*__*
Moyo waliopewa WANAWAKE akipewa Mwanaume hata kwa Siku 2 tu LAZIMA AFARIKI!
Ule uwezo wa kuvumilia Maumivu ya Kuzaa ndio huwa unawafanya wavumilie mambo wanayotendewa na Wanaume kiasi ambacho hadi wewe Mwanaume unajiuliza,
HADI HILI AMENISAMEHE, INAWEZEKANAJE!
Kama kuna jambo Wanaume huwa wanakosea basi ni kudhani kwamba Wanawake ni Wajinga.
Hawajawahi kuwa Wajinga ila Wameumbwa na Moyo wa Uvumilivu uliopitiliza..
Na Mungu aliwatengeneza hivyo makusudi...
Mwanamke anaweza kumvumilia Mwanaume ambaye kwa Miaka 10 hamtimizii mahitaji yake lakini Mwanamke yupo tu..
Uvumilivu ulioje! Mwanamke anayeweza kukaa na Mwanaume mlevi anayempiga ngumi kila akirudi ila yeye yupo tu..
Sio kwamba ni Mjinga,LA HASHA!Ni katika ule Uvumilivu tu.
Kasheshe ni pale Mwanamke huyu ANAPOCHOKA...
Anaweza akavumilia miaka 10...Unampiga...Anakufumania..Humfikishi Kileleni..Ila Siku Akichoka akasema KWAHERI,
Ule Moyo wa Uvumilivu huwa UNAGEUKA na kuwa JIWE GUMU na hata uimbe mashairi ya "Bado ananijia ndotoni ila nikiamka simuoni bado ananijia nikilala Haki ya Mungu sio masihara"
Sijui kaimba nani yule mimi nimemsahau
Utaimba sana lakini HATARUDI na utabakia kiwete wa mahaba yake daima...
-------------------------------------------------------------------
USHAURI WANGU:
Kabla hajafikia wakati ws KUKUCHOKA, chondechonde kumbuka na yeye ana Moyo,MPE ANACHOSTAHILI!
Usichanganye Uvumilivu wake ukadhani ni Ujinga,ITAKUGHARIMU.✍