SIMULIZI FUPI YA KUSISIMUA YA
JASTINA SEHEMU 2.
ENDELEA NAYO...
Hiyo imetokana na kuwa, ni miaka mingi sana wameishi katika ndoa bila kupata mtoto japo walipata misukosuko kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki lakini wao hawakujali waliamini siku zote mtoto ni riziki kutoka kwa Mungu. Basi baada kukamilika taratibu zote waliruhusiwa kurudi nyumbani, walitoka hospitalini na kuingia wene gari na kuondoka.
Njia nzima kila mmoja alikuwa kimya akitafakari ni jina gani ampe mtoto wao, walikuja kushtuka baada dereva aliekuwa akiwaendesha kuwaambia kuwa tayari washafika nyumbani.
Wafanya kazi wote walikuwa nje wakiwassubiri kwa hamu, waliposhuka tu kwenye gari watu walipiga vigelegele na kuwakaribisha ndani. Kwa vile walikuwa wamechoka sana waliekee chumbani kwao na kupumzika. Siku ya pili mapema asubuhi waliamka na kushuka chini, walishangaa kukuta kumebadilika sana, kwenye meza kulikuwa na keki kubwa ilioandikwa "Welcome to the world little princess".
Ukweli nyumba hiyo ilijaa furaha kupita maelezo, na hiyo ilitokana pia na ukarimu wa matajiri hao kwa wafanya kazi. Kiufupi hawakuwachkulia kama ni wafanya kazi bali ni kama ndugu zao tu.
Siku kadhaa zilipita na muda wa kumpa jina ulifika, hapo sasa kukawa na mshikemshike maana wafanya kazi wa kike walikuwa wakimsapoti mama na wafanya kazi wa kiume walikuwa wakimsapoti baba. "Bora aitwe Jessey" huyo alikuwa ni bwana Hendrix, "bora tumuite Christina" na huyo alikuwa ni mke wake, mdahalo huo uliendelea kwa muda mrefu bila kupata jibu mpaka iliposkika sauti yenye kukwaruza ikisema "kwanini msimuite Jestina, Jes kutoka Jessey na Tina kutoka christina", "lakini kweli hapo itakuwa vizuri maana atakuwa na jina alilochaguliwa na baba yake na mama yake pia" wote walikubali na kumuita mtoto wao "JESTINA".
"Prisca mama yangu kwanini usiache tena kufanya kazi maana umri ushakwenda sana" Mr Hendrix alimuita na kumueleza hayo mfanya kazi huyo ambae alikuwa akimheshimu kama mama yake maana ndie aliemlea tokea wazazi wake wapo hai mpaka wamekufa na ndie anaejua ni kwa jinsi gani utajiri huo umepatikana "mwanangu Hendrix kama nitaacha kufanya kazi nitapata wapi pesa ya kula" aliongea mwanamke huyo alienekana kuzeeka na umri wake ulikuwa ni kati ya miaka sabini hadi sabini na tano.
INAENDELEA...