Tambi za Sausage na Karoti
Mahitaji ya kupika Tambi za Sausage na Karoti
- Tambi
- Sausage
- Karoti kubwa 1
- Chumvi
- Mafuta
Jinsi ya kupika Tambi za Sausage na Karoti
- Bandika sufuria jikoni na maji kiasi na uweke chumvi kiasi.
- Kata kata sausage zako vipande vidogo vidogo.
- Kwangua karoti kisha katakata vipande vidogo vidogo vya nusu duara.
- Maji yakichemka weka mafuta kisha weka tambi na funikia zichemke.
- Zikianza kuiva weka sausage na karoti, acha viive pamoja.
- Epua, chuja maji na andaa mezani tayari kwa kuliwa.
Enjoy!