Notification texts go here Contact Us Buy Now!

MOYO ULIOJAA MAUMIVU SEHEMU YA 44

MOYO ULIOJAA MAUMIVU

SEHEMU YA 44

Theo hakuwa na habari, alifika mahali hapo kwa kazi moja tu. Aliwaona wanawake wote kuwa sawa, kichwa chake kilikuwa na mawazo juu ya familia yake na yale mambo yote ambayo walikuwa wakipitia.

Kushuti video hiyo ilichukua saa nne ndipo wakapumzika kwa ajili ya kupata chakula. Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi ya Iyanya kumfuata mwanaume huyo na kutaka kuongea naye. Haraka sana akasimama alipokuwa na kuanza kumsogelea.

Wapambe wake walipomuona, wakamzuia lakini Theo akawaambia wamuache kwani kusingekuwa na tatizo lolote lile kama angekaa na msichana huyo na kuzungumza naye.

Kwa Iyanya hiyo ikaonekana kuwa kama bahati, alikuwa na nafasi moja maishani mwake, nafasi ambayo ingempa hatma ya maisha yake kwa mwanaume huyo, hiyo nafasi alitakiwa kuitumia kwa umakini sana, yaani kama angeshindwa hiyo, basi asingeweza kupata tena.

Alimwangalia Theo, akamsogelea na kukaa karibu naye huku wakila. Moyo wake ulikuwa na furaha mno, alimpenda mwanaume huyo kupita kawaida, alitamani kumwambia kile kilichoujaza moyo wake muda huo lakini akaamua kutulia kwanza.

“Hii ni nafasi ya bahati sana kuwa katika video yako,” alisema Iyanya huku akimwangalia mwanaume huyo ambaye kwa mbali alionekana kutokuwa sawa.
“Kwa nini?”

“Wewe ni maarufu sana. Nadhani kupitia video yako nitakwenda kupata jina,” alisema Iyanya huku akiachia tabasamu pana, kwa jinsi alivyokuwa mzuri, uzuri wake ukaongezeka maradufu.
Theo hakujibu kitu zaidi ya kuachia tabasamu tu.

Alimwangalia msichana huyo, ni kweli alikuwa mrembo lakini hiyo haikuwa sababu ya kutaka kulala naye kwa sababu alijiheshimu sana, kubwa zaidi alimuheshimu mno mke wake.
“Theo! Ninahitaji msaada wako!” alisema Iyanya huku akimwangalia Theo.
“Msaada gani?”

Maoni 1

  1. Mpenzi wangu aliachana na mimi, najua ilikuwa kosa langu ambalo lilimfanya aachane na mimi, akanipata nikiongea juu yake, kuna kijana niliyemwita rafiki yangu alinivuta na kufanya naye mapenzi kisha mpenzi wangu akatushika, basi aliachana na mimi, ninampenda sana, nilifurahisha kwa wiki na miezi hakukubali kunikubali, nilikuwa nikisoma mkondoni jinsi ya kumrudisha mpenzi wangu basi nilikuta na makala juu ya jinsi mwanamke alirudi Mumewe aliyempa talaka, alisema kuwa Dk Lomi amsaidia alifanya sala kadhaa na mumewe amerejea kwake, basi na mimi nikawasiliana na Dr Lomi na kuelezea kile kilichotokea kisha akanisaidia kufanya maombi kadhaa na mpenzi wangu akarudi akiniombea alijuta kuwa bado ananipenda na leo tumerudi pamoja na naahidi kamwe hatutazungumza juu yake na leo tunafurahi, ikiwa unahitaji pia Msaidizi wa Dk Lomi kuwasiliana naye kwenye Line ya nambari ya WhatsApp; +2349034287285 unaweza pia kumtumia barua pepe; lomiultimatetemple@gmail.com kwa msaada
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.