Notification texts go here Contact Us Buy Now!
Machapisho

JINSI YA KUANDAA SINGO

Assalam Alaykum
Habari zenu......🌹

💓❤

 _*Baada ya kuona jinsi ya kuandaa singo ya maziwa leo tuangalie aina nyengine ya utayarishaji wa singo*_

💕 JINSI YA KUANDAA SINGO NO 2 💕


1) Chukua karafuu yako roweka.

2 ) Tia haliudi, rose water, misk, Pompia na Yasmin

3) Tia asumin kavu na mbichi

4 ) Tia bizar ya njano ya unga

5) Tia Oliver oil au mafuta ya nazi

6) Tia powder nyeupe  kidogo na mawarid fresh

✔Changanya vitu vyote kwa pamoja kama umevikamilsha vifaa vyote uzuri ila sio lazima uwe na vyote hivyo.

💕JINSI YA KUMSINGA BWANA 💕

💖Hakikisha chumba chako umeshakifukiza uzuri oga na piga msuaki jifukize mwili mzima na nywele zako pia  weka makeup zako unazopenda mwanamke usafi.

💝Tandika busati, au kanga,  kijikeka kidogo

✔Anza kumueka kichwa chake mapajani mwako
Umsugue shingoni  kifuani, mikononi mpaka vidole ukimaliza mnyanyue kichwa  muwekee mto aulalie juu ya kichwa chake.

Kisha anza kumsugua  tumbo,  sehemu zake za siri msugue vizuri hapo kwa utaratibu bwana mkubwa umuache kama alivyo huyo ana massage yake maalum na vitu vyake maalum.

Wakati unamsugua miguuni unaweza kuweka miguuni yake kwenye mapaja yako na uendelee kumsugua mpaka kwenye kucha na nyayo za miguuni.

❗ Kuna wanaume wengine wazito wameshiba maziwa  ya mama zao hatua nyengine ukiwa huwezi mlaze  tu chini moja kwa moja na uendelee na kumsinga hali ya kuwa yuko chini kalala.

Ukisha mmaliza chukua kisahani  chako kikiwa  na hangerchif  na kinyoleo ikiwa utatumia mashine au kiwembe inategemea mume anavyotumia mnyowe malaika ya sehemu zake za siri na nywele za kwapani.

Ukisha mmaliza mfute fute kwa mkono au kitambaa mabaki yote ya singo then mshike mkono nenda nae Bafuni  mgogeshe .

Ukimaliza kumuosha mfute fute maji kwa Tawla
Kisha mkaribishe  kitandani utachukua mafuta ya Oliver oil au lotion utampaka mwili mzima.

Kinachofuata hapo aidha kumpa haki yk .au kumtengenenezea chakula akala.

Kwa siku hiyo ya singo la bwana ni vyema ukamtayarishia chakula akipendacho.

Asante🌹

BEAUTY AND LOVE ZONE

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.