Notification texts go here Contact Us Buy Now!

HASSAN MCHEPUKO ALIYEIMARISHA NDOA YA JOHN

Hii ni barua ya Mr John kwa mchepuko wa mke wake aliyeibadilisha ndoa yake na kuifanya ndoa yake iwe imara zaidi.
Habari yako bwana HASSAN
Narumaini hatufahamiani.mimi naitwa mr JOHN au baba Hellen.mkewangu ni ANITA ambae kwa sasa ndio baby wako kipenziiii kwa maelezo niliyoyakuta kwenye simu yake.
Leo nakutumia sms hii sio kwa ubaya bali kwa kukupongeza kwa kumbadilisha sana mkewangu.kitu ambacho hata mapadre na wazazi wake walishindwa.kwakweli Anita wangu sasa hivi kabadilika sanaaa.hanywi tena pombe kupitiliza kama hapo mwanzo,hafokei hovyo watoto na kuwapiga kama mwanzo,harudi nyumbani usiku tena.sasa hivi Anita ananipikia na kunifulia.Nimeshangaa sana.haya mambo niliyasahau muda kutoka kwa mkewangu mpendwa.

Tatizo lilikuwa ni mimi mwenyewe.baada tu ya kunifumania na mwanamke mwengine ndipo mkewangu alibadilika sanaa.mpaka nilijuta.kila jitihada zilishindikana za kumrudisha awe kama zamani.ikawa inapotokea nashindwa kutimiza haja zake za kimwili kama zamani basi ni ugomviiii,naonekana kama nimemalizia nguvu huko nje.

Mabadiliko ya hivi karibuni ndio kitu kimenishangaza.mkewangu amekuwa na furaha kama mwanzo,amekuwa mcheshi na watoto.anapika na kufua.
Lakini nimegundua sababu kubwa ya mabadiliko haya ni wewe HASSAN.toka akupate uwe mchepuko wake amekuwa akikuheshimu sana.amekuwa akikusikiliza sanaaa.nimekuta sms zako nyingi ukimuuliza mkewangu
Anita umepikia watoto?
Anita umemuandalia chakula mumeo?
Anita uko wapi saa hizi muda wa kurudi mumeo,rudi kwako haraka.
Nimefurahi sana kwani nae amekuwa akitii maagizo yako kuliko yangu.

KWELI MCHEPUKO MPYA UNANGUVU KULIKO MUME.
Nimefurahi zaidi kwakuwa hunywi pombe kulingana na imani yako.na hivyo hata yeye umemkataza kunywa pombe na ameacha kabisaaa.hata nilizo nunua mimi ili anywe ziko tu kwenye friji.hataki kabisa kwakuwa anakuogopa.

Wewe ni wanaume wachache sana ambao hutembea na mke wa mtu na bado akahitaji asiharibu ndoa yake.yaan wewe kutembea na mkewangu kumeimarisha sana ndoa yangu.
Hata unapomuudhi wewe huwa najua.maana atashinda hana raha kabisaaaa.
Ahsante sana HASSAN.ila ninachokuomba mwambie na mie asinisahau sana kwenye tendo la ndoa🙈🙈.maana mkiahidiana kukutana wiki ijayo ujue wiki nzima sipewi anakutunziaa🤣🤣.
Naomba umwambie hilo.mimi ni mtu mzima.nahitaji kulea wanangu kwa amani zaidi.pengine nguvu zangu za sasa siwezi mtimizia mahitaji yake ya kimwili.
Bora adui mmoja ninaekujua kuliko akiwa anahangaika ovyo kutafuta kukidhi haja ya mwili wake.

SIKU NJEMA MR HASSAN.
usimwambie Anita kama nimekujua maana atachukia sana na anaweza nuna mwezi mzima.
TUMPENDE MKEWETU.
WAKO MR JOHN


Je! ingekuwa ni wewe umemfahamu mchepuko wa mke wako ndio anayefanya mke wako atulie na kukuheshimu ungefanyaje??

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.