*SEHEMU YA HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI WAKATI WA KUFUNGA KONGAMANO LA 36 CHAMA CHA MADAKTARI WA MIFUGO TANZANIA*
*UKUMBI: Simba Hall - AICC, ARUSHA 07/12/2018*
Mheshimiwa Mwenyekiti wa TVA leo naomba niongee wazi bila kumung'unya maneno mbele ya wajumbe hawa......
1. Wataalamu wa mifugo ninyi ndio mmekuwa wachawi wenyewe katika kuendeleza hii sekta ya mifugo hapa nchini na mmekuwa waharibifu wenyewe wa sekta ya mifugo kwa tabia zenu za kutokuonesha kuthamini mifugo yetu hapa nchini mkitumia hii fani yenu muhimu........ Mhe. Luhaga J. Mpina (TVA conference 07/12/2018)
2. Wataalamu wa mifugo wamekuwa sehemu ya kukandamiza wafugaji na mmejiweka pembeni pale yanapotokea matatizo yahusuyo mifugo na kushindwa kutetea ama kuwasaidia wafugaji na mifugo yao na wakati mwingine kujihusisha kupanga njama za kula rushwa kwa kushirikiana na taasisi zingine wanapokuwa kwenye operesheni mbalimbali ........ Mhe. Luhaga J. Mpina (TVA conference 07/12/2018)
3. Nimewahi kukuta mahali ng'ombe takribani 1,600 waliokamatwa Hifadhini na kushikiliwa kwa muda mrefu bila chakula wala maji huku takribani ng'ombe mia tatu wakifa kwa njaa na msongamano na wakati eneo hilo hilo likiwa na wataalamu wa mifugo ambao kwa utaalamu wao ndio wanapaswa kuzijua vema na kuzisimamia na kuzitetea sheria za ustawi wa wanyama na sheria ya magonjwa ya mifugo ambazo zinaelekeza wazi namna ya kuhifadhi wanyama hao. Lakini katika tukio hilo hakuna afisa hata mmoja aliyediriki kutoa taarifa aidha kwa maandishi au hata kwa simu ama kukemea kitendo kile cha kikatili na badala yake waliwaacha ng'ombe wale kuendelea kufa kwa kukosa chakula na maji na kulundikwa sehemu isiyostahili......... Mhe. Luhaga J. Mpina (TVA conference 07/12/2018)
4. Hivi kwann afisa mwingine anaweza kujitokeza na kukamata mifugo kwa kusema anatumia sheria ya Hifadhi za wanyama pori na eneo hilo hilo mtaalamu wa mifugo anashindwa kusimama na kujiamini kutetea na kutoa maelekezo ya matakwa ya sheria za mifugo? Badala yake afisa mifugo naye anaungana nao na kupanga mipango ya kula rushwa kutoka kwa mfugaji na kuendelea kumkandamiza mfugaji.......... Mhe. Luhaga J. Mpina (TVA conference 07/12/2018)
5. Ninaongoza Wizara ngumu inayomgusa mwananchi mojakwamoja na yenye changamoto kadhaa. Katika wizara yangu upande wa mifugo kuna shida sana ya watu kutokuwa na ushirikiano, wataalamu wa upande wa mifugo wengi ni wabinafsi ambao hawataki kushirikiana na wengine ili kuendeleza sekta, badala yake wamekalia kujionesha kuwa wamesoma sana. Kwa upande wa Fisheries wako vizuri na wanashirikiana sana...... Mhe. Luhaga J. Mpina (TVA conference 07/12/2018)
6. Tanzania inayo mifugo mingi na takribani asilimia 80 ya ng'ombe wanaouzwa minadani wanapelekwa kuliwa nje ya nchi, wengi wao wanatoroshwa na wachache ndio wanalipiwa hizo tozo kidogo tunazotoza wakati madaktari mpo na mmejiweka pembeni kabisa, kwahyo kwa tafsiri rahisi ni kwamba Tanzania ndo shamba la kufugia ng'ombe na mbuzi ila nyama inaliwa nje ya nchi na ninyi ni madaktari wa nje ya nchi......Mhe. Luhaga J. Mpina (TVA conference 07/12/2018)
7. Madaktari wengi mmejiweka pembeni huku mkiacha wafugaji wakihangaika bila msaada wa utaalamu mlio nao na wakati mwingine kujihusisha na shughuli zingine zisizohusu mifugo na ufugaji, maana kama mnafanya kazi kikamilifu mbona hatujawahi ona barua ama tamko la daktari yeyote kulalamika kwamba amezuiwa kutekeleza majukumu yake kama daktari au kuzuiwa kusimamia kikamilifu sheria mnazopaswa kuzisimamia?.......... Mhe. Luhaga J. Mpina (TVA conference 07/12/2018)
8. Madaktari wa mifugo mnapaswa mjitathimini na kuonesha uwezo wenu na sio kujitutumua na kuringia A's ulizotoka nazo darasani. Kama unaringia vyetu pasipo kutatua kero za wananchi ww haufai na waweza kufa na kuviacha vyeti vyako kuliwa na panya tu...... Mhe. Luhaga J. Mpina (TVA conference 07/12/2018)
9. Mheshimiwa mwenyekiti suala la uhitaji wa Madaktari 99 kwa ajili ya mikoa 10 na LGAs 89 nimeliona na ninaahidi kulishughulikia kwa nguvu zote, nitamshirikisha pia mwenzangu wa Utumishi wa umma ili madaktari hao wapatikane na waajiriwe mapema ili tuweze kutekeleza sheria zilizopo........ Mhe. Luhaga J. Mpina (TVA conference 07/12/2018)
10. Mimi uwa nasema kama suala liko ndani ya uwezo wangu na limeibuliwa na mm ndio napaswa kulitatua basi hakuna haja ya kusubiri kwenda huko ofisini ndio nilitekeleze, utaratibu wangu ni kutoa majibu hapo hapo nilipo. Na nilishaelezwa na DVS kuhusu jukumu la uteuzi wa maDVO na kwa kuwa kumbe nina uwezo wa kuwateua basi pia ninao uwezo wa kuwatengua nikiona sijaridhishwa na utendaji kazi wao. Kwahyo; Ninawateua Rasmi madaktari wote wenye sifa kuanzia leo na barua zao za uteuzi zitasambazwa kuanzia Jumatatu tarehe 10/12/2018........ Mhe. Luhaga J. Mpina (TVA conference 07/12/2018)
11. Serikali imetoa dawa za kuogeshea mifugo kwa ajili ya majosho yote yaliyo mazima nchi nzima, pia serikali itaendelea kutoa dawa hizo kila baada ya miezi sita na zoezi hili litakuwa endelevu mpaka pale serikali hii ya awamu ya tano itakapo maliza muda wake. Wafugaji watachangia gharama ndogo kulingana na kikokotoo tulichoweka ili waweze kumudu kuogesha mifugo yao kununua ile dawa inayohitajika kuongezewa kila baada ya michovyo 1,000 na wataalamu wa wizara watapita kuungana na walioko LGAs kutoa elimu kwa wafugaji wetu. Kwahyo madaktari mkasimamie utekelezaji huo na hakuna mfugaji atakayeachwa asiogeshe mifugo yake. Pia tutafanya ufunguzi wa kampeni ya uogeshaji mifugo tarehe 16/12/2018, madaktari wote mjitahidi kuwepo katika hafla hiyo kule wilaya ya Chato. Pia serikali tayari imenunua mitambo ya kuzalisha chanjo ya CBPP na muda si mrefu tutaanza kuzalisha chanjo hiyo wenyewe, lengo likiwa ni kuweza kupunguza bei za chanjo hizi kwa mfugaji....... Mhe. Luhaga J. Mpina(TVA conference 07/12/2018)
12. Kuhusu mkanganyiko wa mitaala iliyopo kwenye vyuo vya mifugo hili sio suala la kufumbia macho naomba nipate mkanganyiko ulivyo na tutawaona wahusika na kuwataka wafanye marekebisho yanayotakiwa ili kuweza kuzalisha wataalamu tunaowataka........Mhe. Luhaga J. Mpina (TVA conference 07/12/2018)
13. Kuhusu uendeshaji wa shughuli TVLA na ofisi ya DVS, masuala ya uendeshaji wa mazoezi ya chanjo za mifugo na mambo mengine ambayo mtaona yanafaa kwa ajili ya kuboresha na kuendeleza sekta ya mifugo naomba myaandike vizuri na hata kama tutahitajika kutoa Waraka wa Waziri ili kurahisisha utekelezaji tutafanya hivyo. Kwahyo Mheshimiwa mwenyekiti wa TVA naomba leo Muunde timu maalum ya watu watano (5) ambao watakaa pamoja na kuandika mapendekezo yote ya kutekeleza ili kuboresha sekta. Kwahiyo naelekeza wajumbe hao wa timu mtakayounda wakutane Dodoma na kazi hiyo ifanyike ndani ya siku tano (5) kuanzia Jumatatu 10/12/2018 na ifikapo Ijumaa nipate document ya mapendekezo yenu na ikiwezekana na rasimu za Waraka wa Waziri mtakazopendekeza nitoe na mm nitayasimamia mapendekezo hayo na kuyatekeleza.......Mhe. Luhaga J. Mpina (TVA conference 07/12/2018)
14. Kuhusu yale mambo ambayo mnaona yanakwama utekelezaji wake wakati huu ambapo mchakato wa kuwahamishia watumishi wa mifugo kwa Katibu mkuu mifugo haujakamilika, tunaweza kutoa maelekezo kwa 'Waraka wa Waziri' ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu katika sekta ya mifugo na mnaweza kutoa mapendekezo namna bora ya utekelezaji wake.......... Mhe. Luhaga J. Mpina (TVA conference 07/12/2018)
15. Kuhusu Internship kwa madaktari wanaohitimu Shahada ya Tiba ya Wanyama hili ni jambo zuri na muhimu sana na hapa nimefurahi kwa kuwa naamini sasa tutaweza kupata madaktari ambao tayari wameelewa ufugaji ni nini na pengine watapata hamasa ya wao kufuga na kupenda kuhudumia mifugo badala ya kuhitimu na kwenda kufanya kazi zisizohusiana na mifugo. Kwahyo nitalisimamia hili kuhakikisha linatekelezwa maana ni muhimu sana, "kwani kwa nini wengine wasikilizwe na wafanikiwe mambo ya sekta zao alafu sisi tushindwe kufanikiwa"? Naahidi kulisimamia na mnaweza kulijumuisha kweny kazi itakayofanywa na timu hiyo..... Mhe. Luhaga J. Mpina (TVA conference 07/12/2018)
16. Mwisho; Leo nimefurahi sana kupata fursa hii ya kuzungumza na madaktari wangu wa mifugo wa nchi nzima maana fursa niliikosa mwaka jana kutokana na muingiliano wa majukumu, lakini namshukuru pia naibu Waziri aliwasikiliza na kunieleza yote mliyomweleza. Nimekubali na kujibu hoja zote kama zilivyowasilishwa na Mwenyekiti wa chama cha madaktari wa mifugo nchini na naahidi hakuna hata moja litakalonishinda katika kulifuatilia na kulipatia ufumbuzi wake. Asanteni sana....... Mhe. Luhaga J. Mpina (TVA conference 07/12/2018).