hukutaka dini ashike,
bali utandawazi aweke,
na kuficha moyoni mwake.
Umemfunza kuita dady eti kina father ni washamba,
hukumtaka ashike jembe ati hatoishi shamba,
kwenye mitandao akatamba,
ili asionekane mshamba,
mimi sio mtoto wa mtaani, mimi ni mjukuu wako.
sketi fupi na vibamba,
ndivyo ulitumia kumpamba,
filamu za gabo zigamba,
nyumbani kwako hazikutamba,
ila zile zifundishazo ugumba,
mpaka makasha ulipamba,
mimi si mtoto wa mtaani, mimi ni mjukuu wako.
akiwa na miaka kumi na sita,
mwanao mpenzi kapata,
kumkanya ukasita,
ili jina la mumy asije akafuta,
umeshinda nyumbani mwenyewe
hadi muda wa saa sita,
mwanao anarudi kumuhoji ukasita,
eti oooh sweart heart mdamrefu nakutafuta
mimi si mtoto wa mtaani mimi ni mjukuu wako.
"your not the house girl"ndo maneno ulimwambia,
pale ulipomkuta kaamua kujifulia,
mwanao kaugulia,
mimba tumboni imetulia,
kila muda kalilia,
mbali kuitupilia,
ulimshahuri kutulia,
atapojifungua mbali mtatupia,
mimi si mtoto wa mtaani,mimi ni mjukuu wako.
miezi ikatimia,
hospitali mkahamia,
mapesa mkatumia,
duniani nikahamia.
mimi si mtoto wa mtaani, mimi ni mjukuu wako.
ghafla nikawa kero kwenu,
hamkutaka nyumba yenu,
niishimo mimi mwanenu,
mkasaka mr shenu,
mume wa mwanenu,
na kumkabidhi mjukuu wenu,
mimi si mtoto wa mtaani, mimi ni mjukuu wako.
mr shenu mzee wa pombe,
kanitupa kwenye vikombe,
jalalani mitaa ya chang'ombe,
mimi si mtoto wa mtaani, mimi ni mjukuu wako.
kwakudra za mungu nimeishi,
maisha ya kizushi,
leo namkaba mwanaishi,
na kesho mwanahamisi,
mimi si mtoto wa mtaani, mimi ni mjukuu wako.
leo nakuona barabarani,
na gari la mamilioni,
nakuomba shilingi ishirini,
japo nishibe punje kwenye sahani,
chaajabu wanijibu,
huna kitu mfukoni,
je?hiyo petroli garini,
umepewa na jirani?
mimi si mtoto wa mtaani mimi ni mjukuu wako.
nimekufata na nyumbani,
naomba japo sahani,
wanijibu hunakitu ndani,
ila nikitazama shimoni,
naona vyakula vya thamani,
mimi si mtoto wa mtaani,mimi ni mjukuu wako.
umenibatiza jina duni,
eti mtoto wa mtaani,
kwani we unavyodhani baba yangu anaitwa mtaani?
umenitesa sana moyoni,
umeninyima amani,
ndo maana naiba sokoni,
ili hata nikiwekwa kifungoni,
nipate hakika ya kula jioni,
mimi si mtoto wa mtaani,mimi ni mjukuu wako.
nakutakia amani,
hivi sasa niko kifungoni,
kwani ulivyoninyima sahani,
niliiba uraiani,
nikashikwa kwa amani,
na kuwekwa kifungoni,
ni mimi wako mpendwa,
mtoto wa mwanao,
neno moja tuu kwako,
mimi si mtoto wa mtaani mimi ni mjukuu wako