UGONJWA WA PULLORUM KWA VIFARANGA (MUHARA MWEUPE)
Ni ugonjwa unaoenezwa na bakteria SALMONELLA PULLORUM. Hupitia kwenye mayai hadi kwa vifaranga. Vifaranga hupata ugonjwa wiki ya 3 baada ya kuanguliwa, pia huweza kupata ugonjwa kwa kula chakula chenye bakteria wa ugonjwa huu.
DALILI
1. Vifo hutokea siku 10 za mwanzo baada ya kupata ugonjwa.
2. Vifaranga hulegea mabawa, huzubaa na kupiga kelele.
3. Vifaranga huchechemea na kuanguka kabla ya kufa.
4. Vifaranga huvimba matumbo.
5. Vifaranga HUARISHA KINYESI CHEUPE KAMA CHAKI, KINYESI HUGANDA SEHEMU YA KUTOLEA HAJA.
6. Vifaranga hukosa hamu ya kula.
UPASUAJI (POSTMORTERM FINDING)
1. Maini na mapafu huvimba.
2. Maini huwa meusi sana.
3. Mapafu hupauka.
4. Moyo huwa na maji maji ya damu.
5. Maungio ya miguu ya kuku mgonjwa huvimba.
TIBA
1. Tumia dawa kama TRIMAZINE 30%, TRISUL, ESB3, n.k.
2. Fanya usafi wa banda, tenga kuku wagonjwa na wahudumie bila kuchanganya vyombo vya maji na chakula.
ASANTE....!