⏩haiitaji mambo makubwa kuundeleza moto wa mahaba ktk ndoa yako, mambo madogo madogo unayoyapuuza na kudhani sio ya muhimu ndio Hasa yanachangia pakubwa katika kujenga ndoa yako na uimara na mafungamano yakudumu.
Njia ya 6 kufanya mahaba yenu yaendelee kung'ara
1)NENDENI KITANDANI PAMOJA
Kwenda kitandani Pamoja na mwenza wako itasaidia sana kuendeleza moto wa mahaba ktk ndoa yenu, Aidha Hakikisha Wewe na mwenza wako mnapata kiwango kizuri cha usingiz kila siku, mwenza wako akiwa kitandani mfuate Muwe wote kwa pmj mkibadilishana mawazo mbalimbali sio mwenza yupo kitandani ww upo seblen unachati.
2)PUNGUZENI MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII
Kushikamana sana na mitandao ya kijamii humaanisha una mda mwingi sana wa simu yako na muda mdogo kwaajili ya mwenza wako, jambo ambalo litaathiri vibaya ndoa yako Utafiti mmoja kuhusu Mwenendo wa binadam umebaini kuwa kuna uhusiano hasi kati ya matumiz makubwa ya mitandao ya kijamii na furaha ya ndoa yako, unapokua nyumban kwako na mwenza wako weka pemben simu achana na mitandao ya kijamii kua bze na mwenza wako,
3)JARIBUNI MAMBO MAPYA PAMOJA
Kujaribu vitu vipya Pamoja na mwenza wako itasaidia sana kuendeleza moto wa mahaba ktk ndoa yenu , wataalam wa haiba na saikolojia wamebainiwanandoa wanaojaribu mambo mapya mara nyingi huwa ni wenye uhusiano wenye ubora mkubwa ,Kua mwenye mawazo mapya kwa mwenza wako na kushauriana mambo mapya mara kwa mara
4)MKUMBATIE MWENZA WAKO MARA KWA MARA
Kumkumbatia mwenza wako mara kwa mara huimarisha afya ya ndoa yenu, Kumbatio la mara kwa mara hutuma ujumbe chanya kwa mwenza wako na kukufanya Wewe uhisi utulivu kwa mwenza wako, mume unapokwaruzana na mke wako mmbembeleze mueke kifuani, mkumbatie na mwambie maneno matamu utaona atajirud na kua sawa, naww mke unapokwaruzana na mumeo jisogeze kifuani kwa mume wako mmbembeleze, mkumbatie na mwambie maneno matamu na utaona atakavyojirud
5)USISAHAU KUSEMA "AHSANTE "
Mara nyingi huwa tunajisahau sana kiasi cha kuhisi kwamba sio muhimu kuwashukuru wenza wetu kwa kutusaidia kazi mbalimbali au kwa kutununulia zawadi, kumshukuru mwenza wako hata kama jambo ni dogo kuufanya upendo wenu kuendelea kua hai, Jenga taratibu ya kusema neno ahsante,,,mume unapopikiwa chakula na umekula umeshiba Jiwekee taratibu ya kumwambia neno "ahsante kwa chakula mke wangu " iyo itasaidia pia,,Na pia mkimaliza raha zenu za tendo la ndoa kuweni na mazoea ya kupeana ahsante ya kazi mlioifanya usione tabu kwambia mwenzio ahsante mke /mume wangu Hakika nimeEnjoy hny wangu kweli Wewe umenijulia.
6)ONDOENI MAZOEA KATIKA TENDO LA NDOA
Ongeza vitu maridhawa katika maisha yenu ya kitandani ili kuondosha uchoshi kwenye tendo, njia mojawapo ni kufanya tendo ktk style tofauti au eneo toafuti tofaut, tendo sio lazima lifanywe Chumbani au kitandani, linaweza kufanywa sehemu yoyote Iwe chini ya capert kwenye kochi, kitandani, jikoni, na maeneo mengne unayoweza kuyabuni.
⏩Hayo machache ukiyapenda yachukue yanaweza kukusaidia kuonekana mpya ktk ndoa yako
#DumishaNdoaYako
