MOYO ULIOJAA MAUMIVU
SEHEMU YA 13
“Oh! I’ve nothing to say.” (Oh! Sina cha kuongea)
“No! Tell me, what is it?” (hapana! Niambie kitu gani)
“I’m the lucky guy in the world by now?” (mimi ni mtu mwenye bahati sana duniani kwa sasa) alisema Theo.
“Why?” (kwa nini?) aliuliza Violeth huku akitoa tabasamu pana.
“I have sat next to an extremely cute girl in the world,” (nimekaa pembeni ya msichana mrembo mno duniani) alijibu Theo na wote kuanza kucheka.
Theo hakutaka kufuatilia tena kinyang’anyiro kilichokuwa kikiendelea, alibaki akizungumza na Violeth tu. Muda wote alikuwa akimwangalia msichana huyo, uzuri wake ulimchanganya, hakujua ni kwa jinsi gani alibahatika kukaa pembeni yake.
Alijisikia amani, furaha kubwa huku moyo wake ukianza kuingiwa na mapenzi mazito ambayo hakuwahi kuwanayo kabla.
Kila alipomwangalia Violeth alisikia sauti moyoni mwake ikimwambia kwamba huyo ndiye mwanamke ambaye alitakiwa kuwa naye, kumuoa na kujenga familia pamoja.
“Violeth! Nilisikia kuhusu mume wako! Pole sana,” alisema Theo kwa sauti ya chini.
“Ahsante sana. Ila unaniangalia sana mpaka nasikia aibu,” alisema Violeth huku akiachia tabasamu.
“Najua! Nashindwa kuyatoa macho yangu kwako.”
“Kwa nini?”
