Msimamo wangu Sehemu ya 09
SEHEMU YA 9 || BY SIMULIZI MIX ENTERTAINMENT
WHATSAP/TXT/CALL: 0712505163||APP,U2BE, FB PAGE&INSTA @Simulizimix
WRITTER: HANS MASLEEN || VOICE OVER: FELIX MWENDA
MSIMAMO WANGU SEHEMU YA TISA
WRITTER: HANS MASLEENNiliamua kurejea mjini musoma!
Huo ndio ulikuwa mwanzo mzuri wa mawasiliano baina yangu na mwanadada aliyeuteka moyo wangu kwa asilimia zote zaynabu msumi.
Urafiki ulinoga huku tukitambulishana kwa baadhi ya marafiki na baadhi ya ndugu pia kujuana!
Hakika zaynabu akawa Rafiki yangu wa kwanza wa kike bora tangu nizaliwe ambapo sikuwahi kumpata hapo awali.
Ila lengo langu la kuanzisha mahusiano na dada huyo nililiweka kiporo huku nikisubiri muda ndio uamue. Nilimtendea mambo mema ili kumvuta dada huyo taratibu ilimradi hata siku nitakayomwambia iwe ni rahisi mno kukubaliana nami.
Mara nyingi tulikuwa tukitumia muda mwingi kutoka out pamoja na dada huyo kipindi cha wikiend. Yaasini pia alinufaika pia katika uhusiano wangu na dada huyo kwani naye alinizoea mno na mara kibao alikuwa akija nyumbani kwangu kipindi cha wikiendi.
Wikiendi ambayo si mimi wala zaynab alikuwa kazini tuliamua kuitumia wikiendi hiyo kwa ajili ya kutoka na kuelezana mambo mawili matatu huku lengo langu likiwa ni kuvunja ukimya niliouweka kwa dada huyo.
Mara nyingi nilikuwa mimi nikimfuata yeye mkoani mwanza kwa ajili ya kutoka out lakini safari hii aliamua yeye kunifuata mimi ndani ya mji wa musoma.
Nilitumia vizuri kufatwa huko kwa dada huyo kwa kumpeleka sehemu zenye vivutio mbalimbali vya mkoa huo. Ambapo tulianzia katika makumbusho ya baba wa taifa , mbuga ya Wanyama na hatimaye tulitafuta restaurant nzuri kwa ajili ya mazungumzo.
Tulitulia ndani ya restaurant nzuri maongezi yakiendelea huku tukifurahia msosi.
“aiseee nimeinjoi sana leo martin na nashukuru sana” aliongea zaynab kiutulivu huku akiionesha furaha hiyo usoni mwake.
“karibu sana!” niliongea huku nikijaribu kutafuta neno zuri la kumwingilia dada huyo. Asikuambie mtu hakuna kitu kigumu kama kumtongoza mwanamke uliyeanza nae urafiki, ni kigumu mno! Nilipata shida sana jinsi ya kumuanza dada huyo. Na cha kushangaza Zaidi hadi muda zaynab kuweza kurudi kwao ukafika lakini sikubahatika kumwambia lolote Zaidi ya kubaki moyoni.
Nilimsindikiza na kumpandisha basi la kwenda mwanza bila kumwambia lolote.
Nilijilaumu mno kwa kosa hilo!
Hakika usiku mzima wa siku hiyo hakuwa wenye Amani kwangu kila nikifikiria kosa nililolifanya mchana wake nilibaki nikijiita mjinga katika kundi la mataira.
Nikiwa kitandani nikitafakari jinsi ya kumueleza dada huyo ndipo nilisikia mlio wa text umeingia kwenye simu yangu.
Nikaiendea simu na kuifungua kwa upesi. Alikuwa ni zaynabu
“good night boy, me nimefik salama” text ilisomeka hivyo
Nikaandika haraka haraka kuijibu meseji hiyo
“ooh hongera mbona mapema walala”
Nikaituma meseji hiyo na baada ya muda ikajibiwa
“nimechoka sana martin wacha nipumzike, takutafuta asubuhi”
Alinitumia meseji hiyo ambayo ilinipa maswali lukuki kuwa atanitafuta asubuhi kwa shida ipi,ina maana nay eye anahitaji kunieleza kuwa ananipenda. Ndipo nikajishtukia swali hilo nikiliandika kumuuliza zaynab.
“kuna shida”
Meseji hiyo haikuweza kujibiwa! Kila muda nilikuwa naangalia simu yangu labda meseji ya mrejesho itaingia lakini ilikuwa waapi!
Kuna muda nilijilaumu kuituma meseji hiyo nikiwaza labda nimemkera kwa swali hilo, nikatamani niifute meseji hiyo lakini wapi hakukuweza kuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Nikabaki mpole nikijilaumu kimya kimya.
Usingizi nao haukuniacha salama nikiweza kuyaacha macho yangu yakiangaza, hivyo ukanichukua na kujikuta nasinzia na hatimaye kulala kabisa!
Mlio mkali wa simu yangu ndio uliokuja kunishtua!
Huku nikiwa na usingizi nikaichukua simu yangu ambayo nililala nayo hapo hapo kitandani, kuangalia nilikutana na jina zaynab. Nilishtuka mno kwani taa ya chumbani humo bado ilikuwa ikitoa mwanga kuashiria bado hakujakucha.
Nilipoyatupia macho yangu kwenye saa ndogo ya ukutani iliyomo chumbani humo niligundua ni saa kumi alfajiri.
Nikaipokea simu hiyo!
ITAENDELEA