Notification texts go here Contact Us Buy Now!

Kadiri wanawake wanavyopambana kujikwamua kiuchumi ndivyo *NDOA* nyingi zinazidi kuingia matatizoni.

Kadiri wanawake wanavyopambana kujikwamua kiuchumi ndivyo *NDOA* nyingi zinazidi kuingia matatizoni.


Tatizo siyo wao kupambana bali tatizo liko hapa: Wanapambana kwa madhumuni gani? Wanawake wengi hawapambani kwa maana ya kuwasaidia waume zao [kama Mungu anavyotaka] bali kwa maana ya kutoka kivyao;

 Ndio maana utawasikia wanaongea kauli zao za kiuanaharakati, " *_Usimtegemee_* *_Mume_* ", "Wanaume hawaaminiki", "Bora mwanamke niwe na uchumi wangu n.k".

Hivi mnajua kuwa...
Kama Mume ni Kichwa maana yake Mke ni Kiwiliwili; bahati mbaya ni kwamba macho na ubongo viko kwenye kichwa na sio kiwiliwili.
Kiwiliwili kisipo kiamini kichwa "Automatically" kitaielekeza miguu kokote na kwa kuwa hakuna macho; mwili( *Ndoa* ) kuumia kutokana na kujikwaa ama kufa kabisa kwa kutumbukia shimoni.

Ngoja niwaambie; *Ndoa* yeyote ambayo Mwanamke amekaa kiuanaharakati uwe na uhakika ilishajifia siku nyingi ama iko njiani kufa na ukiona Wanandoa wanaendelea kuishi pamoja basi ujue ni kwa "kujilazimisha". Sijakutana na Mwanamume yeyote Duniani ambaye anaweza kuishi kwa furaha nyumba moja na Mwanamke anayeleta Tabia za Uanaharakati ndani ya Ndoa.

Nataka ufahamu ....
Ukiruhusu Mwanamke ndani ya Ndoa ajione anaweza kusimama bila wewe (Mumewe) basi, ujue unacheka na nyani na muda wowote tutakuja tukusanye mabua tukalishie ng'ombe wetu.
Kuishi na mke hakuhitaji *_DEMOKRASIA_* , kunahitaji *AKILI* , ujinga unaofanywa na Wanaume wengi siku hizi ni kuruhusu *_DEMOKRASIA_* kutawala Ndoa badala ya AKILI.

 Wewe kama unadhani Demokrasia ndiyo Uzungu na Mapenzi kwa Mkeo, shauri yako; hao wazungu unaowaigilizia Ndoa zao zishawakimbiza siku nyingi.

Msifanye mchezo wandugu..

Ninawaonya mapema ili nisije kusikia eti mtu ananiambia mke aliemtafuta na kumuoa mwenyewe, amemshinda!

Khaa! Yaani hapo itabidi utandikwe viboko vya mgongo; maana unakuwa umeudhalilisha Uanaume.

Uanaume tafsiri yake ni "Kuishi na Mke wako kwa akili kiasi kwamba abaki akikuheshimu na kuwepo na Amani, Utulivu na furaha ndani nyumba"

 Ukiona mwanamke anakudharau na hakusikilizi basi ujue umeshapoteza Uanaume wako.
Andika hii pointi mahali..
Elewa kwamba Uanaume haukai kwenye suruali bali Uanaume unakaa kwenye *AKILI*   
                                                  
Kila la Heri

Maoni 1

  1. Hakuna jasiri👌SHUPAVU👌 mvumilivu👌mwenye nguvu, mbunifu, mwenye uwezo, mpambanaji na mchapakazi kama mwanamke👰mwanamke simama imara 👌 👌 acha kubweteka. Acheni ile kauli yakusema eti mwanamke akiwezeshwa anawezaa😀😀😀 hata sisi tunaweza kujiwezesha👌 usikae kusubiri nguvu yamtu ikutoe ulipo,👆kuolewa au kuzaa kusikufanye ukakosa haki zako zamsingi👌 simama sasa na uuvae ujasiri. Ukisimama wewe mwenyewe hakuna wa kukukalisha chini tena👌👌 MWANAMKE ❤️ SHUPAVU 🙏🙏🙏🙏
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.