Notification texts go here Contact Us Buy Now!

Noti Bandia | SEHEMU YA 07

Ofisi zetu ziko ghorofa ya juu katika jengo la Benjamin Wiliam Mkapa. Baada ya kuegesha gari kwenye maegesho ya Hotel JB Belmont, nilikwea ngazi mbili tatu nikaitafuta lifti iliyonipeleka juu kabisa. Shambulizi la usiku lilinifanya niliweka ulinzi wa kutosha kuzunguka eneo la ofisi zetu. Kazi yangu ya kwanza niliyofanya usiku baada ya kutuliza akili yangu ni kuwasiliana na Sajenti Julius Nyawaminza, huyu ni Komandoo aliyebobea, akilitumikia jeshi katika vikosi vya Zanzibar. Nilimwagiza kufika haraka Dar es Salaam, kwa vile Unguja ni karibu alifika Jijini asubuhi na kujiweka kwenye pointi niliyompangia awe. Kwa kuwa vijana wetu wa Dar es Salaam wanafahamika kwa kiasi fulani, nilipanga kuwatumia kwa kazi zingine, hivyo niliwasiliana pia na Luteni, Claud Mwita kutoka vikosi vya Komandoo mkoani Morogoro, ambaye pia aliweza kufika kwa wakati, akafanya kile alichoelekezwa kufanya.





Ofisi zetu ziko ghorofa ya juu katika jengo la Benjamin Wiliam Mkapa. Baada ya kuegesha gari kwenye maegesho ya Hotel JB Belmont, nilikwea ngazi mbili tatu nikaitafuta lifti iliyonipeleka juu kabisa. Shambulizi la usiku lilinifanya niliweka ulinzi wa kutosha kuzunguka eneo la ofisi zetu. 

Kazi yangu ya kwanza niliyofanya usiku baada ya kutuliza akili yangu ni kuwasiliana na Sajenti Julius Nyawaminza, huyu ni Komandoo aliyebobea, akilitumikia jeshi katika vikosi vya Zanzibar. Nilimwagiza kufika haraka Dar es Salaam, kwa vile Unguja ni karibu alifika Jijini asubuhi na kujiweka kwenye pointi niliyompangia awe.



Kwa kuwa vijana wetu wa Dar es Salaam wanafahamika kwa kiasi fulani, nilipanga kuwatumia kwa kazi zingine, hivyo niliwasiliana pia na Luteni, Claud Mwita kutoka vikosi vya Komandoo mkoani Morogoro, ambaye pia aliweza kufika kwa wakati, akafanya kile alichoelekezwa kufanya.

Nilichelewa kwa dakika kadhaa kufika ofisini kwa Kanali Emilly kama ambavyo tulikuwa tumeafikiana, kuchelewa kwangu kulitokana na mipango ya hapa na pale, maana mtu akikuanza utani lazima ujiandae kutaniana naye, lakini pia akikuanza uchokozi muonyeshe kuwa amepita njia mbaya.

Mapokezi nilipokelewa na Linnah David, Katibu Muhtasi wa Kanali Emilly, "Ulikuwa wapi Teacher? Mzee anakusubiri kwa shauku kubwa, amesema ukitia pua tu, usisimame, moja kwa moja ingia ofisini kwake", Linnah alitania.

"Vipi hali yako Linnah, sikukuacha ofisini, nilisikia wewe pia umepata likizo kulikoni? Au ndiyo umeitwa haraka kama mimi?", nilimuuliza akatabasamu.

"Nitakwambia ukitoka kwa bosi", alisema Linnah huku akinihimiza kuingia ndani ya ofisi ya Kanali Emilly.

Mapigo ya moyo wangu yalianza kunienda mbio, sikujua kilichotokea hata nikaitwa haraka kiasi hiki, taratibu niligonga mlango wa ofisi ya bosi, baada ya kusubiri kwa sekunde kadhaa nilitasua kitasa cha mlango na kuingia ndani. Kanali Emilly aliponiona haraka alisimama na kunielekeza sehemu ya kuketi. Nilishangazwa na hatua hii, kunielekeza mahali pa kukaa karibu kabisa na yeye tofauti kabisa na kawaida yake.


Kanali Emilly alikuwa mzee wa makamo, lakini mwenye busara na nguvu nyingi, hakuwa mwepesi wa kushindwa jambo. Baada ya kupeana mikono na mimi kuketi mahali aliponielekeza, aliinua simu yake ya mezani akamwagiza Linnah atuletee vinywaji. Kabla ya kukata simu, Kanali Emilly alimtaka Linnah kuongeza vinywaji kwa ajili ya wageni wanaokuja. Mimi nikabaki kimya.

"Karibu sana Teacher, pole kwa kukatisha likizo yako fupi, nimekuita kwa sababu kuna tatizo limetusibu, tutakuwa na wageni hapa ofisini muda si mrefu, wanakuja kuongea na sisi, tutawasikiliza, tutashauriana nini cha kufanya", alisema Kanali Emilly, aliinua tena simu yake ya mezani akaongea na watu ambao mimi sikuwajua, akawajulisha kuwa mimi nimefika hivyo waje ofisini kwake. 

"Kuna tatizo gani bosi, maana sielewi kinachoendelea?" nilimuuliza Kanali Emilly.

"Kuna tatizo kidogo limetoke. Nikaitwa haraka nyumba kubwa, kutakiwa kurudi kwako haraka ni agizo la Rais. Wakati tunawasubiri hawa ndugu zetu, nitakudokeza kidogo kilichotokea", alifungua droo ya meza yake, akatoa bahasha kubwa iliyojaa mapesa, pia akatoa kiboksi kilichojaa makaratasi yaliyoandaliwa kama pesa, akanipatia.

"Hizi ni pesa zangu?", nilimuuliza Kanali Emilly akache

"Ziangalie kwanza Teacher, halafu nitakueleza sababu".

Zilikuwa pesa nyingi zinazotumika katika mataifa mbalimbali duniani. Zilikuwepo noti za shilingi elfu kumi za kitanzania, nilizipitia noti hizi moja baada ya nyingine, sikuona tofauti. Niliendelea kuziangalia noti hizi kwa umakini mkubwa, zilikuwepo noti za Saandaang Piso zinazotumika Jamhuri ya watu wa Philipines, Diez ya Uruguay, Paundi ya Misri, Birr ya Ethiopia, Yen ya Japan na Won ya Korea Kusini.

Niliendelea kuzipitia pesa hizi kwa umakini sana, Kanali Emilly alikaa kimya akiniangalia, sikufahamu lengo la mzee huyu kunipatia pesa hizi niziangalie tu. Niliendelea na zoezi la kuzikagua noti hizi, Rupiah ya Indonesia, Rupee ya Pakistan, Rand ya South Afrika, Afghan ya Afghanistan, Rouble ya Belerus na Peso ya Cuba. 

Kulikuwa na idadi kubwa ya noti, ni vizuri nikutajie aina zote za noti zilizoko mbele yetu ili uweze kunielewa vizuri, kabla mzee hajasema jambo. 

Aina nyingine ya pesa sikuwahi kuziona kabisa, kama Rouble ya Russia, Litu ya Luthuania, shilingi ya Kenya, Franc ya Afrika ya Kati, Real ya Brazil, Drams ya Armenia, Lira ya Uturuki, Krone ya Denmark na Riyal ya Saudi Arabia. Zingine ni Paund ya Sudan, Lei ya Romani, Dong ya Vietnam, Dollah ya New Zealand, Peso ya Argentina, Dinar ya Libya, Hryvmy ya Ukraine, Sum ya Uzbekistan, Kwacha ya Zambia, Franc ya Kongo, Franc ya Chad, Dinar ya Algeria, Rouble ya India, Franc ya Cameroun, Mark ya Ujeruman na Dollar ya Marekani.

Baada ya kuzipitia pesa hizi, nikazirejesha mikononi mwa Kanali Emilly, ambaye alizijaza kwenye bahasha kubwa, akaniangalia kwa sekunde mbili tatu, alipoona nimekaa kimya nikimwangalia akatoa bahasha nyingine iliyojazwa makaratasi yaliyokatwa kwa mpangilio mzuri mfano wa pesa. Karatasi hizi zilifungwa kwa mafungu sawa na noti, zikitofautiana kwa ukubwa wa aina ya pesa husika.

Niliendelea kuumiza kichwa changu, nilijiuliza sababu ya Kanali Emilly kuleta pesa hizi mbele yangu, kilichoanza kunizindua ni haya makaratasi yaliyokatwa mfano wa pesa, mawazo yangu hayakunipeleka mbali, nikahisi kuwa huenda karatasi hizi zimekamatwa kwa matapeli waliotapakaa kila kono ya miji ya Afrika Mashariki na duniani, wakiwaibia watu kila siku.

"Naam kamanda wangu, nifahamishe sasa. Kuna habari gani mkuu?", nilimuuliza baada ya kumaliza kazi ya kuzipitia karatasi alizokuwa amenipatia. "Hizi noti na karatasi nahisi zimekamatwa kwa matapeli", niliongeza.

"Afadhali tungekuwa tumewakamata, Teacher hili ni tukio linalotia huruma sana, huwezi kuamini nikikueleza kile kilichofanyika, watu wameuza majumba, magari na wengine wamefirisika kabisa kutokana na pesa na karatasi hizi ulizoziona", Kanali Emilly alieleza.

"Ehee?", nilihoji huku nikikiweka tayari kumsikiliza. Mara simu ikaita, akainua mkonga wa simu na kuiweka katika sikio lake la kushoto, baada ya muda alisema, "Waruhusu wapite tafadhali", akaweka simu chini.

"Teacher, kabla sijakueleza hali halisi ya tukio hili, bahati nzuri wahusika wamefika, utawasikiliza kwa makini, wataeleza kilichowasibu, sidhani kama tutashindwa kuwasaidia katika hili", alisema Kanali Emilly.

"Itategemea na kazi yenyewe bosi, kama ujuavyo hii ni dunia, hata uwe mjuzi wa kuogelea kiasi gani, iko siku maji yatakuzidi ujanja, unaweza kuingia mpaka kimo fulani ukashindwa kuendelea, lolote laweza kutokea", nilimwambia. Sikuona vizuri kumsimulia kuhusu tukio la usiku, hivyo nilimezea. 

Mlango wa ofisi uligongwa, Linnah akaingia akifuatiwa na watu wawili waliotakata vizuri, ukiwaangalia huhitaji kuuliza, moja kwa moja niliamini kuwa watu hawa ni vigogo kutoka serikalini ama matajiri wenye mapesa yao.

ITAENDELEA

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.