Notification texts go here Contact Us Buy Now!

MOYO ULIOJAA MAUMIVU SEHEMU YA 38

MOYO ULIOJAA MAUMIVU

SEHEMU YA 38

Violeth alikuwa akilia, Theo alivyomwangalia, alishindwa kuvumilia, akaenda pembeni na kuanza kulia.

Moyo ulimuuma mno, hakujua ni maneno gani ambayo alitakiwa kumwambia mke wake huyo aliyekuwa na kiu ya kuwaona watoto wake, alihisi kabisa angeumia mno lakini pamoja na hayo yote ilikuwa ni lazima aujue ukweli juu ya kile kilichokuwa kimetokea.

“I want to see my twins...” (nataka kuwaona mapacha wangu...) alisema Violeth huku akilia.

Daktari na manesi walipata kazi kubwa kumtuliza mpaka kutulia. Baada ya kuona wamefanikiwa, akamfuata Theo na kumwambia sasa ulikuwa ni muda wa kumfuata mke wake na kumwambia kila kitu kilichokuwa kimetokea, hakutakiwa kumficha kwani endapo angefanya hivyo lingekuwa kosa kubwa sana.

“Ila ninaumia sana...” alisema Theo.
“Najua! Jikaze, wewe ni mwanaume...” alisema daktari.

“Atalia sana...itakuwaje? Nitashindwa kuvumilia,” alisema Theo huku akiyafuta machozi yake.

“Unatakiwa kuvumilia...” alisema daktari.
Hakuwa na jinsi, akajifuta machozi na kumfuata mke wake pale kitandani.

Alipomwangalia, alihisi kitu chenye ncha kali kikiuchoma moyo wake, aliumia kupita kawaida kwani kwenye vitu ambavyo hakutaka kabisa kuviona katika maisha yake basi yalikuwa machozi ya mke wake.

Violeth alimwangalia mume wake, bado moyo wake ulimwambia kulikuwa na jambo kubwa lililokuwa likiendelea, alihitaji kujua, alitaka kuambiwa ukweli ili kama kulia, alie, ahuzunike lakini mwisho wa siku akubaliane na ukweli juu ya kile kilichotokea.
“Mke wangu...” aliita Theo huku akimwangalia Violeth.

“Niambie ukweli...niambie ukweli mume wangu...” alisema Violeth huku akilia.
Theo hakuwa na jinsi, alitakiwa kufanya kama alivyoambiwa, alimwambia mke wake ukweli kwamba alijifungua watoto wawili kama walivyotaka lakini mtoto wa kiume ambaye walipanga kumpa jina la Harry alifariki dunia.

“Mume wangu...mume wan...” alisema Violeth lakini hata kabla hajamalizia sentensi yake akaanza kulia.

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.