Mahitaji ya kupika biriani
1 kilo mchele wa basmati
1 kilo nyama iwe ya kuku au ng'ombe au mbuzi kata katika umbo dogo la kutosha kula kisha ichemshe na tangawizi na kitunguu swaumu, unga wa binzari (turmeric powder) pili pili manga na chumvi ili kuweka ladha nzuri. Ikisha iva itoe iweke pembeni na mchuzi wake uweke pembeni utautumia baadae.
1 kilo ya vitunguu kata slice ( mviringo)
1 kilo nyanya nyekudu zilizoiva, osha vizuri kisha katakata saizi ndogo ndogo sana
1/2 lita ya mafuta ya kupikia
1/2 kilo ya samli au mafuta yeyote ya kupikia
2 maggi chicken soup cubes
3 kijiko kidogo cha chai unga wa pilipili mwekundu
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa binzari
3 kijiko kidogo cha chai unga wa girigilani (giligilani)
2 kijiko kikubwa cha chakula mchanganyiko wa tangawizi na kitunguu swaumu vilivyosagwa
korosho iliyo kaangwa usizisage zibaki nzima robo kikombe
Kuna aina mbalimbali za upishi wa biriani ambapo mara nyingi hutofautiana kutokana na viungo vinavyotumika katika upishi.
Mahitaji ya kupika birian
1 kilo mchele wa basmati
1 kilo nyama iwe ya kuku au ng'ombe au mbuzi kata katika umbo dogo la kutosha kula kisha ichemshe na tangawizi na kitunguu swaumu, unga wa binzari (turmeric powder) pili pili manga na chumvi ili kuweka ladha nzuri. Ikisha iva itoe iweke pembeni na mchuzi wake uweke pembeni utautumia baadae.
1 kilo ya vitunguu kata slice ( mviringo)
1 kilo nyanya nyekudu zilizoiva, osha vizuri kisha katakata saizi ndogo ndogo sana
1/2 lita ya mafuta ya kupikia
1/2 kilo ya samli au mafuta yeyote ya kupikia
2 maggi chicken soup cubes
3 kijiko kidogo cha chai unga wa pilipili mwekundu
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa binzari
3 kijiko kidogo cha chai unga wa girigilani (giligilani)
2 kijiko kikubwa cha chakula mchanganyiko wa tangawizi na kitunguu swaumu vilivyosagwa
Weka mafuta katika sufuria yako iliyo juu ya moto tayari, kisha kaanga nyama yako iliyokwisha chemshwa mpaka iwe na rangi ya kahawia (golden brown)
Kisha itoe nyama hiyo na ichuje mafuta ili mafuta yanayobaki weka kitunguu na endelea kukaanga kwa dakika 7-10 kisha weka unga wa binzali, unga wa pili pili mwekundu, unga wa girigilani, mbegu za hiriki na nusu ya mbegu za pili pili manga.
Changanya vizuri mpaka utapata mchanganyiko mzuri mkavu miminia humo maji uliyotunza baada ya kuchemshia ile nyama yako na kuiweka pembeni ipoe. kisha weka nyanya fresh ndani ya sufuria yako pika mpaka maji yakauke na mafuta yaanze kuoneka kwa juu ndani ya sufuria.
Kisha weka nyama yako ndani ya sufuria pole pole halafu punguza moto acha ijipike kwa muda mpaka mchuzi wako na nyama vikamate ladha pia usisahau kuweka chumvi kulingana na ladha unayopenda.
Chukua sufuria nyingine weka mafuta ya samli na vitunguu ilivyoslice kisha kaanga na majani ya girigilani, korosho funika kwa dakika 10 i, kisha weka mchele wako mkavu uliokwisha oshwa vizuri na uchanganye vizuri ongeza vikombe 5 vya maji na chumvi kidogo mchele ukishaanza kuchemka funika sufuria lako na punguza moto maji yakisha kauka kiasi weka mchanganyiko wa ile nyama yako nusu tu juu ya wali wa basmati acha wali uive kabisa kisha itakua tayari kula na pakua chakula chako kikiwa cha moto
Changanya mtindi na tangawizi pamoja na kitunguu swaumu viache vikae kwa muda wa saa moja
Chukua sufuria weka mafuta na kisha kaanga vitunguu maji, weka nyanya, chumvi, kotimili na limao halafu weka karafuu na kanga hadi vichanganyike vizuri
Miminia mchanganyiko wa mtindi na baadaye weka pilipili na baadaye weka unga wa dhania
Chukua mchele uliochemshwa changanya na mchanganyiko huo
Palia moto juu ya chakula chako na acha kwa muda wa dakika 30
Baada ya hapo chakula chako cha biriani kitakuwa tayari kwa kuliwa
Jinsi ya kupika Biryani ya nyama ya kuku
Mahitaji ya kupika Biryani ya nyama ya kuku
Vikombe 2 mchele wa basmati
½ kijiko cha chai mbegu za jira (cumin seeds)
Star anise 1
¾ kijiko cha chai chumvi
Kilo 1 nyama ya kuku
Kijiko 1 cha chakula tangawizi
Kijiko 1 cha chakula kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chakula chicken bouillon powder
½ limao
¼ kikombe mafuta ya mzaituni (olive oil)
Vijiko 2 vya chai tangawizi
Vijiko 2 vya chai kitunguu saumu
Kitunguu maji 1 kikubwa Vijiko 3 vya chakula mafuta ya samli/ mafuta ya kupikia
Pilipili kichaa 2
Nyanya 3 kubwa
½ kilo viazi ulaya
½ kikombe mtindi
½ kijiko cha chai pilipili ya kukausha (chili pepper flakes)
Vijiko 2 vya chai garam masala
Kipande cha mdalasini
Bay leaf 2
Punje 4 karafuu
Punje 4 iliki
½ kijiko cha chai mbegu za jira
Kijiko 1 cha chai unga wa giligilani
Kijiko 1 cha chai binzari ya manjano
Chumvi kwa kuonja.
Maandalizi ya Biryani ya kuku
Kumarinate nyama yako ya kuku
Toa ngozi na kuchanja nyama; Andaa viungo vya kuku; twanga kitunguu saumu na tangawizi; kamua maji ya limao
Kwenye bakuli kubwa, changanya vizuri kuku na viungo vyote vya kuku
Funika bakuli au weka nyama kwenye mfuko. Acha viungo vikolee kwa masaa 4 au inapendeza zaidi akikaa usiku kucha
Ukiwa tayari kupika, andaa mchele kwa kuuosha hadi maji yawe masafi kabisa. Loweka kwenye maji kwa muda wa dakika 30
Ukiloana, chuja maji weka pembeni
Andaa viungo vya sosi/ gravy; katakata pilipili vipande vidogovidogo vya mraba; katakata viazi ukubwa utakaopenda; twanga kitunguu saumu na tangawizi, weka pembeni
Weka nyanya na kitunguu maji kwa ajili ya sosi kwenye mashine ya kusagia chakula kutengeneza rojo, weka pembeni
Andaa viungo kwa ajili ya juu/ garnish; Katakata kitunguu maji vipande virefu; katakata na majani ya giligilani na majani ya mnanaa, weka pembeni
Loweka zafarani chache kwenye ¼ kikombe cha maji ya uvuguvugu. Weka pembeni
maandalizi ya nyama ya kuku
Washa oven katika joto la 150 degrees C. Kwenye sufuria katika moto wa juu kiasi, chemsha vikombe 4 vya maji. Ongeza mchele, mbegu za jira, star anise na chumvi. Pika mpaka wali ukaribie kuiva
Ipua, chuja maji. Weka pembeni
Kwenye kikaangio katika moto wa wastani kaanga kitunguu kwa ajili ya kuweka juu (garnish) mpaka kiwe na rangi ya kahawia ila kisiungue
Toa kitunguu kwenye mafuta, hamishia vitunguu kwenye sahani iliyotandazwa tissues za jikoni au chujio la bati ili mafuta yachuje. Weka pembeni kwa ajili ya kuweka juu ya biryani badae
Ukitoa kitunguu, weka viazi kwenye mafuta. Kaanga mpaka viive vizuri, ipua weka pembeni
Kwenye sufuria katika moto wa chini kiasi, weka mafuta ya kupikia au samli. Yakichemka ongeza kitunguu saumu, tangawizi na pilipili kichaa. Pika paka viive na harufu ya ubichi iishe, kama dakika 2
Ongeza kuku na viungo vizimavizima; mdalasini, mbegu za jira, karafuu na iliki. Kaanga kwa dakika 5, ukigeuza mara chache isishike chine
Ongeza rojo ya nyanya, majani la bay na viungo vikavu vilivyoandaliwa kwa ajili ya sosi; giligilani ya unga, pilipili ya kukausha, manjano na garam masala. Acha ipike mpaka nyanya ziive vizuri
Ongeza mtindi, koroga vizuri, ongeza na chumvi ikibidi
Funika sufuria, acha nyama iive taratibu kwenye moto wa chini kwa dakika kama 10, ukigeuza inapobidi; au mpaka sosi iwe nzito, ibakie kama kikombe 1 cha kuivisha wali
kupangilia biryani
Ongeza viazi changanya vizuri na sosi. Katika chombo cha kuokea au sufuria nyingine kubwa zaidi sambaza nyama chini ya sufuria
Sambaza wali juu ya nyama. Ongeza na majani ya giligilani, majani ya mnanaa yaliyakatwakatwa kwa ajili ya kuweka juu pamoja na kitunguu cha kukaanga. Nyunyizia kwa juu maji yenye zafarani
Funika na foil, acha wali uive kwenye oven iliyopata moto kwa dakika 20 hadi 30; au mpaka wali uive vizuri. (unaweza pia kupalilia kwa mkaa, au kuoka kwenye oven katika chombo chenye mfuniko)
Changanya vizuri
Tenga cha moto na kachumbari ya tango, nyanya na mtindi; au ya tango na mtindi
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser. The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.