Notification texts go here Contact Us Buy Now!

KUFILISIKA NI JAMBO MOJAWAPO TARAJIWA KWA MFANYABIASHARA

kuna watu wanajisikia aibu kukiri kufilisika. Ni jambo la kawaida tu mtu kufilisika.

Unapofanya biashara unakuwa na leseni ya biashara, unalipia kodi ya mapato.

Biashara ya inayoleta faida ndio huendelezwa. Biashara isiyo na faida husitishwa.

Ukisitisha biashara unawataarifu TRA vingine wataendelea kukuhesabia kodi.

Mwaka 2014 nilikuwa nikitoa huduma ya usafirishaji abiria Singida-Iguguno-Kiomboi-Singida chini ya IGUGUNO EMPIRE nikaona biashara hailipi, nikaamua kusitisha biashara kwa maana ya kufilisika.

Huwezi kufanya biashara ya kujionyesha ni tajiri wakati haupati faida yoyote, hiyo itakuwa ujinga uliopitiliza.

Kuna mambo mengi yanaweza kuchangia kuyumba kibiashara.  Umefungua chuo kwa pesa nyingi unakosa wanafunzi au gharama za uendeshaji zinakuwa kubwa kuliko mapato au sawa na mapato.

Umeanzisha gazeti utakutana na ujio wa mitandao ya kijamii, unajikuta watu wanapata Breaking news tu hivyo hawasomi magazeti.

Unanunua teksi, ujio wa bodaboda na bajaji unakuelemea.
Una Kiwanda cha maji watu wanakunywa kandoro mtaani.

Angalia bongo movie walivyokutana na changamoto ya uuzaji wa kazi zao.

Hapo unalazimika tu kutangaza kufilisika kama biashara hailipi.

Umefungua duka la nguo kubwa lakini miezi mitatu umeuza suti mbili tu. Watu wanaangalia kipaumbele muda fulani, badala ya kuvaa wanaangalia tumbo kwanza.

Unauza kuku watu uchumi umebana hawali kuku ili wabane matumizi. Wanakula tu maharage na matembele tu.

Tuwe wakomavu wa biashara, biashara ikiyumba ujue unahitaji mbinu mpya.


About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.