ULIMWENGU WA MBWA MWITU.
# PHYZZOELPRESENT :
# pinifapetv
TELL- +255 655 207 957
Sehemu ya 01....
Dunia hii ilipo ubwa, Mungu alituweka ili tuwe watawal wa vitu vyote vya dunia hii, leo hii binadamu ndio anamtawala binadamu mwenzake,kua pamoja nami katika simulizi hii na ya kufundisha ukupata kitu usisahau ku share.
ulikua ni usiku wa kwanza tu mimi na mke wangu kitandani, mke wangu aliitwa Janeti Kaki, na mimi nikiwa na fahamika kwa jina la Michael Msisili, usiku ulikua wa kwanza kwasababu ndio tu mchana wake tume funga pingu za maisha, wakati tuko kitandani nilifikiria mengi kwanza usingizi ulikua hauji, nilimuangalia mke wangu na niliruhusu taratibu mkono wake upite kwenye kifua changu, huku akiniangalia kwa macho yake malegevu yenye kutoa shukrani kemu kemu kwa kuolewa kwake,mikono yangu haikuona aibu kumvuta vizuri mabegani mwangu na kumbusu usoni, nilimwambia tume pambana sana tangia tulipo kua wachumba na sasa mke na mme, japokua nyumba yangu ni ndogo hakuna shida tuta jenga tu na tutaishi au tuhame sinza mpenzi, alidakia ndio huku akipitisha mkono wake kwenye kifua kuelekea chini > tuhamie bwani, huko tuanzi maisha yetu mengine yatosha kukaa mchokole ,, nilimkubalia mke wangu na tulipanga bei ya kuuza nyumba ile,hatukua na mpango wa kujenga bali tulienda kutafuta nyumba ya kifahari kidogo yenye thamani ya milioni70,baada ya wiki kuisha tulihamia rasmi bwani, nyumba ile ilikua vile vile kama tulivyo iacha, tulianza kutoa mizigo kwenye gari na kuanza kupanga ndani, ya jumba lile, wakati tunaendelea kushusha vitu mara mke wangu alimuona mzee mmoja ambaye ni bibi akipita na kuangalia nyumba yetu kwa jicho baya sana kisha akapiga hatua akatema mate nakuondoka, tukio lile lili mtisha sana mke wangu na kuliogopa, alikuja kwangu na kunieleza lakini nilimwambia usihofu kila kitu kitakua sawa mana hatuja mzulumu mtu yeyote, niliwapa hela vijana walio kua wakinisaidia kushusha mizigo na kuingiza ndani bila kusahau usafiri walio kuja nao.Niliingia na kuanza kurekebisha baadhi ya vitu na kutega vizuri mapazia kwenye madirisha, mke wangu aliniita nifunge jiko la gesi haraka ili aweze kupika mana kulikua kunaenda jioni,ilikua si kazi kubwa nilifanya haraka iliniendele na mambo mengine,baada ya masaa kadhaa nyumba yetu ilipendeza , baadhi ya vitu vilikua vime sha pangika, nilipiga simu na kuagiza kihifadhia maji (tank) na wauzaji waliniambia litafika kesho, nilijituliza kwenye kochi nikiwa na subiri mkewangu amalize kupika, punde mkewangu alimaliza kuivisha ugali na alikwenda nje kumwaga takataka lakini gafla alirudi akiwa anakimbia, aliniita kwa sauti >> mume wangu njoo uone kitu cha ajabu, ,niliamka fasta mahala nilipo kaa na kumfuata mke wangu alipo,alinishika mkono na kutoka na mimi njee aliniambia angalia huku nayeye akiniangalia mimi, lakini mimi nilipo tazama mbele sikuona chochote, alipo ona naangalia kana kwamba natafuta kitu nae aligeuza macho yake kuelekea kwenye galala na kukuta hakuna kitu, aliniachia mkono na kwamshangao alitahamaki kutokuona kitu, nilimuuliza kwani kulikua na nini eneo lile, alinijibu huku akiwa anahema kwa kasi >> palikuwepo na mbwa mwitu wengi wanakula nyama, pale galalani tulipo pachimba leo, sasa nashangaa wametoeka?, nilishuka na kuangalia maeneo yale hakukua na damu wala nyama yoyote hata nyayo za hao mbwa hazikuonekana, nilirudi na kumwambia mke wangu, unajua tangia tuje kwenye hii nyumba umekua hueleweki mara umeona bibi amepita na kutema mate, saivi umeona mbwa , mbona mimi sioni kitu chochote,naelewa kua yaweza ikawa umesikia hadithi za watu kama nilivyo sikia mimi eti watu wanakimbia mji huu kwasababu ndugu zao wanapotea na wengine wanakufa, huu ni mji wawachawi ndo mana unakua na presha, nilimcheka na kumvuta nikamkumbatia, nilimwambia mambo yazamani yakipita hayawezi kurudi, hizo hadithi zazamani zisikuchanganye , mbona kunawatu bado wanaishi katika mji huu, nimekuleta huku ili ufurahi,gafla sufuria ndani ilianguka na wote tuka shtuka na kuachana katika kukumbatiana na mke wangu aliogopa na kuhofia kua labda ndo wameamua kuja na huku ndani tena, alikua na mashaka lakini nili msogeza pembeni nikaingia kwa ujasiri mkubwa ndani na kutizama kilicho tokea..................