MAHITAJI YA JUICE YA NANASI NA EMBE
- Nanasi Kikombe 1
- Embe Kikombe 1
- Sukari vijiko 5
- Arki Vanilla kiduchu
- Maji ya baridi Vikombe 3
JINSI YA KUTENGENEZA JUICE YA NANASI NA EMBE
- Weka Nanasi kwenye jagi la blenda na maji nusu kikombe
- Saga mpaka ilainike kiasi mara 3
- Mimina kwenye chombo chako
- Mimina Embe na maji Vikombe 2 kwenye jagi
- Weka sukari na arki
- Saga mpaka ilainike
- Mimina kwenye chombo chako
- Mimina maji yalobakia kwenye jagi kumalizia Juice iloganda kisha mimina kwenye chombo chako
- Koroga vizuri kisha weka kwenye friji ipate baridi vizuri
- Tayari kwa kunywa
Angalizo :
- Sijaichuja juice nimesaga vizuri tu kupata juice fresh
- Nimetumia Kikombe kidogo cha chai```