Notification texts go here Contact Us Buy Now!

SIMULIZI: JASTINA-SEHEMU YA 03

SIMULIZI YA KUSISIMUA

JASTINA SEHEMU 3:

ENDELEA...

Sijamaanisha uondoke hapa, hapa wewe ni kwako na mpaka mwisho wa maisha yako utaendelea kuishi hapa. Ninachomaanisha ni kwamba uache kufanya kazi tu kula utakula na mahitaji yako yote nitakupatia"Aliongea Hendrix na kumkumbatia bibi huyo ambae alimpenda kupita kiasi. "kama ni hivo sawa ila naomba kitu kimoja tu, niwe nacheza Jestina" aliongea bibi huyo huku machozi yakimtoka jambo ambalo Hendrix alilikubali kwa mikono miwili.

Baada ya hapo aliamuru chumba cha Jestina kiongezwe kitanda kimoja kikubwa kwa ajili ya Prisca na kazi hiyo ilifanyika siku hiyohiyo kisha kila kitu cha bibi huyo kikahamishiwa chumbani huko. Ukweli bibi huyo alikuwa akimpenda sana Jestina na yeye ndie alieshauri kuwa mtoto huyo aitwe Jestina.

Jestina alikuja na baraka ndani ya nyumba hio, maana mambo mengi yalikaa sawa huku bishara zikinawiri. Maka ilisogea na hatimae ilifika siku ya kusheherekea kuzaliwa kwa Jestina akiwa anatimiza miaka mitatu, watu wengi sana walialikwa katka sherehe hiyo. "mke wangu fanya haraka tushachelewa" mzee Kelvin alikua akimharakisha mkewe ili wawahi kwenye sherehe. "nishamaliza mume wangu nakuja" alijibu mkewe huku akitoka na mtoto mdogo wa kiume mwenye umri wa miaka minne akiwa amembeba.

Waliwasha gari na kuelekea katika sherehe, na kwasababu hakukuwa mbali, walitumia dakika tano tu mpaka kufika, walishuka kwebye gari na kuelekea ukumbini. "karibu Mr na Mrs Kelvin" aliongea Mr Hendrix baada kuwaona wakiingia, "asante lakini samahani kwa kuchelewa" alijibu Mr Kelvin ambae alionekana ni mwenye busara. "mbona kijana wenu anaonekana hajachangamka" Aliongea Mr Hendrix baada kumuandalia mtoto aliebebwa na mke wa Mr Kelvin. "ah ni kawaida yake huyo hawezi shangwe" alijibu Mr Kelvin huku akicheka, "anaitwa nani" aliuliza tena Mr Hendrix, "Alwin ndio Jina lake"alijibu Mr kelvin huku akimchukua Alwin kutoka mikononi mwa mkewe na kumshusha chini.

"Alwin nenda kacheze na wa wenzako" alimwambia lakini Alwin wala hakusogea hata hatua moja, "mume wangu si unajua mtu mwenyewe huyo hawezi kujichanganya, acha tu nitakaa nae mimi" mkewe aliongea. "muache akacheze na wenzake na wewe nenda ukasalimiane na wanawake wenzako" alijibu Mr Kelvin akiwa amekunja sura.

Bila kuuliza kitu mkewe aliondoka na kumuacha Alwin akiwa amesimama pembeni ya babaake. "unajua sikujali sana hii tabia ya mwanangu kutojichanganya kipindi ambacho nilikuwa naishi nje ya mji huu, lakini sasa hivi lazima ajifunze kwa sababu hapa ni kwao" aliongea Mr Kelvin, basi Mr Hendrix alimwita mfanya kazi mmoja na kumwambia ampeleke Alwin kwa watoto wenzake.

INAENDELEA..

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.