MOYO ULIOJAA MAUMIVU
SEHEMU YA 27
“Na hiyo harusi itafanyikia hapa au Ufaransa?” aliuliza mwandishi.
“Hapahapa Tanzania!”
Kila walilolisema ndilo lililofanyika kwani baada ya kupita mwezi mmoja, hatimaye Theo na Violeth wakafunga ndoa kwenye Kanisa la St. Joseph lililokuwa jijini Dar es Salaam na watu hao kuwa mume na mke.
Harusi hiyo ilikuwa gumzo, kanisa hilo lilijaza watu wengi, kila mmoja alitaka kushuhudia kilichokuwa kikienda kutokea. Wengi walipiga picha kwa ajili ya kuweka kwenye mitandao yao ya kijamii, waandishi wa habari walikuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha wanapata picha ya kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
Wanandoa hao walikuwa na nyuso za furaha, walimshukuru Mungu kwa kutimiza ndoto walizokuwa wamejiwekea za kufunga ndoa na kuwa pamoja.
Kila mtu Tanzania alikuwa bize kufuatilia harusi hiyo iliyokuwa gumzo kila kona.
Masupastaa wengi duniani walihudhuria, walifurahi na kuona hatimaye yule msichana mrembo, ambaye mpenzi wake alikufa kwenye ajali ya ndege hatimaye alikuwa akiolewa na mwanaume mwenye pesa na maarufu mno barani Afrika.
“She is very beautiful,” (ni mrembo mno) alisema mwanamke mmoja, alikuwa ni Naomi Campbell, mmoja wa wanamitindo maarufu duniani.
|
|
Je, nini kitaendelea?
Kumbuka hii ni miongoni mwa simulizi zinazoumiza na kufundisha mno. Endelea kunifuatilia.