Notification texts go here Contact Us Buy Now!

KIFUA KUUMA NI DALILI YA MAGONJWA MENGI SANA

“CHONDE CHONDE USIDHARAU MAUMIVU YA KIFUA (CHEST PAIN)” HASA UKIHISI KAMA KINAWAKA MOTO , KUNA KITU KINACHOMA AU MGANDAMIZO CHINI YA ZIWA KISHOTO”
  •  Kifua kuuma ni dalili ya magonjwa mengi Sana , zaidi ya magonjwa 100 huweza kusababisha kifua kuuma.
  •  Lakini pia ni dalili ambayo haitakiwi kupuuzwa au kuchukuliwa kirahisi kwani inaweza kuwa dalili ya magonjwa hatari na yanayoweza kusababisha kupoteza maisha haraka – kama magonjwa ya moyo (heart attack) au ya mapafu (pulmonary embolism).
  •  Kutokana na umuhimu wa dalili hii , napenda tuangalie mambo machache ya muhimu kufahamu kuhusu maumivu ya kifua.
  •  Mshituko wa moyo (Heart attack/ Angina Pectoris)
  •  Vijidudu kwenye moyo (infections) – (Pericarditis, myocarditis,endocarditis)
  •  Matatizo ya valve za moyo
  •  Magonjwa ya mshipa mkuu wa damu (aortic aneurysm, dissection)

Dalili:

  •  Kifua kuuma kama mzigo mzito umekandamiza moyo
  •  Au maumivu makali kama mshale umekaa kwenye moyo
  •  Maumivu husikika upande wa kushoto wa kifua, sehemu ya katikati au yaweza kuwa popote kifuani
  •  Pia huweza kusikika kwenye bega, shingo, taya, mkono wa kushoto au hata kwenye meno (Radiating pain type).
  •  Kifua huwa kizito, na kujisikia kukosa hewa
  •  Moyo kuenda mbio
  •  Kutoka jasho jingi, kizunguzungu, kutapika au kwikwi isiyokatika
  •  Pia dalili nyingine huweza kujitokeza kama – kupoteza fahamu, tumbo kuuma n.k.
  •  Maumivu huzidishwa na mishughuliko (activities/exertion) au msongo wa mawazo(stress). Kutulia au kupumzika (rest/relax) huleta nafuu au kuondoa maumivu.
  •  Homa hutokana na kuwepo kwa vijidudu (infection) kwenye moyo au damu.
  • MUHUMU: Ukipata dalili moja au zaidi kama zilizotajwa hapo juu, au maumivu ya kifua yasiyoisha zaidi ya dakika tano au yasiyotulia hata baada ya kupumzika au kutumia dawa za maumivu , tafadhali wahi hosipitali! Inapowezekana tafuta huduma ya matibabu ya haraka ya wagonjwa waliozidiwa (emergency care).
  •  Damu kuvilia kwenye mishipa ya damu ya mapafu (pulmonary embolism)
  •  Vijidudu kwenye mapafu – husababisha homa ya vichomi (Pneumonia, Bronchitis, Tuberculosis/TB,) n.k.
  •  Kujaa maji, damu au hewa kwenye mfuko wa nje wa mapafu (pneumothorax, haemothorax or pleura effusion)
  •  Saratani.
  •  Haya husababisha maumivu ya kifua aina ya vichomi Au maumivu makali wakati wa kupumua – kuvuta hewa.
  •  Maumivu huwa popote katika kifua, bila kusikika nje ya kifua kama kwenye bega au shingo (non radiating type)
  •  Husababisha shida katika kupumua, mtu kujisikia kukosa hewa na kuhema haraka haraka.
  •  Mara nyingine husababisha rangi ya midomo au mikono kubadilika kuwa blue(cyanosis).
  •  Homa au kutoka jasho sana hasa wakati wa usiku huashiria vijidudu – virusi, bacteria, TB nk.
  •  Mara nyingi huambatana na kikohozi – kikavu au chenye makohozi
  •  Kiungulia au Vidonda vya tumbo
  •  Michubuko au vijidudu kwenye njia ya chakula (oesophagitis)
  •  Magonjwa mengine ya njia ya chakula, tumbo, kongosho au hata ini.
  •  Husababisha maumivu ya kifua hasa sehemu ya chini, katikati ya matiti,
  •  Huweza kuwa kama moto, au maumivu tu makali katika eneo hilo
  •  Wakati mwingine husikika sehemu ya chini ya moyo upande wa kushoto
  •  Usambaaji wake(radiation) huelekea upande wa bega la kulia au mgongoni
  •  Mara nyingi huwa na uhusiano na chakula – maumivu wakati wa kumeza, baada ya kula, wakati mtu ana njaa, baada ya kula aina fulani ya vyakula, au akibadilisha utaratibu wa chakula.
  •  Kama tatizo limeshakuwa kubwa huweza kusababisha maumivu makali hata bila kuhusiana na chakula.
  •  Moto wa mungu (Herpes zoster) kwenye eneo la kifua
  •  Magonjwa ya matiti
  •  Magonjwa ya mifupa au vishikizo vya uti wa mgongo
  •  Magonjwa ya mishipa ya fahamu ya kufua
  •  Michubuko, kuumia au kuvutika kwa misuli katika kifua
  •  Michubuko, vijidudu au kuumia mifupa, viungo(joints) au vishikizo vya viungo(tendons and ligaments) katika eneo la kifua
  •  Magonjwa mengine ya misuli na mifupa ya kifua
  •  Maumivu yanayosababishwa na magonjwa haya huweza kufana na maumivu yeyote yaliyotajwa hapo juu.
  •  Ni muhimu kujua historia au maelezo ya maumivu hayo kwa undani, kufanyiwa uchunguzi wa kina na vipimo pale vinapohitajika ili kujua tatizo.
  •  Magonjwa ya kisaikolojia au kuhema haraka karaka
  •  Sumu za aina fulani kama – lead, carbon monoxide
  •  Magonjwa ya Saratani

Magonjwa yanayosababisha maumivu ya kifua, hasa yatokanayo na moyo au mapafu huweza kusababisha kupoteza maisha haraka sana kama yasipotibiwa kwa wakati. Tafadhali wahi hospitali ili upatiwe tiba mapema na kuokoa maisha yako. Usipuuzie maumivu ya kifua; Ni afadhali kumsumbua daktari kwa kuwahi hospitali na kukuta hakuna tatizo, kuliko kuogopa kumsumbua daktari halafu ukachelewa hospitali na kupata madhara ambayo yangeweza kuzuilika, au kupoteza maisha.

Angalizo : Kama Wewe ni Muhanga wa Maumivu haya ya Kifua Yasiyokwisha na Huna TB na Umetumia Dawa Mbali Mbali hayataki Kusikia TUANDIKIE KWENYE comment box hapa chini


Maoni 2

  1. Mimi ninayo hayo maumivu ya kifua
    1. Kama Ukipata dalili moja au zaidi kama zilizotajwa hapo juu, au maumivu ya kifua yasiyoisha zaidi ya dakika tano au yasiyotulia hata baada ya kupumzika au kutumia dawa za maumivu , tafadhali wahi hosipitali haraka ama wasiliana na daktari wako au aliyekaribu nawe kwa wakati huo.
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.