JINSI YA KUPIKA VI 8 (MITAI)
mahitaji:-
unga ngano nusu
siagi vjk 3
nazi ya unga vjk 3
iliki kijiko kdg
hamira kijiko 1
yoghurt nusu kikombe
🌰kanda unga wako weka vitu vyote unaweza kukandia maziwa au maji. kama huna nazi ya unga kandia tui la nazi yakawaida mpaka unga ulainike.
🌰kata madonge kuasi au kata viringisha mnjongoo mrefu kata vipande zungusha kama namba nane.
🌰acha viumuke choma mpaka ziwe kama maandazi tu.
🌰weka sufuria maji kikombe kimoja,sukari kikombe kimoja, iliku nusu kjko ukipenda weka na vanilla kijiko 1. acha ichemke hadi iwe nzito kama ya visheti.
🌰sasa weka vi nane vyako anza kupeta vikolee ile sukari. vitakua tayari