika Mara ambebe mara amlaze mara Iv,alikuwa na mapenzi ambayo yalimtisha hata Zainabu akiwaza siku akija kugundua mtoto si wa kwake huenda akauwa.

Sasa twende Kwa Zainabu mke wa Khalfan; Zainabu alikuwa mwanamke Malaya sana kiasi cha kutishia amani hata Khalfan alilijua hili lakini akusema kitu na zilikuwepo tetesi mtaani kwamba Zainabu alimwendea mumewe Kwa sangoma ili awe mpole
Zainabu tabia hii chafu alianza tangu akiwa mdogo na ilisababishwa na mazingira aliyokulia mamake pia alikuwa akifanya na asilimia kubwa ya watu wanyumbani kwao ndivyo walivyo
Zainabu kabla ya kukutana na Khalfan alikuwa kishatoa mimba nyingi sana kiasi cha kumsababishia ugumba asiweze kubeba mimba tena
Alipoolewa alijaribu kujizuia asifanye lakini ilishindikana na sasa alianza kutembea na vijana wadogo sana wanaofaa kumuita mama na pengine hata bibi
Wengi ni wanafunzi ambao huwashawishi Kwa kiasi kikubwa chapesa
Zainabu ni mgonjwa waVvu)virusi visababishavyo ukimwi lakini Khalfan ajui chochote kile. Kwa sababu ya usiri wa Zainabu
Zainabu ndiye anayeipaka matope nyumba ya Khalfan ampaka kuwafanya watu wahisi utajiri alionao Khalfan unasababishwa au unatokana na nguvu za Giza kwani vijana wengi waliofanya kaz kwake na waliokuwa majirani zake,hata baadhi ya marafiki zake walikufa vifo vibaya sana
Ikihisiwa Khalfan ndiye aliyewauwa Kwa kuwatoa kafara lakini ukweli ni kwamba Zainabu ndiye aliyehusika Kwa kuwashawishi na kufanya nao mapenzi ambapo aliwambukiza gonjwa la hatari na walikufa Kwa mateso makali mfano wa Tedy
Hakuna uchawi ila tamaa zao wenyewe ziliwauwa
Zainabu alijua yote haya hata mumewe alijua mda si mrefu atakwenda

Siku moja Zainabu alimwomba mumewe waende matembezi katika fukwe za bahari wakiwa na mtoto Faraja ambaye sasa alikuwa anakaribia kuandikishwa darasa la kwanza walishinda huko wakicheza na Faraja mchana kutwa
Wakiwa huko Khalfan alipigiwa simu ofsini kuna mtu anamuhitaji na niwamuhimu
Alimsogelea mkewe na kumweleza

Jaman mume NDO nn?alilalamika Zainabu

Mke wangu ndo yule mteja wa ule mzigo niliokwambia kafata ivyo,"

Aah kumbe wahi mume usichelewe kurudi utatukuta"

Khalfan alingia ndani ya gari na kuondoka kwa kasi
**************

Dk chache tu simu ya Zainabu iliita alipoangalia alikuwa mumewe akapokea

Hallow?

Mke nipo hospitali ya taifa muhimbili nimepata ajari"

What? "

Nakuomba uje"simu ikakatwa na Zainabu akupoteza mda akaondoka akijua mumewe ndo kaumizwa huku akilia mpaka hospital na kufanikiwa kumwona mumewe nje ya ICU chumba cha wagonjwa mahututi

Nini kimekupata mume wangu"ndo swali la kwanza la Zainabu

Nimegonga mtu na hali yake ni Mbaya sana"
.Yuko wap "

Humu ndani na huu ndo mzigo wake"

Zainabu akachukua na kuanza kupekua ndani alikutana na kitambulisho cha kupigia kura
Jina PENINA DAVID

Hata kabla Zainabu ajasema kitu mlango ulifunguliwa na dokta akatoka nje akiambatana na wauguzi kadhaa nyuso zao zilionekana za kawaida zisizo hashiria hatari jambo lililowapa Faraja Zainabu na mumewe
Aliyekuwa wakwamnza kuuliza n Khalfan

Ooh usijali ndugu mgonjwa wako alipaata mshituko tu ajaumia na mnaweza kuondoka nae kama hamtajali yupo sawa kabisa japo anamichubuko Kidogo katika mkono wa kushoto"alisema Daktari na Khalfan alimkumbatia mkewe huku wakiongozwa kuingia chumba hicho kumwona Penina
Walimkuta amekaa kitandani
Zainabu alimwangalia kwa mshtuko Kidogo Penina na kumtazama mwanae aliyemshikilia mikononi
Walimchukua Kwa lengo LA kumpeleka nyumban wanakoishi lakini Penina alikataa walimbembeleza lakini aikuwezekana mpaka wakafika mahali anapoishi Penina wakati huo wote wawili hawa walikuwa wakishangaa na kustaajabu kwani Penina kafanana kila kitu na mtoto mpaka vidole vya mikono
Karibuni jamani hapa ndo napoishi"yalikuwa n Maneno ya Penina wakati akiwaaga
Asante tutakuja kukuona"

Nyumbani usiku hule Khalfan akuweza kutulia akimuuliza mkewe kuhusu Penina
Umeona walivyofanana mke wangu?"

Akina nani?"

Penina na Faraja utafikiri mtu na dadake ama kwel duniani wawili wawili"

Siku zilizidi kwenda na Khalfan alizidisha ukaribu Kwa penina aikupita siku ajaenda kumtembelea na akimsaidia mambo mengi sana kuna wakati akimuuliza Penina kuhusu kazi anayofanya na Penina akuficha alieleza waz tu mm Ni changudoa
Khalfan aliumizwa sana na historia. Ya Penina kiasi cha kumfanya atoke machizi na alimua kumwajiri katika moja ya kampuni zake kama.msimamizi
Ujue maisha ndo yanayofanya muonekano wa mtu uweje
Khalfan siku zilivyozidi kwenda alianza kushangazwa.na.mabadikiko ya Penina Penina alipendeza sana ,Penina kajazia sehemu zote stahiki lait ungemuona kawa binti mrembo sana kuliko maelezo aliwaliza wanaume wengi
Khalfan bila.kutegemea alijikuta akimpenda Penina sana mpaka kushindwa kujizuia na kuona bora.amweleze.tu ukweli

Penina samahan"

Bila samahan.boss"

Ujue nakupenda sana.na natamani kukuoa "alisema Khalfan kitu kilichomfanya Penina kushika mdomo wake Kwa mshangao kwan hakutegemea kusikia maneno haya kutoka.katika kimywa cha Khalfan mtu akiyemweshimu sana,na anatambua vyema ana mke na mtoto Penina akijikuta akishindwa kukubali ombi la Khalfan kwan anamuheshimu sana Zainabu na hayupo tayari kuwa chanzo cha matatizo katika familia hiyo,

Asante kaka Kwa msaada wako lakini kuhusu hili sipo tayari"

Kwa nn penina?"

Katika maisha yangu sijawahi kuwaza kuolewa na mume wa mtu nayafahamu vizuri matatizo yake,unajua mifano ninayo mingi tu...."alisita na Khalfan akiendelea

Kuhusu Zainabu usijal isitoshe dini inaruhusu Penina "

Hapana jaman m nifukuze tu kazi nirudi mitaani njoo na ubebe kila ulichonipa kwangu......."alisita tena baada ya kumwona Khalfan akipiga magoti Kwa lengo LA kumbembeleza na kuendelea Jaman unafanya nn kaka?$

Nakupenda penina"

Penina akujibu kitu zaidi ya kuondoka na siku iliyofuata akuonekana kazini
Khalfan akukoma akiendelea kumfatilia Penina mpaka mkewe aligundua ilo lkn akuwa mkali kama ilivyokuwa inategemewa alichokisema kumwambia mumewe
Wewe Khalfan mwache mtoto wa watu usije kumsababishia matatizo taarifa zako ninazo"
Na hakuongeza neno jingine kwan wakati huo alijuwa akisumbuliwa na kikohozi
Basi siku zilivyozidi kwenda Zainabu alianza kupungua uzito bila sababu na kuugua homa za Mara Kwa Mara karibu kila wiki alipelekwa hospital
Homa ikawa homa wakati huo Khalfan alikuwa nje ya nchi kikazi
Zainabu akaanza kukohoa na hatimaye akapata kifua kikuu TB alilia usiku na mchana na akimwomba mumewe arudi upesi kuna kitu anataka kumweleza
Maumivu ya ugonjwa yalipomzidi kiasi cha kumfanya asiweze kunyanyuka,mwili mzima ulitapakaa vidonda kutokana na vipele ungemuona usingeamini kitandani na Khalfan bado ajarudi Zainabu alimtumia ujumbe penina aje nyumbani kuna kitu akitaka kumwambia
Lkn penina hakuweza Kwa hofu tu ndipo Zainabu alipochukua karatasi na kalamu na kumwandikia muwewe barua Mbili akimwomba mama yake azitunze
Zainabu naye alifariki alfajiri ya siku ya pili na Kwa kuwa waislamu awacheleweshi mazishi alizikwa siku hiyo hiyo uku akiwachaa vijana wengi wakiwa wamekata tamaa ya maisha wengine wakijiua wenyewe Kwa sababu wakigundua sababu ya kifo chake

(Mjukuu usipo jifunza kutokana na
Hadith hii pole sana)

ITAENDELEA..........

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.