Mwongozo wa Walimu wa Kujitolea umeandaliwa ili kutoa maelekezo ya namna ya kupata walimu wenye sifa stahiki na kuwaajiri kwa mkataba wa kujitolea, kutoa taratibu za mafunzo kabilishi, kupanga na kutoa maelekezo ya kutosha kitaaluma na kitaalamu ili kazi zifanyike kwa ufanisi. Aidha, Mwongozo huu unalenga kutoa maelekezo ya upatikanaji wa walimu wanaojitolea na huduma zao ikiwemo: posho, motisha na usimamizi wa nidhamu pahala pa kazi kwa kuzingatia masharti ya ajira za mkataba
Inatarajiwa kuwa matumizi ya Mwongozo huu yataimarisha ushirikiano wa wadau wa elimu hususani Uongozi wa Elimu, jamii, walimu na wazazi. Pia Mwongozo utawezesha walimu wanaojitolea kutoa huduma stahiki za ujifunzaji na ufundishaji kwa kuzingatia matakwa ya elimu nchini. Hii itasaidia kutatua changamoto za ujifunzaji na ufundishaji na kuleta matokeo chanya yaliyokusudiwa katika elimu ya awali, elimu ya msingi, elimu ya sekondari na vyuo vya maendeleo ya wananchi Tanzania.