Notification texts go here Contact Us Buy Now!

KUNA AINA MBILI ZA MAARIFA

KUNA AINA MBILI ZA MAARIFA.

Na Thadei Ole Mushi.

Kuna aina mbili za watu SMART yaani kuna aina mbili za maarifa yanayomfanya mtu Smart.

Kuna kitu kinaitwa BOOK SMRTS na STREET SMARTS.

Book Smarts ni maarifa unayoyapata vitabuni. Mara nyingi haya ni Yale maarifa waliyoanayo wasomi mbalimbali wa ngazi za juu.

Tatizo lolote linalokuja mbele yake mpaka afikirie principle aliyowahi kuisoma kwa lengo la kutatua tatizo husika.

Mara nyingi akishindwa kutatua matatizo au kutafsiri mambo ambayo yapo mbele yake hukimbilia kwenda kuchukua degree nyingine ya juu. Kama alikuwa na Masters anawaza kuchukua PhD.

Watu wa aina hii hawana Tabia ya kuimprove Skills walizonazo. Ndio maana Graduate aliyepo karibu na garage ya magari hajawahi hata siku moja kwenda kujifunza namna ya kufunga Tairi.

Kuna maeneo huwezi kutumia Book Smarts ukatoka lazma ujaribu aina nyingine ya maarifa ili ufanikiwe.

Mara nyingi Book Smarts yaani waliofaulu vizuri Darasani wasipoajiriwa wanapotea kabisa mtaani. Na hawa ndio wanaotoa vichaa wengi masokoni kama hawataajiriwa yaani matarajio na ndoto zao kama hazikutimia basi ni Rahisi kufyetuka chap na kukimbilia Sokoni kuokota uchafu. Hujawahi kusikia kila kichaa unayeonyeshwa unaambiwa alikuwa vizuri Darasani?

Street Smarts ni Yale maarifa unayoyapata mtaani na yanakusaidia kupambana na mazingira   au yanakusaidia kuyatafrisi na kuyapambanua mazingira yanayokuzunguka.

Ni maarifa yanayokuletea kashikashi lakini yanakupa na njia za kuzitatua.

Mtaani kwako kuna watu wengi sana wana hii Street Smart. Kila siku unawaona mambo yao yanaenda na hujui wanapata wapi fedha.

Maisha yao hayana Kanuni na kwa muonekano ni marahisi sana japokuwa yanahitaji maarifa mengi sana.

Leo utamuona na Mayai ya Kuuza Kesho ana bajaji tatu za kukodisha keshokutwa ana kakibanda cha kuuza Simu nk.

Kwa kuwa Mimi na wewe tuna Book Smarts na hatuwezi kushindana nao mtaani tunaamua kwenda kusoma tena shuleni. Tunarudia principle zile zile za Kitaaluma na kupata A kibao.

Tunarudi tena Mtaani.... Tunakuta hali ni ile ile.

Ukichunguza Sana kwenye maisha Street Smarts ni mabosi wa Book Smarts kwenye maeneo mengi. Yaani Street Smarts kama wapo serious hufanikiwa mapema kuliko Book Smarts na hivyo waliosoma sana hubisha hodi kwa hawa wahuni wa mtaani kuomba kazi.

Nataka kusema nn?

Kwanza sidiscourage wanaosoma na wenye maarifa ya Darasani yaani ya kwenye vitabu. Nachotaka kukisema ni vizuri ukachanganya maarifa uliyonayo yaani uwe na ya Darasani lakini usidharau ya mtaani.

Hii naandika kwa ajili ya vijana wanaograduate. Msijitenge na vijana wa mtaani wana maarifa Mengi sana ya kuwavusha kwa haraka kuliko kusubiri ajira.

Kaeni nao na shirikini shughuli za kujiingizia kipato walizonazo huko mtaani. Msiogope kuchoma nao mishikaki, msiogope kukamua nao Juice za Mua, msiogope kufungua nao vibanda vya MPesa.

Kaeni nao kwenye vijiwe vya kuchomea grills kwa kuanza wasaidie kutafuta maua na design nzuri kwa Ku google wewe si unaaccess ya mitandao? Wale Dada zangu wafuateni kwenye Saluni zenu za Kike wasaidieni Kazi wapeni misuko mipya kwa kuitafuta kila mahali. Msiwaache wenyewe kwenye masoko makubwa makubwa nendeni nao kila mahali hata kule feri kwenye kukangua Samaki na kutafuta wateja wa Samaki.

Fungueni vikampuni vidogo vidogo vya Usafi kwenye ofisi za Umma kama mabenk, jifunzeni kupamba, jifunzeni kupika na mfungue vikampuni vidogo vidogo vya upishi nk.

Huku mtaani ukija huko na Degree zako utalalamika kila Siku. Ni kweli kuwa Mimi Ni mwajiriwa lakini kabla ya kuajiriwa nilifanya haya na nilikuwa na kipato haswa. Nimepoteza Yale maarifa nasubiria wanikamue kwenye asilimia 25 za kustaafu.

Kwa kufanya hivi ajira inaweza ikaja ukaikataa ukaendelea na Mambo yako yanayokuingizia Kipato.

Ni aibu kwa Graduate kila siku kulipiwa round ya bia na STD Seven. Msikumbuke mliyoyasoma sana Darasani, maisha hayapo sana vitabuni.

Zile Ndoto ukizokuwa unaota za Kuzunguka kwenye Ofisi zenye viyoyozi sahau sasa. Ongezeni maarifa ya darasani kwa hawa vijana wa mtaani.

Leteni ubunifu kwenye maarifa ya mtaani mtatoboa haraka sana.

Wewe uliyemaliza Chuo na bado huna Kazi tafuta mwenye Street Smart aliyekaribu na wewe mfanye awe Rafiki na mfanye akuonyeshe njia.

Ukiishi kwa kujiita Msomi utapata shida sana katika zama hizi ambazo ajira zimekaba. Kuweni na Local Knowledge itawasaidia sana na Mara nyingine ina faida kuliko hata degree ya Sheria ya pale Mlimani.

Marafiki zangu wakuu ni wachache sana ambao ni Book Smart wengi ni Street Smart. Hawa wajamaa wanaishi Simple sana na wanapendana. Wanapenda kunitania wewe si umesoma bhanaaa. Lakini hawamaanishi ni utani tu. Wapo vizuri sana na si wachoyo.....

Mfowardie graduate yeyote ambaye yupo mtaani anapambana na kutafuta ajira.

Ole Mushi
0712702602

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.