Notification texts go here Contact Us Buy Now!

UTAMU WA MAMDOGO SEHEMU YA 02

Mtunzi: Geofrey Mustafa, Artist Jafa.
Mahali: Ubungo Riverside, DSM
WhatsApp: 0713024247.
Instagram: @Jafa Love Story.

  Umri___+
        
"KISA NA MAJINA SIO KWELI NI STORY TU"

                  *(SEHEMU YA 02)*

*ILIPOISHIA==>*
Basi alikuwa ni Mama akiongea na Mdogo wake uyo Mamdogo Sakina, Mimi nikaabiwa na Baba nitafute vijana wa pikipiki ili waje kubeba uwele na ulezi Bamdogo alileta mwigi tu maana sisi wanyamwezi hatuwezi kuishi bila kula ugari wa uwele au asubuhi uji wa ulezi. Mama alijaribu kupanda ulezi  hapa Mbingu ila uligoma kutokana na maji kuwa mengi kwaiyo Baba alisema bora waagize tu nyumbani TABORA alafu msimu ujao tutaenda milimani huko Ilola tukajaribu kuchoma mabiwi alafu tumwage ulezi tunaamini utakubali tu.

Asubuhi saa kumi na mbili niliondoka zangu na baiskel aina kamongo mayai kuelekea shule, nilikuwa nasoma St. Merry  shule ya Masister hapa Londo iyo nikutokana na uwezo wangu kuwa mkubwa darasani kwaiyo Baba hakutaka nisome shule za yebo yebo, nilishukuru maana ni wazazi wachache sana wenye imani na watoto wao.....
*Artist Jafa*

                     __ENDELEA SASA__
Ilipofika saa tisa safari yakurudi nyumbani toka shule ikaanza maana Hostel za wavulana zilikuwa bado walikuwa wanakaa Hostel wasichana tu kutokana na usalama wao. Nilifika nyumbani saa kumi na nusu nilichelewa sana maana baiskel yangu ilipata pancha njiani nikatembea kwa miguu mpaka magenge makubwa nikaziba Ndio nikaendelea.
"Wee Juma mbona mji mpo kimya ivi.?"
Nilimuuliza Mdogo wangu baada yakuona Nyumba ipo kimya kabaki yeye tu.
"Mama na Mamdogo walienda kununua ndizi za kuchemsha asubuhi, ila Baba na bamdogo wameenda kutafuta Nyumba yakupanga huko nimebaki Mimi kulinda mji hapa.."
Basi nikala zangu msosi nikaanza kujisomea somea maana izi shule za mission sio mchezo ukivulunda tu kwenye mtihani unarudishwa nyumbani ukaanze primary upya, hawataki kabisa kukaa na wanafumzi mabongo lala.

"Ujambo"
"Sijambo Mama, shikamoo"
"Marhaba, tena bora nimekukuta... nenda kasaidie kuingiza ndizi ndani hapo nje"
Basi nikafunika kitabu nikaweka madaftari vizuri nikaenda zangu nje,  Ooh! Shiit nikamuona vizuri kabisa Mamdogo umbo lake kwa upande wa mgongoni, "Aisee yani bamdogo kapata mwanamke mzuri jamani mmh! Cheki kiuno chake..rudi makalio sasa ndio balaa utadhani kaweka vipande vya maboga kumbe makalio yake original kabisa daah! Kweli Mamdogo Sakina sio poa..!!"
Yalikuwa ni mawazo yangu kichwani Mara tu baada yakuona sura au wazungu wanasema view ya mgongoni.
"Shikamoo Mamdogo Sakina"
Akageuka shingo tu maana mikono yake ilikuwa busy kuizuia ile baiskel kubwa na chakavu aina ya Avon au maarufu Kama Anitha kama wengi wanavyo penda kuziita baada ya mwanamuziki wa Ubongo wa fleva kutoa ile hit song ya Anitha. Basi nikasogea nakumuomba Mamdogo nimsaidie kushikiria iyo baiskel, akasema, "Nashukuru mwanangu maana mikono yangu ilikuwa tayari imeisha nguvu"
Mamdogo akasogea pembeni kidogo nikaikamata baiskel ile chakavu iliyojaza mikungu kadhaa ya ndizi Mzuzu zilizo komaa wataalamu wa ndizi uziita Ndwanga...!!

"Jamani Mimi nipo ndani huku"
"Sawa Dada"
Mamdogo aliaga nakuingia zake ndani huku Mimi nikibaki na uyu jamaa  msomba ndizi, tulipomaliza kutelemsha mikungu yote na wakina Baba wakawa wanafika muda uo huo ilikuwa tayari ni saa moja kasoro. Tukasaidia kuingiza store mikungu yote kisha tukaingia zetu ndani kusubiri Chakula cha usiku.
Wakati tunakula nilimsikia Baba akimwambia Mama kuwa wamepata Nyumba nzima yakupanga maeneo ya jilani tu hapa japokuwa ilikuwa ni ubarozi mwingine kwaiyo dalali kasema tusubiri baada ya siku mbili ili Mwenye Nyumba atoe toe vitu vyake. Mama akasema sawa mradi isiwe kwenye unyevu nyevu maana Baba Tizo wee unajua masika jinsi Mbingu panavyokuwa unyevu unapanda mpaka juu kabisa ya kwenye msingi wa Nyumba. Baba akasema kuwa anamkubali sana yule Dalali anayejiita BK Dalali, hawezi kumpa Nyumba mbaya mbaya.

Basi maisha yaliendelea huku Bamdogo akiendelea kumfaidi Mamdogo zile siku za mwanzo mwanzo wazungu uziita Honeymoon. Atimaye ilifika siku na ndipo Mamdogo na Bamdogo wakaondoka nyumbani kwetu nakwenda kwenye Nyumba yao ambayo mali ya mzee Mnora ambaye ni bwana mifugo hapa Mbingu ana Nyumba nyingine nyingi tu ila aliyopanga Bamdogo ndio ilijegwa kisasa zaidi, basi Mamdogo sakina aliomba awe anakaa na Mdogo wangu akike Mdogo Sauda ambaye alikuwa yupo Darasa la tatu ikawa ndio ivyo, maisha yakaendelea huku Mzee mzima naendelea kupiga kitabu na kila Annual Examination Mimi nilikuwa nabukua tu huku nikifuatiwa na rafiki yangu Amani Kainga aliyekuwa anaishi mashambani huko Nyangudi, alikuwa anajitahidi sana maana ni mbali alafu masika kunakuwa na maji mengi sana na matope lakini rafiki yangu hakukata tamaa.

Basi baada ya wiki kadhaa, Bamdogo alikuja nyumbani nakuaga kuwa anasafiri kwenda Tabora kwenye biashara zake maana hapa Mbingu yeye ni mgeni hajui mchongo wowote zaidi ya kilimo, basi Baba akamwambia hakuna tatizo ila ni bora abebe chochote toka hapa Mbingu apeleke huko TABORA  kama kikilipa basi iwe Ndio biashara yake iyo kila aendapo TABORA. Basi Bamdogo akachukua Samaki wakavu wakutosha Kama wa Laki tatu ivi ambao kwa hapa Mbingu ni wengi sana Kama tenga nne ivi tena wakiwa wamepasuliwa kwa jina lingine wanaitwa baibai.
Basi alifuatilia kibali Kama siku tatu toka mamlaka usika ili asije kusumbuliwa na mali ya siri njiani, alipoona anazungushwa zungushwa alitamani aghaili alafu mzigo aupige mnada ata kwa hasara lakini Baba akamwambia;

"Kufanya ivyo sio sulusheni, Unatakiwa utoe pesa ndugu yangu ivi wewe unadhani lushwa imeisha nchi hii..? Lushwa imeisha  kwenye radio, Television, na midomoni mwa watu hasa wanasiasa. Sasa endelea kusubiri upate icho kibari bure bure uone Kama Samaki ujawamwaga wote ikawa mali ya mbwa na paka, wee mshike mkono mtendaji uone..!!"

Basi baada ya Bamdogo Erasto kupata ilo wazo akalifanyia kazi, kisha akarudi nyumbani nakumwambia Baba kuwa kafanya kama alivyo mshauri anasubiri majibu. Baba akamwambia kesho unapewa kibari chako utaniambia.
Kweli kesho yake ilipofika mida ya saa sita tu mwakipesile ambaye Ndio mtendaji alifika nakumpa vibari vyote vya biashara yake ya Samaki wakavu ambao wanafaa kabisa kuvuliwa kwa njia sahihi nakuuzwa.

Basi siku ya jumanne Bamdogo alipeleka Samaki Tazara kwa ajili yakuwafanyia Booking akawaacha hapo hapo Tazara maana Trein ilikuwa inapita usiku..kidogo, tulikaa nyumbani tukipiga piga mastory Mama aliniambia niende kulala sababu asubuhi natakiwa kwenda shule, ila Mimi nikamwambia wala usijali Mama ile ni mission shule ya gharama hakuna habari zakuhesabu namba pale Kama shule za buku buku izi za zinazoitwa za bure alafu elimu yenyewe hakuna..!!
Basi wote wakacheka pale ndani ila Mamdogo yeye alitabasmu tu kidogo, basi Baba akaniambia;
"Usiache mbachao kwa msara upitao, wewe Mwenyewe umesoma huko primary mpaka umefaulu vizuri nakufika hapa."
"Baba bidii na juhudi zangu zakujisomea Ndio zilisaidia Kama ni walimu mbona wenzangu walifeli wengi sana..!!"
Nikamjibu Baba huku nikiwa na furaha, Muda uo huo Bamdogo akasema kuwa ni saa  tatu na dakika 48 inamaana ni saa NNE kasoro. Basi ikabidi tuanze kusogea Tazara ili bamdogo akasimamie Samaki wake wanapopakiwa ndani ya Lageji....Ile tunafika tu Tazara kuli mmoja akagonga kengere kuashilia Trein ndio imetoka Mgeta tayari kwaiyo kila mmoja akaye tayari waliombali wasogee sogee......!!

Tunasonga wazee na ili dubwana....

                 ____ITAENDELEA____

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.