NYAMA KAVU NA LAINI.
JINSI YA KUPIKA NYAMA KAVU
Nyama ya mafupa, nimechanganya na thom, tangawizi, pilipili manga, uzile, curry powder, ndimu, na jumbo powder, Mimi huwa situmii chumvi nikitia jumbo huwa inatosha. Nyama ilipowiva na kukauka nikatia kitunguu maji, pilipili boga na kotmiri, nikachanganya nikaepuwa.
Nyama hii nzuri sana hasa ukitia vitunguu maji vingi.