JASTINA
SEHEMU 7
ENDELEA
Alwin: "haiwezekani kwa sababu swala huyo kashakufa tayari, kauliwa na simba"
Swali la nne: " Clinton ana uraia wa nchi mbili wa Jamaica na wa Brazil, alizaliwa Jamaica lakini sasa anaishi Brazil, kwa sababu za kisheria Clinton hawezi kuzikwa Brazil. Je sentensi ya mwisho ni kweli ama uongo?"
Alwin: "ni kweli, kwa sababu Clinton bado hajafa"
Swali la tano: " kuna wakati kipindi cha christmas, Santa Claus hakuwapa watoto zawadi. Alikwenda North pole akiwa na chupa mbili za wiski, chupa tatu za wine na chupa nne za bia katika begi lake. Alikunywa zote mpaka tone la mwisho kisha akalala. Alikuja kuamka saa tatu asubuhi akiwa na chupa tisa ambazo zinakaribia kuwa tupu. Ikiwa sentensi tatu za mwanzo ni kweli basi sentensi ya mwisho ni kweli au uongo"
Alwin: "uongo, kwa sababu kumebakiwa na tone moja katika kila chupa, hata hivyo hakuna asubuhi wakati wa decmber katika north pole, kuna usiku tu".
Swali la sita: " kati ya namba hizi ipi haigawinyiki kwa tano. 786, 981 na 123"
Alwin: "zote zinagawanyika, ukichukua 786 gawa kwa tano unapata 157.2, 981 gawa kwa tano unapata 196.2 na 123 gawa kwa tano unapata24.6"
Maswali yaliendelea mpaka yote yalipoisha akawa amejibu yote kwa usahihi bila kukosea hata moja. Baada ya hapo alipelekwa katika chumba kingine lakini huko waliambiwa hawaruhusiwi kuingia ndani hivo walisubiri nje. Baada ya nusu saa daktari alitoka na Alwin na kuwaambia kuwa wasubiri muda si mrefu watapata majibu. Robo saa baadae daktari alitoka na ripoti kamili ya Alwin huku akitabasamu na kuwaomaba wamfuate. "kwanza niwape hongera kwa kuwa na kijana mwenye uwezo mkubwa sana wa akili, Akili ya Alwin inafanya kazi kwa kasi mara nne zaidi kuliko binadamu wengine, ninaposema hivyo namaanisha kuwa Alwina ana uwezo mkubwa sana wa kufikiri.
Hii hapa ni ripoti yake kamili , ana IQ ya 170 . Hii ndio sababu ya yeye kupata ugumu katika kushirikiana na wenzake kwa sababu uwezo wake wa kupambanua mambo si wa kawaida, hivyo lolote utakalo mwambia basi yeye atalitafutia maana kwa undani zaidi"
Daktari aliendelea kuawafafanulia tabia za Alwin na kuwaambia kuwa wasipokuwa makini basi watamsababishia matatizo makubwa sana kwa sababu akili yake huwa haiko tayari kulazimishwa kufanya jambo ambalo halitaki. Baada ya kuelezwa kila kitu walifanya malipo na kuondoka zao kurudi nyumbani, wakiwa njiani "Umejuaje kama Alwin ni genius" aliuliza Mr Kelvin. "ni kwa sababu hata Jestina pia ni genius lakini yeye IQ yake ni 150, na ile puzzle waliokuwa wakishindana kuipanga nilipewa na daktari ili nimpe mwanangu wakati anaposhindwa kutatua jambo, ni watoto wachache sana ambao wana uwezo wa kupanga puzzle ile wakati mawazo yao yapo kwengine, wakati ule wakishindana mawazo yao yalikuwa ni kwa jinsi gani wangeweza wangeweza kukabiliana na umati mkubwa wa watu uliokuwepo ukumbini. We unadhani hawakutuona wakati tuna warikodi, walituona lakini kwa vile kimawazo hawakuwa pale basi hawakutushughulikia tu.
Usiniulize nimejuaje yote haya, ni kwa sababu nimesomea saikoloji" alijibu Mr Hendrix na kumfafanulia rafiki yake kila kitu. Walifika nyumbani kwa Mr Hendrix na kuagana, Mr Kelvin aliekea kwake akiwa na furaha kubwa sana na alipofika alimueleza mkewe kila kitu.
ITAENDELEA..