USO WA FEDHA | FACE FO MONEY.
USO WA FEDHA # 16 [SWAHILI].
MTUNZI : Sunday JoaquimContact : 0658 593 797
Chosta alikuwa akiishi maeneo ya kimara Korogwe,pale mtaani kwake alijitangaza kuwa yeye yupo kitego nyeti cha serikali ili majirani wasimtilie shaka,kumbe alikuwa ameshajuana na wakubwa wengine na ana mkono kwenye kila kundi la ujambazi na ujangili,ilikuwa ngumu kuamini mpaka jamaa yangu wa karibu Khamisi aliponihakikishia kwa kunitajia majina ya vijana vinara anaowatumia Chosta kupata taarifa na katika kufanikisha ujambazi wake "sikiliza Uso wa Fedha usihangaike na hlo jambazi sugu itakupoteza lina vijana wengi sana hapa mjini isije ukapanga mipango ukajiona upo salama kumbe unapanga mipango na vijana wake wakakuuza" aliongea Khamisi kwa msisitizo sana hapo niliishiwa pozi,niliona kuna haja ya kufikiria kwanza kabla ya kuendekeza hasira,nilimuuliza Khamisi "sasa unanishauri nifanye nini?" "fanya hivi wewe andika orodha ya vijana unataka kuwatumia kwenye kazi alafu mimi kesho nitakuja na orodha yangu alafu tutalinganisha" nilikubaliana naye tukafunga mjadala kwa siku hiyo.
Kesho mapema kabla sijatoka nyumbani Khamisi alifika "oya unalala mpaka saa hizi una hela sana eeh?" aliniluliza huku akicheka "ah wapi nilichoka tu jana" "lazima uchoke una msichana wa kazi mzuri namna hii hata ningekuwa mimi ningechoka mara mbili yako" "ah tuheshimiane bwana mimi na mfanyakazi wapi na wapi?" "wewe unaaminika kama umeweza kumuoza mkeo kwa kujidai baba mdogo utaaminika kwa kifaa kama hiki?" "weeeh acha upuuzi wako haya lete hiyo orodha yako nione" Khamisi alitoa karatasi kwenye mfuko wa shati iliyokunjwa akanikabidhi,dooh kuisoma majina yote nayajuwa na baadhi yao nilishawaita waje tuongee niwape mkakati wa kazi "aseeeh umeniokoa rafiki yangu duh ! hawa wote wamo kwenye orodha yangu,nilikuwa naingia kwenye mdomo wa Mamba "eeh unajuwa hawa jamaa wote nipo nao karibu sana huwa nawkodisha vitendea kazi ndiyo maana najuwa mambo mengi sana kuhusu wao".
Nilikuwa nimeketi kwenye sofa lakini nilihisi linawaka moto kwasababu nilipanga ili kulipa kisasi vizuri lazima na mimi mwenyewe nishiriki kikamilifu,nilimshukuru sana Khamisi,niliamua kuanzisha kundi jipya la ujambazi kwani kipindi hicho pesa ilishaanza kupungua niliona nitaaibika mjini wakati Uso wa Fedha jina kubwa,nilitafuta vijana nane toka mikoa ya kusini wawili kati yao walikuwa wanachama wa kundi la zamani lililosumbua sana Mtwara lililojulikana kama TUKALE WAPI?,hao walikuwa balaa,niliona kazi yangu itakuwa rahisi sana,niliwapa mafunzo ya silaha kwenye mstu wa Nyuki siku hizi panajulikana kama Malamba Mawili,vijana waliiva vizuri,nikatafuta kazi ya kwanza ili nione wataifanya kwa mafanikio kiasi gani,ilikuwa nikuteka fedha zilizokuwa zinapelekwa Singida,wakati huo ulitumika usafiri wa gari kusafirisha fedha,ilikuwa ni kazi ngumu sana lakini vijana waliipiga klkazi muda mfupi kuliko nilivyotarajia na walitoweka bila kuacha ushahidi.
Nilipiga matukio mfululizo bila huruma,hali yangu ya kifedha iliimarika sana,nilizungushia ukuta nyumba yangu nikaweka geti na walinzi,nilinunua simu ya mkononi ya kwanza ilikuwa kubwa kama mchwe wa sabauni,wakati huo walikuwa nazo matajiri wachache sana,nilijiona na mimi nipo kwenye ulimwengu wa kisasa,simu ya mkononi ilikuwa anasa,baada ya muda nilinua simu nyingine mbili ili kurahisisha mawasiliano kati yangu na vijana wangu, Jumanne alikuwa ndiye mkuu wa kundi langu jipya al maarufu J4,mimi nilikuwa natafuta kazi,natoa maelekezo,fedha na kukodi vitendea kazi,vijana walikuwa na njaa sana pia walikuwa na hasira ya maisha,walipiga kazi za kushangaza kiasi makundi mengine ya majambazi walikuwa wakiulizana hao ni kina nani? wametokea wapi? wengine walidai ni watu toka nchi jirani wengine walisema ni watu wa serikali,lakini Chosta alipeleleza mpaka alijuwa kuwa mimi nahusika na hao vijana.
Bila kutegemea nilikuwa nikipata chakula cha mchana nyumbani simu iliita,namba siijui,nilipokea "hallo" huku nikisikilizia sauti "haaa haaaa haaaa we jaama yangu kiboko sana yaani unapiga matukio kimya kimya mpaka serkali inajiuliza" nilisikiliza sauti vizuri ilikuwa sauti kama ya Chosta,nilikata simu sikutaka bugudha,simu iliita tena "sasa jama yangu unakata simu unajuwa unaongea na nani?" "sijui lakini ustaarabu ungejitambulisha kwanza" "anhaa sawa Bosi unaongea na Chosta hapa" "okay niambie unataka nikusaidie nini" "we usijitoe fahamu hizo kazi unazo piga ni gumzo hapa mjini nataka tukutane tuongee haiwezekani neema ule peke yako" "daah mbona unanifuatilia sana au unaniona bwege umenitesa na sijafanya chochote? achana na mimi kabisa kila mtu afe kivyake" "sawa pesa si imekupa kiburi tutaona kama hizo kazi kama utapiga tena" "poa tuone basi kwani wewe nani usinitishe kabisha nyau wewe" tulijibisha na kibabe,nilikaa nikafikiria jinsi ya kujilinda.
Niliona dawa ni kuongeza vijana,niliongeza mpaka walifika thelathini na mbili,kumi kati yao walikuwa vizuri kwenye michezo ya mapigano yaani karate,nilijiona nimeshakuwa mbabe sana mjini,sikuwa nikiogopa kitu wala mtu yeyote,pesa zilichanganya,nikawa najipanga jinsi ya kuanzisha biashara kwa ajili ya kuwazuga walimwengu,maana wakijuwa unafanya ujambazi wao wenyewe watageuka mahakimu,nilifanikiwa kuanzisha Baa nikaipa jina THE HOOD maeneo ya Mgomeni Morocco,japokuwa wabongo wenzangu waliitamka ZE HUD lakini ilipata umaarufu mkubwa hasa kwa mishkaki na nyama choma nzuri,vijana wachoma nyama niliwatoa Arusha,wateja walifurika mpaka watu waliamini nina mganga anaye sababisha wateja wajae,ilikuwa ni rehema zake Mwenyezi Mungu tu,niliona ni wakati wa kuleta bendi ya muziki kutumbuiza ili kukonga nyoyo za wateja wangu.
Khamisi alinishauri niende Kongo wakati huo ikiitwa Zaire,nilijipanga kwenda Zaire,nilimwomba Khamisi twende wote,alikubali,tatizo lilikuwa Baa yangu namwachia nani nikiondoka? hapo nilikuwa mpole,niliumiza kichwa bila majibu,nilijipa siku mbili za kufikiria,niliporudi nyumbani ilikuwa saa saba za usiku,mlinzi alinifungulia geti nikaingiza gari,wakati nashuka nikamwona mtu amesimama pembeni yangu,nilishtuka sana,nilishangaa walinzi mbona wamemruhusu mtu bila kuniambia,kwasababu ya mwanga hafifu,nilijitahidi kumwangalia vizuri bila kumtambua,nilimwangalia tena khaa ndipo nilimtambua,nilihisi mapigo ya moyo yalitaka kusimama............ENDELEA NA KUSOMA SEHEMU YA 17 YA SIMULIZI YA USO WA FEDHA.
FACE OF MONEY #16 [ENGLISH VERSION].
Chosta was living at kimara areas, at his neighborhood he declared himself that he is a sensitive government selector so that the neighbors could not doubt him, so he had already known him with other elders and has a hand in every group of violence and lies, it was hard to believe until my close guy is close. When he assured me by calling me the names of the young people who send them to get information and in achieving his share "listen to the face of money do not struggle with the chronic thug it will lose you it has a lot of young people here in the city lest you plan plans and see you are safe but you are planning to sell it" A lot of emphasis there I was moved to pose, I saw there was a need to think first before proposed anger, I asked him all " now what do you advise me to do?" " do this you write a list of young people you want to send them on work and then I will come with my list and then we will compare it " I agreed And on that day we shut up the debate on that day.Tomorrow early before I came out of home, all arrived " hey you are sleeping until now you have a lot of money huh?" he asked me while laughing " ah where did I just get tired yesterday " " you have to be tired you have a girl of such a good job even if I was me I would be tired twice " ah Let's respect each other Lord me and employee where and where?" " you are believed if you have been able to marry your wife by bragging a young father you will be trusted on such device?" " eeh stop your nonsense bring that list of yours to see " all gave paper in a shirt that has been covered He handed me, I know to read all the names I know and some of them I called to come talk and give you a strategy of work " oh you saved me my friend duh! All of these are on my list, I used to enter the crocodile's mouth "oh you know all these guys I am with them very close I always hire them that's why I know so many things about them".
I was sitting on the sofa but I felt it hot because I planned to pay well revenge I must and myself fully participate, I really appreciated the all, I decided to start a new group of distributors since that time the money started to decrease I saw that I will be ashamed in the city when the face of a big money, I looked for me. From the southern regions two of them were members of the old group that really disturbing mtwara which was known as where we eat?, those were trouble, I saw my work would be very easy, I gave them a weapon training on the bee of bees nowadays known as two malamba, young men. They cooked well, I looked for the first job to see how successful they will do, it was to take the money that was taken to singida, at that time used car transport to transport money, it was a very difficult job but the young people worked less than I expected and disappeared without evidence.
I took events series without mercy, my financial situation was so high, I surrounded the wall my house and I put a gate with the guards, I bought the first mobile phone was as great as a of ant, at that time they had very few rich people, I saw myself and I am in the world of the world Modern, mobile phone was luxury, after a while I killed another two phones to simplify communication between me and my youth, Tuesday was the chief of my new group al famous j4, I was looking for a job, I'm giving instructions, finance and rent jobs, Young people were so hungry they were also angry in life, they worked some shocking jobs some other groups were asking each other? Where have they come from? Some claimed it's people from neighbouring countries some said they are people of the government, but chosta alipeleleza until he knew that I am concerned with those young people.
Without depending i was getting lunch at home, the phone called, the number I don't know, I received " hallo " while listening to the voice " haaa haaaa haaaa you my jaama is very whip I mean you are making the events quiet until the government asks himself " I listened to the voice well it was like the chosta, I gave the phone I didn't want to go back, the phone called again " now my people you are cutting your phone and you know who you are talking to?" " I don't know but civilization yourself first?" " Okay, boss you are talking to me " " okay tell me what you want me to help you " you don't know what you are doing. It is a chat here in the city I want to meet and talk, it is impossible for the grace alone " " Daah why are you following me so much or you see me a fool you have tortured me and I haven't done anything? Leave me completely, everyone should die his own. " ok money is not given you pride. We will see if those work if you will beat again " " good let's see then who don't scare me at the kitten you " we held up with a babe, I stayed and thought how to protect yourself.
I saw medicine was adding young people, I added until they reached thirty-two, ten of them were good in fighting games I mean in Karachi, I thought I had become very arrogant in the city, I was not afraid of anything nor anyone, money mixed, I became planning how to start a business for To deceive the world, because when they know you are doing their own business they will turn into judges, I succeeded to start a bar and gave it to the hood in Morocco, although my fellow tanzanians woke up ze hud but it got a great popularity especially with roasted meat and meat, the young people who fed up in Arusha, the customers were flooded. Until people believed I have a healer who causes customers to come, it was only God's mercy, I saw it was time to bring a musical band to perform the hearts of my customers.
All advised me to go to Congo at that time called Zaire, I planned to go to zaire, I asked him for all let's go all, he agreed, the problem was my bar whom I leave? When I was humble, I hurt my head without answers, I gave myself two days to think, when I came home it was seven hours of night, the guard opened me the gate and entered the car, when I went down and saw someone standing next to me, I was shocked, I wondered why the guards had allowed anyone to tell me, because of Light Light, I tried to look at him well without realizing him, I looked at him again and then I knew him, I felt the heart of the heart wanted to stand............CONTINUE TO READ PART 17 OF FACE OF MONEY.