Mahitaji:-
🔽Maziwa ya lozi au ya ng'ombe kikombe 1
🔽Majani ya chai vijiko 2 vya chakula
🔽Siagi 1/4 kikombe
🔽Sukari 3/4 kikombe
🔽Ndizi mbivu 1 ilopondwa
🔽Vanilla kijiko 1 cha chai
🔽Mafuta ya kula 1/4 kikombe au ya nazi
🔽Unga wa ngano kikombe 1 3/4
🔽Baking powder kijiko 1 1/2 cha chai
🔽Baking soda kijiko 1 cha chai
🔽Hiriki ya unga 1/2 kijiko cha chai
🔽Chumvi 1/2 kijiko cha chai
🔽Kungu manga 1/2 kijiko cha chai
MATAYARISHO NA NAMNA YA KUPIKA :
1. Washa oven joto 180°C. Paka chombo cha kuokea siagi au mafuta. Weka pembeni.
2. Pasha maziwa moto jikoni hadi uone yanaanza kutokota tia majani kisha zima na wacha majani yakoe kwa muda wa dk 10. Chuja wacha ipoe
3. Piga siagi na sukari kwa mchapo hadi mchanganyiko uwe mweupe. Tia mafuta ya nazi na ndizi kisha koroga vizuri kuchanganya.
4. Tia chai ilopoa na vanilla kisha koroga vizuri kuchanganya. Katika bakuli lingine changanya unga, baking powder, bakinh soda, spices pamoja na chumvi hadi vichanganyike vizuri.
5. Mimina mchanganyiko wa siagi katika mchanganyiko wa unga na koroga taratibu kuchanganya vizuri hadi mchanganyiko uwe smooth.
6. Mimina mchanganyiko wako katika chombo cha kuokea ulichoanda kisha tia katika oven na oka kwa muda wa dk 50 hadi saa au hadi ukichoma kijiti kati kitoke safi.
7. Acha keki ipoe katika chombo chake kwa muda wa dk 10, kisha itoe acha ipoe kabisa.
8. Keki yako tayari kwa kula. Enjoy!