Notification texts go here Contact Us Buy Now!

SIMULIZI: JASTINA-SEHEMU YA 08

JASTINA
SEHEMU 8

ENDELEA..

Alias na miaka mitano Jestina alimpoteza mtu muhimu sana katika familia yake, Bi Prisca aliaga dunia baada siku chache tokea kusheherekea mwaka wa tano tokea kuzaliwa kwa Jestina. Hili lilikuwa pigo kubwa sana hasa kwa Jestina kutokana na mapenzi makubwa aliokuwa nayo juu ya bibi huyo. Walifanya maziko na kuomboleza baada ya hapo kila mtu alirudi kwake, na kadri muda ulivyokwenda Jestina alikaa sawa na kuendelea na maisha kama kwaida kwa sababu alielewa hapa duniania tunapita tu na kila mtu ipo siku atakufa.

Kutokana na uwezo mkubwa wa akili Jestina na Alwin walipelekwa shule ya vipaji maalum, na huko moto uliwaka wanafunzi wengine waliisoma namba maana wawili hao walikuwa hawapitiki. Hiyo ilipelekea mpaka wanafunzi wengine kuwachukia lakini wao hawakujali hilo, kwao masomo yalikuwa wanayapa kipao mbele. Miaka ilisonga mbele huku kila siku uwezo wao akili ukizidi kuwa mkubwa, hatimae walimaliza shule ya msingi na kujiunga na high school kwa ajili ya kujiendeleza na masomo zaidi. Kwa wakati huo Alwin alikuwa na miaka kumi na tatu na Jestina alikuwa na kumi na mbili.

Pamoja na umri mdogo lakini uzuri wa Jestina uliwavutia mapaka shume na kuanza kumtongoza. Lakini wengi waliambulia pakavu, lakini kwa Alwin ilikuwa tofauti japo yeye alimpenda alishindwa kumwambia. Lakini aliuonyesha dalili zote za upendo hata hivyo Jestina hakuonyesha dalili zozote za kumpenda zaidi ya upendo wa kirafiki tu.

Maisha yalisonga mbele huku walimu wakivutiwa sana na juhudi za wawili hao japo walikuwa magenius, hatimae walimaliza high school na kujiunga na college. Sasa Alwin alikuwa na umri wa miaka kumi na saba na Jestina alikuwa na umri wa miaka kumi na sita, uzuri wa Jestina ulizidi kunawiri huku ukitii kanuni za kibaolojia.

Macho yake makubwa yalimpendeza yakisindikizwa na uso wa duara uliopambwa na pua ndogo nzuri pamoja na mdomo wenye lipsi ambazo muda wote ziling'aa. Hakuwa na kifua kikubwa lakini kilitosha kumueleza rijali yeyote kuwa tayari kifua hicho kilishamea vya kutosha, kiliambatana na mdidimio mkubwa kiunoni na hips zilitanuka vizuri sana huku zikiruhusu mwili huo uonekane kama nambari nane ambayo imeandikwa na fundi alieumba kila kitu.

Kwa kweli uzuri wake ulipitiliza sasa na kuanza kuwachanganya walimu pamoja na wafaunzi na kila aliepishana nae njiani. Wapo waliojikwaa na kudondoka, wapo waliokosa kupata ajali kwa kumshangaa pindi anapopita, lakini kwa Alwin yote hayo yalikuwa yakawaida sana ukizingatia yeye amekua nae. Wakiwa college ukaribu wao ulimjengea uhasama mkubwa Alwin na kujikuta akipewa vitisho mara kwa mara. "Jestina na Alwin munaitwa ofisini" aliingia mwanafunzi darasani na kutoa tangazo hilo. Bila kuchelewa waliinuka na kuelekea ofisini walipoitwa.

ITAENDELEA..

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.