Story: Sehemu ya 01
-------------------------------------------
Baada ya miaka Saba nilikutana na mama yangu mzazi...
Sikujua Kama ndie Alie nizaa sababu baba na mama walitengana nikiwa mdogo na mama kurudi kijijini kwao alikozaliwa..
Lilikuwa tukio la ajabu maishani kwa sababu sikuwahi kujua Kama mama alikuwa hai
Sababu toka nakua nakupata utambuzi sikubahatika kumuona mama kabla..
Nilikuwa nikipata simulizi Kutoka kwa malehemu Bibi kuhusu mama lakini hakuwahi kunieleza alipokuwa...
Siku zote furaha ya Bibi ilikuwa kuniona nikiwa salama Mikononi mwake
Mara zote alinipamba kwa maneno mazuri mazuri maneno yaliyonipa faraja Hadi kupelekea kuamini kuwa Bibi ndie aliekuwa mama yangu mzazi...
Nikiwa porini siku moja mvua Kubwa ilinyesha pale kijijini huku Miungurumo ya Radi ikitawala Kila mahali miyale ya umeme wa Radi ikipiga huku na Kule kuashiria uwepo wa mvua Kubwa siku hiyo..
Nikiwa nimekaribia nyumbani kishindo Cha ajabu kilisikika huku wingu la Moto likishuka toka Mbinguni kuifunika nyumba ya Bibi..
Mwili wangu ulikuwa umelowa kwa mvua nilitetemeka Kama mjane aliepatwa na subiani Meno yaligongana mfano wa sahani huku macho yangu yakishuhudia wingu Kubwa la Moshi likitoka ilipokuwa nyumba ya Bibi..
Sikuamini macho yangu kwani nyumba yetu ilikuwa imepigwa na Radi iliopelekea kuungua kwa nyumba nzima..
Nilijikaza kwa mwendo wa udadisi ili kujua kilichokuwa kimejiri pale nyumbani lakini sikuweza kupenya mlangoni Kutokana na Moshi mzito ulioenea pale...
Ukelele ulioambatana na ukichaa wakutokuelewa kilicho mbele ya macho yangu ulinitoka ghaflaa huku Nguvu za ajabu zikinijia...
Nilitimua mbio nisijue pakwenda huku utelezi nao ukipambana kuzuia Safari yangu..
Hatua chache nilikuwa tayari mbele ya nyumba ya mzee Martin Keilembo..
Sauti ya kuomba msaada ilitangulia madai yangu ya msingi nilitamani kumnusuru Bibi yangu na ule Moto sababu nilijua kweli alikuwa ndani ya ile nyumba...
Kisingiti Cha mlango wa mzee Martin kilinikwaa ghaflaa nikawa sebureni katika nyumba ya mzee Martin..
Naikumbuka kauli yangu ya mwisho nilisema Bibi amefariki japo sikumbuki Kama niliimalizia kauli hiyo kuitamka..
Kumbe nilizirai nakupoteza fahamu sikujua kilichotokea baada ya hapo...
Nikiwa katika zahanati ya Kijiji nilianza kurudiwa na fahamu lakini sikuwa na nguvu za kunyanyuka kutokea pale usingizi wa ajabu ulinivaa nakumiliki mamlaka ya mwili wangu..
Nilianza kuona kundi Kubwa lakina mama waliovalia nguo nyeupe huku ngozi zao zikimeta kwa mfano wa nyota ya Jaa..
Nilitamani kumjua mmoja wao lakini haikuwa bahati sababu japo nyuso zao zilikuwa za binadamu lakini miili Yao ilikuwa ya kioo cheupe...
Nilijitahidi kutaka kumkamata mmoja wao ili niongee nae lakini haikuwa kazi nyepesi kwangu sababu Kila nilipo jitahidi kuinuka pale mwili ulikataa..
Ghafula Lile kundi lilipotea machoni kwangu kwa mbali walianza kusogea vimwali wa Mbinguni huku wakitembea mwendo wa kimiss...
Macho yangu yalibaki kulitazama kwa umakini Lile kundi ghafula nilianza kuona sura ya mtu nilie mtambua huku akiwaongoza wale mabinti wa Mbinguni kuja kwangu..
Hakika walipendeza kwa mavazi ya hariri huku vifua vyao vikibaki wazi
Chuchu zao zilichongoka mithiri ya soli ya kiatu Cha mcheza blues..
Sikuhitaji mkalimani kumtambua aliekuwa mbele yangu japo Sasa alikuwa katika umbile lake halisi la usichana wa miaka ithna ashara..
Alisogea karibu yangu huku akinyoosha mikono yake kunisogerea..
Sauti ilitoka nyuma ikimkemea Yule mtu huku ikisema miili ya udongo na Maji haishikani na miili ya Nuru na Moto daima ispokuwa kwa udugu wa Mauti..
Huyu alikuwa ni mjane wa mzee Kamgisha bi Kemilembe ambae daima alinilea kwa nafasi ya mwanae Sasa nilikuwa nikimshuhudia katika ndoto...
Nilijitutumua kutaka kumkamata lakini haikuwa rahisi..
Ghafula nishtuka Kutoka usingizini nilipoangalia pembeni walikaa watu wawili ambao walikuwa ni manesi mmoja alimwambia mwenzie muite Dr haraka naona Amezinduka..
Sikujua kilichotokea Hadi Mimi Kuwepo pale lakini nilikumbuka baadhi tu ya matukio..
Baada ya hapo aliingia Dr na vipimo vyake Kisha akawa anaongea na wale nesi hatmae nikapewa ruhusa ya kuonana na ndugu zangu..
Pale kijijini sikumjua ndugu yeyote zaidi ya Bibi hivyo nilitegemea kumuona akiingia lakini haikuwa hivyo Bali waliingia majirani huku mke wa mzee Martin Keilembo akiongoza msafara..
Nilijiuliza kulikoni Bibi akose pale?
.........................
SEHEM 02:
---------------------------
Nilikuwa siamin macho yangu nilihisi mazonge moyoni mwangu
Lakini tabasamu la mke wa mzee Martin lilinipotezea huzuni chungu niliokuwa nayo..
Sauti nyororo iliobeba kitetemeshi Kama vibration ya Itel ilimtoka mama Martin pole mwanangu lilikuwa ni Neno la awali kuliskia Japo pole yake haikuwa na majibu sawia na hisia zangu..
Kabla ya kuitikia pole pole nilijikuta na Muuliza Mke wa mzee Martin alipo Bibi maana haikuwa kawaida kwake kukosekana katika dhiki zangu...
Nyamaza Kwanza Asmah Bibi yako utamuona...
Nilijibiwa hivyo huku uso wa Mrs Martin Keilembo ukikunja ndita ghafla hatmae mifereji ya machozi iliota kwa wote waliokuwa pale..
Nilijiuliza kulikoni lakini moyo mganga nilijua wazi familia yetu ilikuwa imepatwa na Janga...
Ukakasi ulinikamata moyo haukuweza kuhesabu nilianza kuhesabu idadi ya matukio katika maisha yangu..
Kabla ya kuja kijijini nilikuwa na kumbuka kuwa niliishi na baba Kule Nzega mkoani Tabora japo sikumbuki vyema ni lini baba na mama walikuwa wametengana lakini naikumbuka vyema siku ambayo baba alinileta kijini kwa Bibi..
Tokea siku hiyo sikuweza kumuona baba ispokuwa baada ya miaka miwili nikiwa natoka Shule wakati huo nakumbuka nilikuwa darasa la tatu pale Shule ya msingi Rwihja..
Gari mbili ziliongoza msafara na hatmae ziliweka Nanga mlangoni kwa Bibi..
Kumbe hata Bibi hakujua lengo la ule msafara Hadi pale alipo shuka kijana mmoja ambae kwa hisia zangu alikuwa kiongozi wa msafara ule..
Alisogea pembezoni kidogo huku akimshika mkono Bibi na kumsogeza pembezoni mwa ukuta wa nyumba yetu..
Naamini Yule mwanaume alimpa report kuhusu kifo sababu baadae Bibi alisikika akitoa ukelele wa Nguvu ambao mwangwi wake ulikikusanya Kijiji kizima kwa ukelele ule ambao kwa masikio yangu haukutafautiana sana na ile khadithi ya siku ya qiyama siku smbayo Israfilu atalipuliza baragumuu na walio hai wote kufa na wafu nao kuonja uhai kwa Mara nyingine..
Ule ukelele uliamsha hisia za wakazi wa Kijiji Cha Irumndu...
Kina baba na kina mama wa Kila Rika walianza kukusanyika pale nyumbani huku maskini Bibi Mrs Kamgisha mjane wa Babu Kamgisha akijipinda pinda ungedhani Joka la midimu Kule unyamwezi mitaa ya Kaliua..
Baada ya maombolezo maisha yaliendelea Kama kawaida na Sasa rasmi nilijua kuwa baba yangu hakuwa hai tena lakini Bibi yangu mara zote aliniambia uwepo wa mama japo hakujua wapi aliko lakini kulingana na taarifa ilisemekana kuwa mama aliolewa na mwanaume mwingine na Hatimae alipelekwa nje ya nchi..
Hivyo maisha yangu yote nilitamani kuonana na mama japo masaa mawili na hasa pindi majanga yalipo nikabili..
Baada ya kurejea Nyumbani nilikutana na umati wa watu ambao wengi niliwatambua lakini wengine sikuwahi kuwa nimewaona hapo Awali..
Ulikuwa ni msiba wa Kijiji msiba wa mama mjane aliefiwa na mmewe miaka sita iliopita Sasa zamu ya mwili wake kuungana na kundi la marehem wateule ilikuwa imekamilika..
Nilianza kuangaza huku nakule ili kujua kulikoni mkusanyiko ule pale nyumbani
Nguvu za mwili zilianza kuniisha mapigo ya moyo hayakuwa na speed governer tena kuweza kuzuia Hali ile nilihisi ubaridi wa ghafra huku nyota na vichwa vyake vikianza kuifunika Nuru ya macho yangu..
Mikononi mwake Mke wa mzee Martin sikuweza kufurukuta Bali ilikuwa ni haki ya macho yangu kushuhudia mwili ulio lala pasina roho juu ya kitanda tulichokilalia Mimi na Bibi Sasa nilikubali dhahiri ule hakika ulikuwa mwili wa Bibi umelala juu ya kitanda pasina roho..
Sikuwahi kushuhudia maiti kwa Umri wangu ilikuwa ni hatua nyingine ya kitaaluma kushuhudia maiti..
.............................
SEHEM Y A TATU #3
''
Baada ya mazishi na kukamilishwa taratibu zote za matanga watu walitawanyika huku wengi wakiondoka pale kwa Imani kuwa familia yetu ilikuwa yenye Raana sababu vifo vilivyotokana na Radi watu waliamini wazi kuwapo kwa maapizo ya mizimu hivyo kifo Cha Bibi ilifanywa kuwa laana
Niliyaanza maisha mapya japo midomo yangu na macho vilivimba kwa sababu ya kilio Cha Bibi..
Hapakuwa na shida ya chakula wala kuni na Maji sababu watu walichangia Kila kitu ili kufanikisha msiba wa Bibi...
Ndugu waliokuja ni wa upande wa Bibi sababu pamoja na yote lile shamba ilikuwa Mali ya bibi baada ya kikao Cha familia nilikabidhiwa nguo za marehem Bibi shambani nilitakiwa kuondoka baada ya kuhitimu tu masomo yangu ya darasa la Saba..
Sikujua wapi ningeayaanzia maisha lakini niliamini Kama ningefiika mkoani mwanza Basi uenda ningeweza kukutana na mama mzazi sikuhisi Kuwepo kwa ndugu mwingine baada ya kifo Cha Bibi kutokea..
Safari ya kwenda mwanza ilikuwa ni ngumu kwa upande wangu sikuwa na Nauli mfukoni mwangu sababu hata zile rambirambi nilizopata baada ya msiba nilizitumia kugharamikia mtihani wa darasa la Saba..
Nilianza safari ya Kutoka kijijini mida ya saa 10 alfajir kuelekea Bukoba mjini..
Nimwendo wa kilometers 45 Kutoka kijijini kwetu
Sikuwa namna tayari nilikwisha dhamiria kufika mwanza...
Nilitembea kwa kasi Sana nikipitia katika mabonde na miinuko huku msitu mkubwa wa nyabururu nikiuacha kwa umbali kabisa na mapambazuko..
Akili yote ukisema mwanza Mwanza ikawa ndio agenda Kubwa kwangu nilianza kuhisi wimbo wa leyvani ule wa nyegezi nyegezi ukijirudi kwenye hisia zangu..
Ni saa Tisa mchana nimesima pembezoni mwa barabara itokayo kyaka mwili wangu ukiwa umenyongeya kwa safari nilijisogeza katika mti uliokuwa karibu ili nipate mapumziko sijui ni wakati gani usingizi ulinikamata nikiwa katikati ya ndoto ya ajabu nilihisi Hali ya unyevu nyevu katika mwili wangu kwa kuwa nilihisi kuhitaji Maji ubaridi nilio utaraji uliambatana na harufu ya mkojo ghafla nilifumbua macho yangu sikuamini kilichokuwa mbele yangu...
Yowe likinitoka mzee wa makamo alievalia maridadi nae alipatwa na mshutuko baada ya kugundua sehemu aliyoitumia kutimiza haja zake palikuwa na mtu..
Alionekana ni afisa mkubwa tu kwa muonekano japo siku hiyo alionekana kujaa henghover kichwani lakini tahayari iliompata ilimfanya kuwaita wasaidizi wake ili kushuhudia Lile tukiio..
Ulipita usaili mfupi na Hatimae Yule mzee aliniambia niambatane na msafara wao sikujua wapi msafara ule ungeishia nilipanda katika Lile gari liloonekana ni gari la gharama fridge na tv ilikuwa ni sehemu ya gari Lile na Kila Jambo ndani ya Lile gari lilifanyika kwa wireless Signal...
Ndani ya Lile gari ungeweza kuwasliana na watu mbalimbali na kufanya vikao tofauti kwa watu walio mbali..
Ubao uliandikwa karibu wilaya ya Misenyi ulisomeka machoni pangu Sasa ni dhahiri nilijua kwa hakika safari yetu uwenda ingetufikisha Uganda au Karagwe..
Nisingeweza kuuliza Jambo sababu wote ndani ya gari waliongea kingereza muda wote ni Mara chache Yule mzee aliniongelesha kihaya hasa tulipowaona wachuuzi wa nyama na ndizi za kichoma..
Kadri safari ilivyoendelea nilianza kuwajua wale abiria ndani ya gari ni Dreva aliemwita Yule mzee nami kumjua kuwa jina halisi la Yule mzee ni Mr Kamzora..
Usiku ulianza kuingia lakini wakati huo tayari tulikuwa mpakani mtukura..
Nilitolewa ndani ya gari sikujua wapi Sasa nilikuwa napelekwa lakhauraa kumbe ilikuwa ni hatua muhimu kufanyiwa shopping ya Mavazi katika maduka ya pale
Baada ya muda mfupi sikutafautiana sana Prince Charles au Lily Wine Mr Kamzora alionyesha kufurahishwa na namna nilivyokuwa nimetokelezeaa huku mashindano ya Sulfie bila Kikomo yakitawala ndani ya gari Lile..
Mr Kamzora alimtaka dereva kuhakikisha tunafika mkoa wa Masaka ili tuweze kulala pale na mapema tungeingia Kampala..