*JE WAYATAMBUA HAYA*
*NDOA*
Ili mja aishi kwa amani na furaha hapa duniani, jambo la kwanza ambalo anatakiwa kuwa nalo ni kuridhika na Kukinai kwa yale aliyojaaliwa na Allah mtukufu.
Tukirudi katika ndoa zetu mwanamke, kitu cha kwanza ambacho inatakikana uwe nacho ni kuridhika na muwe alokuchagulia mola wako mtukufu na uache kukodolea macho waume wa nje.
Hili ni jambo la kwanza ambalo litakusaidia kuingiza furaha ndani ya ndoa yako
*Jambo la pili nitakalo lizungumzia ni namna unavyoongea na mumeo.*
Kuwa mpole na mwenye heshima kwa mumeo, na kitu cha kwanza kinachodhirisha viwili hivyo ni ulimi wako ( kuongea).
Usimpandishie sauti mumeo mnapoongea, tumia lugha nzuri, usiwe muongeaji sana wa kuwa unaulizwa moja unajibu mia.
Jaribu kunyamaza unapokuwa na hasira kwani kuongea ukiwa na hasira kichwani unaweza kuongea maneno machafu yasiyokuwa na hesima kwa mumeo.
Ipambe na uilainishe sauti yako unapoongea na mumeo ili izidishe mvuto kwa mwenza wako.
*Jambo la tatu nitakalojizungumzia ni namna unavyopaswa kuishi na familia ya mumeo.*
Mwanamke katika familia ya mumeo yafaa uwe mleta amani na si mvunja amani.
Kwa kawaida mwanamke anapoingia katika familia ya mume, kunao watakao mpenda na kunao watakao mchukia.
Katika hali hii mwanamke yatakikana uwe na subra ya hali ya juu kwa watakao kuchukia, usilipize chuki kwa chuki na jaribu kufunika baya kwa jema.
Jiepushe kuongea ubaya wa familia ya mumeo kwa watu, na ujiweke mbali na watu wanaopenda kuongea ubaya wa familia ya mumeo.
Waheshimu wazazi wa mumeo kwa namna vile ungependa wako waheshimiwe.
*Jambo la nne nitakaloliligusia ni uke wenza.*
Kwanza kabisa napenda kutoa pongezi kwa wenye waliukubali uke wenza ambao ni mtihani mkubwa sana kwa idadi kubwa ya wanawake wa kiislam.
Ni wanawake wengi sana wameomba talaka au pia kujivua katika ndoa zao na kuwaacha watoto wao wakitesea mikononi mwa mama wa kambo kwa sababu waume zao wameongeza mke wa pili.
Mume kuongeza mke si sababu ya kisheria kwa mwanamke kuomba talaka hivyo hali hii itakuwa miongoni mwa kuomba talaka bila sababu. Na mjumbe wa Allah (rehema na amani ya Allah iwe juu yake) alisema;
*"Hatoingia peponi wala kusikia harufu ya pepo mwanamke anayeomba talaka bila sababu"*
*Jambo la tano ambalo nitaligusia ni namna ya kudumisha penzi.*
Baadhi ya ndoa huvunjika na sababu *si* kuwa waliooana hawakuridhiani, sababu kubwa huwa ni mwanamke kukosa mbinu za kupalilia na kulikuza penzi lao.
Baadhi ya wanawake wanapojua kuwa wanawapendwa na kuthaminiwa sana na waume zao, huchukua fursa hii kuwanyanyasa waume zao badala ya kutafuta mbinu za kulipalilia penzi hilo ili lizidi kunawiri.
Penzi haliwezi kudumu kama halitapaliliwa. Mwanamke wacha kujiachilia, tafuta mbinu tofauti tofauti, kuwa mbunifu, mfurahishe mumeo udumishe penzi lenu.
*HITIMISHO*
Ndugu zangu katika iman tujitahidi saana wanandoa kuvumiliana, kama hatuna uvumilivu ndoa haiwezi kudumu.
Tujitahidi sana kwa hili kwani kila mwanadamu ana mapungufu yake tuvumiliane ili ndoa zetu ziweze kudumu.
Mwanaume huwezi kumpata mwanamke aliyekamilika kila kitu na wala mwanamke huwezi kumpata mwanaume aliyekamilika kila kitu.
Kikubwa zaid ni *kuvumiliana na kuelekezana!!*
*MWISHO*
*Ukiyapenda yachukue kama yalivyo*
➿➿➿➿➿➿➿➿➿➿