Notification texts go here Contact Us Buy Now!

ZIFAHAMU SHERIA ZAKO ZA MSINGI UKIKUTANA POLISI USINYANYASWE FANYA HAYA UWAPO MIKONONI MWA POLISI

Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako. 2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako. 3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.

1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.
2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.
3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.
4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.
5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.
6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.
7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.
9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.
10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.
12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.
13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.
14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.
15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.
16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.
17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.
19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.
20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.
21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.
22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.
SHARE KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ILI WAZIFAHAMU HAKI ZAO.






Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.